Magu: Wavunja makaburi na kuiba misalaba, nondo

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mkuu wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Salum Kalli amekerwa na vitendo vya baadhi ya wananchi kuvunja makaburi na kutoa vyuma chakavu kama nondo na waya na kwenda kuuza.

Akiwa katika zoezi la Uzinduzi wa Anwani ya makazi Februari 20, 2022, DC Kalli ameagiza kusakwa na kutiwa nguvuni kwa wanaojihusisha vitendo hivyo mara moja.

DC Kalli amesema amesikitishwa na tabia hiyo isiyo na utu ndani yake na ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka kwa udi na uvumba na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria wanaojihusisha vitendo hivyo.

"Nimeagiza Jeshi la Polisi kuwashughulikia haraka na wafikishwe mahakamani na katika hili yeyote atakayehusika na tuhuma hizi sitokuwa na huruma hata kidogo, si uungwana hata kidogo kwenda kuwabughudhi wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki," alisema DC Kalli.

DC Kalli amefikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko toka kwa wananchi kuwa Makaburi ya Ndugu zao yamekuwa yakivunjwa misalaba, na nondo kuchomolewa vilevile baadhi ya makaburi yametinduliwa na kuachwa yakiwa wazi au mianya mikubwa na huku yakiwa yameharibiwa.

Aidha, ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza siku ya 26.02.2022 kwa ajili ya kufanya usafi katika makaburi hayo, ikiwa ni pamoja na kufyeka vichaka ambavyo vimekuwa ni maficho ya wahalifu.

Chanzo: Malunde
 
Dc wa Magu amekosa Kazi Za kufanya. Ded wa Magu Anafanya kazi gani anashindwa kuimarisha eneo la makaburi kwa kujenga uzio na kutumia vibarua kuweka mazingira sawa?
 
Ndo maana siku nimeenda kumzika ndugu yangu mahala pale mwanzoni mwa January, 2022 niliona kuna makaburi kadhaa yamepasuka nikastaajabu.

Lile kaburi la mke wa tajiri wa mabasi ya Batco limesalimika kwenye wizi huo?
 
Hili ni tatzo na tunatakiwa kuanzia kwa wauza madawa ya kulevya wakubwa na ndio tutamaliza hili tatzo.. vijana wengi wanaofanya hayo matukio wameharibikiwa na ulevi wa mihadarati vikiwemo vilevi vikali pombe, unga, mabange na vinginevyo
 
Tusipigane chenga hapa.Uchumi wa familia na mtu mmojammoja ni mbaya mnoo.Mzunguko wa fedha hauendani na mahitaji ya wananchi.Tushughulikie hilo kwanza.
 
Back
Top Bottom