Magufuli, a one man show nani atamfunga speed governor akikosea?

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Kinachonifariji na kunipa nguvu za kuendelea kuandika ni yale maneno yaliyotamkwa na mwandishi maarufu wa vitabu wa zamani wa Marekani, Mark Twain, kwamba andika lakini usiogope shutuma au kulaniwa (write and be condemned). Nitaendelea kuandika kwa kuwa niko tayari kukosolewa, kushutumiwa na kulaaniwa.

Pombe Magufuli ni mtu mwenye maamuzi ya pupa na ya jazba, na hivyo anahitaji mtu wa juu yake mwenye mamlaka zaidi wa kumdhibiti na mtu huyo ni rais! Hebu fikiria mtu wa namna hiyo akiwa yeye mwenyewe ndiyo rais! Hata kwenye zama zake za uwaziri, John Pombe Magufuli hakupata kunisisimua kuwa ni presidential material.

Nimekuwa nikifuatilia utendaji wake kwa muda mrefu, na nadiriki kusema kwamba John Pombe Magufuli ni mchapakazi hodari lakini mwenye kasoro kadhaa kubwa za kufanya maamuzi ya pupa, kuzomoka na kutoa kauli tata hadharani bila kwanza kupima athari zake. Kauli hizo ni kama ile ya kuwaambia wana Kigamboni wapige mbizi kama hawataki kulipa nauli mpya ya kivuko! Kwenye urais hafai; maana anahitaji ufungwa gavana na viongozi wengine wa juu zaidi yake yeye yaani waziri mkuu au rais. Uzoefu unaonyesha kwamba, wakati wa uwaziri wake, kazi hiyo ya kumfunga ?gavana? ilifanywa (si mara moja au mbili) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda au Rais Kikwete mwenyewe.

Labda nitoe mfano mmoja unaohusu suala lile alilolivalia njuga mwaka 2011 la bomoabomoa ya nyumba zilizowekwa ?X? kwa kujengwa katika maeneo ya hifadhi ya barabara, Itakumbukwa kwamba Magufuli aliielekeza Tanroads kupima barabara zote kuu nchini na kuwekea ?X? nyumba zote zilizojengwa katika eneo la hifadhi ya barabara hizo. Zoezi hilo la kitaifa lilitumia mamilioni ya fedha za walipakodi kulikamilisha. Na lilipokaribia kukamilika ndipo John Pombe Magufuli akaanza vitisho vyake kwa wote ambao waliwekewa nyumba zao ?X?.

Akawapa muda fulani wazibomoe wenyewe; vinginevyo zingebomolewa na matingatinga ya Tanroads bila ulipaji fidia. Waathirika wakaanza kulalamika na kutoa shutuma kibao kwa waziri huyo na serikali. Mfano mwingine wa pili ni wa tukio lile la mgomo ule wa wenye malori ya mizigo baada ya John
Pombe Magufuli kuagiza watozwe asilimia tano kwa kila lori litakalozidisha uzito. Wamiliki hao walikataa, na badala yake wakaamua kugoma.

Wakati mgomo huo ukiendelea, John Pombe Magufuli, akitiwa nguvu na sheria kuhusu tozo hiyo mpya, akatamba lazima wenye malori walipe tozo hiyo, na kama hawataki, wayaondoe malori yao barabarani na kuyaegesha majumbani mwao! Japo kweli tozo hiyo ipo kisheria, John Pombe Magufuli hakufikiria athari za kiuchumi kwa taifa kutekeleza agizo lake hilo kibabe. Baada ya mgomo wa wenye malori kuendelea kwa siku kadhaa na kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya pesa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akaingilia kati na kumpiga stopJohn Pombe Magufuli kwa kusitisha ulipaji wa tozo hiyo ya asilimia tano, na pia kuagiza pande mbili zikae chini kutafuta mwafaka - jambo ambalo Magufuli alilikataa mwanzoni.

Baada ya agizo hilo la Waziri Mkuu, mbwembwe, vitisho na jazba alizokuwanazo John Pombe Magufuli kuhusu tozo na mgomo huo wa wenye malori vikayeyuka haraka kama liyeyukavyo pande la barafu ukiliweka kwenye jua kali! Huyo ndiye John Pombe Magufuli mtu ambaye CCM imemuona ndiye anayefaa kuwa rais wetu mpya.

Na hapo, bado sijazungumzia kabisa mambo yake mengine yenye utata kama vile uamuzi wa kuuza nyumba za serikali na ule ya kukamata meli ya
samaki ya kichina bila utafiti wa kutosha au hata suala la uwezo wake mdogo wa kuleta mageuzi ya maana (reforms) ndani ya CCM.
 
haya nenda kachukue mshiko wa buku3 ya weekend kwa riz1 na January makimba.
 
gavana ya nini acha tu liende mbio tutatupia kigingi badae,

Wewe si ndio umeanzisha mada kuhusu nini serekali ifanye kuhusu ada za shule binafsi? Sasa huoni hata kule kwenye shule tusubiri tu tutaweka kigingi baadae. Mwenzio anapotoa maoni yake jenga hoja na sio kutoa maneno ya mchomeko bila kushauri vizuri. Ukumbuke hili jukwaa washauri mbalimbali wa rais wanapita na hata rais mwenyewe hivyo anapoona ushauri mzuri na wapi pana mapungufu anarekebisha. Kule kwenye mada yako umetoa angalizo zuri, je ni sahihi mtu kuchomekea tu wacha waisome namba kana kwamba ni suluhisho la mapendekezo yako? Jifunze kuwa muungwana hata kwa kitu usichopenda kusikia.
 
tindo umemtindua.
 
Pambaf. Tanzania tunamuhitaji Magufuli. Baba ritz kapiga pesa sana bila huruma na kuiacha nchi mufilisi. Ili TZ izaliwe upya tunamuhitaji mkereketwa Magufuli.
 
Safari hii ni kuteremsha kaptula mle sindando. Ungonjwa wenu kwa vidonge haiwezekani. Infection imesambaa sana. Kula dozi. Wacha kulalamika. Nenda JPM Nenda na KM nenda !!!
 
sio bure kwa ubongo inabidi umeze CD ya avast
 
Kinachonifariji na kunipa nguvu za kuendelea kuandika ni yale maneno yaliyotamkwa na mwandishi maarufu wa vitabu wa zamani wa Marekani, Mark Twain, kwamba andika lakini usiogope shutuma au kulaniwa (write and be condemned). Nitaendelea kuandika kwa kuwa niko tayari kukosolewa, kushutumiwa na kulaaniwa.

Pombe Magufuli ni mtu mwenye maamuzi ya pupa na ya jazba, na hivyo anahitaji mtu wa juu yake mwenye mamlaka zaidi wa kumdhibiti na mtu huyo ni rais! Hebu fikiria mtu wa namna hiyo akiwa yeye mwenyewe ndiyo rais! Hata kwenye zama zake za uwaziri, John Pombe Magufuli hakupata kunisisimua kuwa ni presidential material.

Nimekuwa nikifuatilia utendaji wake kwa muda mrefu, na nadiriki kusema kwamba John Pombe Magufuli ni mchapakazi hodari lakini mwenye kasoro kadhaa kubwa za kufanya maamuzi ya pupa, kuzomoka na kutoa kauli tata hadharani bila kwanza kupima athari zake. Kauli hizo ni kama ile ya kuwaambia wana Kigamboni wapige mbizi kama hawataki kulipa nauli mpya ya kivuko! Kwenye urais hafai; maana anahitaji ufungwa gavana na viongozi wengine wa juu zaidi yake yeye yaani waziri mkuu au rais. Uzoefu unaonyesha kwamba, wakati wa uwaziri wake, kazi hiyo ya kumfunga ?gavana? ilifanywa (si mara moja au mbili) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda au Rais Kikwete mwenyewe.

Labda nitoe mfano mmoja unaohusu suala lile alilolivalia njuga mwaka 2011 la bomoabomoa ya nyumba zilizowekwa ?X? kwa kujengwa katika maeneo ya hifadhi ya barabara, Itakumbukwa kwamba Magufuli aliielekeza Tanroads kupima barabara zote kuu nchini na kuwekea ?X? nyumba zote zilizojengwa katika eneo la hifadhi ya barabara hizo. Zoezi hilo la kitaifa lilitumia mamilioni ya fedha za walipakodi kulikamilisha. Na lilipokaribia kukamilika ndipo John Pombe Magufuli akaanza vitisho vyake kwa wote ambao waliwekewa nyumba zao ?X?.

Akawapa muda fulani wazibomoe wenyewe; vinginevyo zingebomolewa na matingatinga ya Tanroads bila ulipaji fidia. Waathirika wakaanza kulalamika na kutoa shutuma kibao kwa waziri huyo na serikali. Mfano mwingine wa pili ni wa tukio lile la mgomo ule wa wenye malori ya mizigo baada ya John
Pombe Magufuli kuagiza watozwe asilimia tano kwa kila lori litakalozidisha uzito. Wamiliki hao walikataa, na badala yake wakaamua kugoma.

Wakati mgomo huo ukiendelea, John Pombe Magufuli, akitiwa nguvu na sheria kuhusu tozo hiyo mpya, akatamba lazima wenye malori walipe tozo hiyo, na kama hawataki, wayaondoe malori yao barabarani na kuyaegesha majumbani mwao! Japo kweli tozo hiyo ipo kisheria, John Pombe Magufuli hakufikiria athari za kiuchumi kwa taifa kutekeleza agizo lake hilo kibabe. Baada ya mgomo wa wenye malori kuendelea kwa siku kadhaa na kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya pesa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akaingilia kati na kumpiga stopJohn Pombe Magufuli kwa kusitisha ulipaji wa tozo hiyo ya asilimia tano, na pia kuagiza pande mbili zikae chini kutafuta mwafaka - jambo ambalo Magufuli alilikataa mwanzoni.

Baada ya agizo hilo la Waziri Mkuu, mbwembwe, vitisho na jazba alizokuwanazo John Pombe Magufuli kuhusu tozo na mgomo huo wa wenye malori vikayeyuka haraka kama liyeyukavyo pande la barafu ukiliweka kwenye jua kali! Huyo ndiye John Pombe Magufuli mtu ambaye CCM imemuona ndiye anayefaa kuwa rais wetu mpya.

Na hapo, bado sijazungumzia kabisa mambo yake mengine yenye utata kama vile uamuzi wa kuuza nyumba za serikali na ule ya kukamata meli ya
samaki ya kichina bila utafiti wa kutosha au hata suala la uwezo wake mdogo wa kuleta mageuzi ya maana (reforms) ndani ya CCM.

...mbona siku hizi huishi kulia lia?!!
 
Haya tumeona umeandika,sasa tuambie unataka tufanye nini?
 
Umehama kuibeza cdm umehamia kumbeza magufuli. Sasa naamini ccm hawalali usingizi kwa anayoyafanya magufuli
 
Jipu lako kalipasua umeanza kuwewesekaweweseka khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee na hakuna wa kuzuia wimbi lake.
 
Mungu alimshusha,Adam,Musa,Ibrahim,Issa/Yesu na Mohamad,Mungu ameona shida ya
Watanzania kwenye maswala ya Uongozi,ameamua kumshusha Magufuli.Eee Mola tunanamuombea Makufuli ulinzi kutoka kwako Aminaaah.
 
Back
Top Bottom