Magombana anavowanyanyasa wanafunzi

daaa

Member
May 5, 2017
18
10
Uyu ni mwalimu wa chuo cha mount Meru University, yaani ni jipu kubwa hapa chuoni analazimisha wanafunzi wamchangie ukikataa anakufelisha, anang'ang'ania kufundisha course za mwisho ili awatie uoga wanafunzi kwa kuwafelisha,

Juzi tuu anawalazimisha wanafunzi wachange hela ya safari Bagamoyo usipotoa unakula sup, yaani ni shida kweli na uongozi wa chuo unajua na unamnyamzia tuu.
 
Uyu ni mwalimu wa chuo cha mount meru university, yaani nijubu kubwa apa chuoni analazimisha wanafunzi wamchangie ukikataa anakufelisha, anang'ang'a kufundisha couse za mwisho ili awatie uonga wanafunzi kwa kuwafelisha, juzi tuu anawalazimisha wanafunzi wachange ela ya safari bagamoyo usipotoa unakula sup, yaani ni shifa kweli na uongozi wa chuo unajua na unamnyamzia tuu
Eleza vizuri tukuelewe.
Magombana yupi weka full names yake!
 
Hili tatizo lilokuwepo hata chuo nilichosoma mimi, Lecturer analazimisha watu kununua vitabu vyake, kuchangia sherehe na hata kuchangia ziara, na anasema kabisa usipochangia tutakutana kwenye course work, kuna Lecturer mmoja alipoona vitabu havinunuliwi akasema atatunga maswali kutoka kwenye hicho kitabu, kitabu chenyewe hata kwenye course outline hakipo na wala hakuna mada inayolingana.

Mimi nilikuwa sina ujinga wa kuchangia michango ya kipuuzi, sijui mambo ya ada ya association ya somo fulani, sikuwa na mpango huo, nakumbuka kuna Lecturer aligoma kunisainia clearance form kwa sababu sikutoa ada ya association ya somo fulani, nikaondoka bila kusaini.

Tatizo kubwa lipo kwa viongozi wa wanafunzi, hata ukipeleka malalamiko kama haya hayafanyiwi kazi, wengi wao ndiyo wanakuwa wahamasishaji wakubwa kwenye mambo ya kuchangisha fedha.
 
Yaani uyu ni shida kila mwaka lazima afelisge watu kibao kwa sababu zake mwenyewe
 
Back
Top Bottom