barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kama Taifa, Na Katika Dunia Hii, Marafiki Zetu Wa Kweli Ni Wachina.Twendeni China.
Ndugu zangu,
Comrade Abdulhaman Babu ndiye aliyetupeleka China. Katika dunia hii, rafiki wa kweli ni yule anayekusaidia wakati wa shida na bila masharti. Nchi yetu ina changamoto nyingi kwa sasa. Ni shida zenye kuiumiza jamii kwa sasa; ni kuanzia kwenye elimu, afya na hata miundo mbinu.
Miaka ile ya 70 mwanzoni tulidhamiria kujenga Reli ya Uhuru kutuunganisha na Zambia. Wakubwa wa Magharibi tuliwafuata kuwaomba msaada, walikataa. Ndugu zetu Wachina walikuja haraka kutusaidia. Mifano iko mingi.
Comrade Abdulhaman Babu mapema kabisa alionyesha kuwa na mashaka sana na nia thabiti ya mataifa ya magharibi juu yetu. Wachina walimjua Babu hata kabla ya Mapinduzi.
Nimeandika, kuwa mwaka 1964 ulikuwa ni mwaka mgumu sana katika utawala wa Julius Nyerere. Mwalimu alikuwa rafiki wa JF Kennedy wa Marekani, lakini akalazimika kufanya maamuzi magumu kwenda China ya Mao. Leo tunajua, kuwa Mwalimu hakukosea.
Miaka ile ya mwanzoni mwa uhuru ina simulizi nyingi za kuelimisha, kuhuzunisha na hata kusisimua. Hayo unayapata vitabuni. Tusome historia yetu.
Maggid,
Iringa.