Maggid Mjengwa: Kuhusu mimi kumfahamu Ludovick

..sasa napata wasiwasi zaidi,more questions than answers...!
 
Kama ulivyosema haki na wajibu, tunaamini haki itatendeka kwa Ludovick na Lwakatare na wewe kama kutakua na wajibu wa kutimiza basi uwe tayari kutimiza.
Ila tumekuelewa kaka Majjid
 
Utetezi wako hauna mshiko kabisaa, ni sawa na malaya kubeba mimba na asijue aliyeiweka. Wewe utaajiri namna gani mtu usiyemfahamu kwa kina ati kajipendekeza. Wakati wa ukweli kujitenga utafika tu.
 
... Missed calls za usalama wa taifa... Nadhani Dr Slaa alikuwa right kuwahusisha hawa jamaa na hilo tukio
 
... Missed calls za usalama wa taifa... Nadhani Dr Slaa alikuwa right kuwahusisha hawa jamaa na hilo tukio
 
we tulia ukweli utajulikana tu, pia watu wanahisi wewe ndio uliomshawishi ludo aisaliti chadema kutokana na ukaribu wa na ccm. NB:HUWEZI KUSEMA WEWE NI MTU WA JAMII WAKATI UKO UPANDE WA WATU WANAOIKANDAMIZA JAMII(CCM)!
 
Maggid

Nimesoma maelezo yako na nimekuelewa. Kamwe siwezi kushutumu Mtu hata nisiyemjua na kisha kumhukumu. Nimesema hata huyo Luddo mpaka sasa Ni mtuhumiwa tu hivyo Bado Ni innocent. Hatua ulizochukua Ni sahihi Kabisa.
Ndugu Lwakatare mpaka sasa Ni mtuhumiwa tu pia.

Kuna watu hapa wana majibu Yao tayari kuhusu kesi hii. Sitatia neno maana kwanza kesi ipo mahakamani na chama changu kimeshatoa tamko. Sina la kuongeza.

Wale wenye midomo mipana ya kusema Kila Kitu waseme tu maana Ni midomo Yao pia hailipiwi kodi. Wakati mwingine hao ndio wale Chinua Achebe anasema wanaolia sana msibani kuliko wafiwa wenyewe. Njia bora Ni kutowajibu na kuvuta Subira maana hatimaye ukweli utajulikana tu.

Uwongo hupanda ngazi Kwa lifti, ukweli Kwa ngazi lakini utafika tu na wasema uwongo na waropokaji wataumbuka.
Tukio la Kibanda na lile la wana habari na Watanzania wengine walioteswa na kuumizwa au kuuwawa linatia simanzi sana. Inasikitisha watu wanapoweka siasa kwenye matukio haya.
Tuache Haki itendeke na kuhakikisha kweli Haki sio tu itendeke bali pia inaonekana inatendeka.

Watesaji wa Kibanda tutawapata tu na wao na waliowatuma watafikishwa mbele ya mahakama. Hatuwezi kuacha watesaji kutamba na kuendelea kutesa watu wengine.
Serikali iache siasa kwenye hili, mahakama itende Haki.
Maana yake kuna makundi hasimu hapa! Na mtoa hoja kundi lake limezidiwa. Kwa mujibu wa Zitto Serikali haihusiki na utesaji wa Kibanda(ameitaka serikali iache siasa{longolongo} na kuiachia mahakama isiwe na upande ifanye kazi zake).
Ningekuwa POLISI mie wala sipati shida kuwakamata wahalifu wa Tanzania.
 
Maggid, rafiki yangu, pole sana. Huo ndio mfumo uliokulea, huwezi kuubadilisha.

Uliporudi kutoka ughaibuni, ulikuwa na muelekeo mzuri na uandishi ulionyooka.

Baadae ukaja kubaini kuwa aina hiyo ya maisha haiwezi kufanya kazi hapa nyumbani kama ulivyozea huko nje ulikokuwa.

Taratibu ukaanza kubaini kuwa ili uweze kuishi hapa nyumbani ni lazima ubadili mfumo wako wa uandishi na kujifunza kubeba viatu vya watawala na mizigo yao.

Pole pole, kwa ustadi mkubwa ukaanza kubadili style ya uandishi wako.

Pale ulipoona watawala wamepotoka, hukuweza kukemea tena kama zamani. Ulitafuta lugha laini, usiwaudhi. Naelewa una sababu za kufanya hivyo.

Makala zako zikaanza kukosa mvuto, lakini halikuwa kosa lako, ni mfumo ambao ulibaini huwezi kuubadilisha mara moja na uendelee na maisha yako.

Ulipobadili muelekeo, ndio hapo ulipoanza kutumika! Maskini pengine bila hata ya wewe kujua.

Pole sana rafiki yangu, naujua uchungu wako, huyu mlezi ameamua kula watoto wake.

Ukitaka uaminike tena, rudi katika mstari. Utapata shida kwa muda, baadae utasimama tena.Pole sana.

Kumbuka Maggid, ni rahisi zaidi kuibomoa kuliko kuijenga nafasi yako katika jamii. Utafakari sasa na kuchukua hatua.
 
Maggid

Pole kwa haya. Kama alivyotamka Zitto, ukweli hutafutwa na uongo hutengenezwa.

Kweli watendaji wa vyombo vya usalama ni weledi la sivyo kwa udaku huu ungekuwa lupango nawe.
 
Nimesoma hadi nilipofika kwenye hii sentensi nikagundua kuwa kumbe nasoma unafiki. Mjengwa wewe ni mojawapo ya watu walioguswa na yaliyotendwa kwa Mwangosi na Ulimboka, na nakumbuka comments zako.
Lakini pia kama mwandishi wa habari, ni wazi kuwa umekuwa ukifuatilia kwa karibu utendaji wa vyombo vya usalama Tanzania. Unless wewe ni mmoja wao kwa namna moja au nyingine, sikutegemea sentensi kuwa "Ni bahati nyombo vya usalama Tz vinafanya kazi kwa ueledi"... sikutarajia...
Hakuna watu wa wabaya kama aina ya mjengwa. Nimemsoma sna huyu jamaa na kuhitimisha kuwa ni mnafiki. Hapendi msimamo wake ujulikane waziwazi mbele ya wakubwa. Kwa lugha ya mitaani naweza kusema ANAJIKOMBA.
 
Ugaid ni tatizo kubwa,kujitetea kwako kunaonyesha Kuna kitu,wewe nae ni wa kuungwanishwa kama Mbowe na Slaa nao inavyobid waunganishwe,CHADEMA Kuna tatizo kubwa,yote ni Mbowe na Slaa.

watu wa aina yako na yule mchumi fake mtakuja kuiingiza Nchi hii matatizoni. mara nyingi mnawaza kwa kutumia masaburi.
 
Ugaid ni tatizo kubwa,kujitetea kwako kunaonyesha Kuna kitu,wewe nae ni wa kuungwanishwa kama Mbowe na Slaa nao inavyobid waunganishwe,CHADEMA Kuna tatizo kubwa,yote ni Mbowe na Slaa.

mimi na jina lako tu "...NTGWAISANGU..."
 
Kwa mujibu wa maelezo ya Mtela Mwampamba POMPO ni ID ya Ludovick Rwezaula, mtuhumiwa wa kesi husika. Kama maelezo yake ni kweli basi ni ishara ya maendeleo kuona mahabusu zetu zimekuwa za kisasa kiasi kwamba watuhumiwa wanaweza kuendelea kuwasiliana na Raia kwa njia ya kisasa kabisa!

Hii inamaanisha ujumbe uliokaririwa hapo juu umeandikwa na Ludovick!

Mkuu Omutwale naomba sana Mods Paw PainKiller nitendewe haki kama ni Mtela Mwampamba amenitaja kuwa mimi ni Ludovick ATHIBITISHE akishindwa ale ban na wakati mwingine Ritz huwa wanataja kuwa mimi ni flani, mkuu Invisible, huku si kuvunja sheria zetu tulizojiwekea?

Nashkru nadhani nitatendewa HAKI kama mlivyofanya kwa Pasco
 
Last edited by a moderator:
Nashkru nadhani nitatendewa HAKI kama mlivyofanya kwa Pasco
Mkuu Pompo, kiukweli siku ile, mimi nilionewa!, aliyetaja fulani ni fulani ni mwingine, mimi niliichukua tuu hiyo quote ya fulani ni fulani, ndipo nikaichambua tena bila hata kutaja jina!, cha ajabu, huyo fulani, badala ya kumtaka aliyemtaja kuwa yeye ndiye fulani, akanitaka mimi niyequote eti ndiye nithibitishe, akanipa na masaa, akaniripoti kwa modes, na kulishwa ban papo kwa papo!. Cha ajabu aliyemtaja fulani ndiye fulani, sio tuu hakutakiwa kuthibitisha, bali pia hakupewa adhabu yoyote!, bali aliye quote fulani ni fulani, ndie aliyetakiwa kuthibitisha na kula ban on top of that!.

Sikuitafuta haki zaidi kwa sababu modes pia they are humans!.

Pasco.
 
Mkuu Pompo, kiukweli siku ile, mimi nilionewa!, aliyetaja fulani ni fulani ni mwingine, mimi niliichukua tuu hiyo quote ya fulani ni fulani, ndipo nikaichambua tena bila hata kutaja jina!, cha ajabu, huyo fulani, badala ya kumtaka aliyemtaja kuwa yeye ndiye fulani, akanitaka mimi niyequote eti ndiye nithibitishe, akanipa na masaa, akaniripoti kwa modes, na kulishwa ban papo kwa papo!. Cha ajabu aliyemtaja fulani ndiye fulani, sio tuu hakutakiwa kuthibitisha, bali pia hakupewa adhabu yoyote!, bali aliye quote fulani ni fulani, ndie aliyetakiwa kuthibitisha na kula ban on top of that!.

Sikuitafuta haki zaidi kwa sababu modes pia they are humans!.

Pasco.
Nakumbuka sana hilo sakata, ulilalamika sana hata Invisible wengine tulimu-PM kuhusu issue yako, na mlalamikaji (PA) nilimuPM na kusema umeonewa, as u said they are humans, tuendelee kuboresha jamvi letu ipo siku HAKI zitatendeka.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu good2015 kwa nini umeamua kututukana kiasi hiki? Kwanini usijenge hoja kupinga tunayo yaandika wewe una jenga matusi? Hii ni ishara ya kushindwa mapema!

michango ya wengi humu haina mashiko zaidi ya kejeli. ndo maana huwa sioni hata umuhimu wakujenga hoja kwa sababu wengi humu haziwatoshi na wametumwa na mabwana zao kuja kuandika wanachokitaka wao. sasa watu waaina hiyo unapoteza muda wa nini kujibishana nao. hawatakuelewa.
 
Wana jamvi.
Achani chuki na misimamo isiyojenga,Majjid ana sababu na ndiye anayepaswa kukakanusha au kuelezea jua ya kuhusika kwake au kutohusika kwake katika shauli analotuhumiwa nalo japo sio rasimi.
Kwa status aliyonayo majjid ktk jamii alipaswa kufanya alichofanya,kwanza kulisafisha jina lake lakini pia kulinda haiba ya kazi anayoifanya ya uandishi wa habari.
Naomba wana jf tusigeuke kuwa wakamataji,wapelelezi,maprosecutor na mahakimu sisi wenyewe,pia tusiijadili maada fulani kwa kinyongo,visasi na chuki dhidi ya anayezungumziwa.
Majjid alichukua hatua ya haraka na madhubuti kama mtu mwenye kuwajibika na hivi ndivyo inavyopaswa kwa muwajibikaji wa kweli,kwani hakujali kuharibika kwa mahusiano yake na Ludo ,bali kilichomuhimu kwake ni kujitenga na uhusika wa tukio linalozungumziwa.
Pia Majjid kujiweka kwake kando na Ludo hakuzuii yeye asihusishwe na tukio kama ushahidi upo,hivyo hakuna mantiki kwa wanaomtuhumu majjid kuendelea kulizungumzia suala la yeye kumuweka kando Ludo,vinginevyo hao wanaomtuhumu Majjid watuthibitishie pasipo shaka kuwa nao kwa njia moja au nyingine hawana maslahi na tukio hilo au upande fulani.
 
Back
Top Bottom