Magereza mapya 52 kujengwa

Magereza mapya 52 kujengwa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,676
Reaction score
57,097
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema serikali ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti nchini.

Masauni aliyesema hayo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rorya, Lameck Airo (CCM). Katika swali lake mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga gereza la Wilaya ya Rorya hasa baada ya kuwa kanda maalumu ya kipolisi.

Akijibu swali hilo, Masauni alisema serikali ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti likiwemo eneo la Rorya lakini changamoto kubwa ni upatikanaji wa fedha. Alisema Wilaya ya Rorya ni miongoni mwa wilaya 52 nchini zisizo na magereza.

Aidha kutokana na ufinyu wa bajeti, serikali itaendelea na ukamilishaji wa magereza ambayo ujenzi wake umekwishaanza ambapo kipaumbele ni kuhakikisha inakamilisha miradi ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
 
Kama Magereza hayo 52 yanajengwa sasa na idadi ya Watanzania kwa sasa ikiwa ni Milioni 55 naanza sasa kuwaelewa ' Kunakotukuka ' Magereza Tanzania. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Yaani Lameck ktk kipindi chako chote cha ubunge jimboni kwako upungufu uliyobaini ni wa gereza tu? Watu wanaomba miradi ya maendeleo wewe unaomba gereza?
 
Wapinzani mjiandae mana mnatengenezewa sehem mpya za kuishi. Ila hapa tz aloko salama ni mmoja tu mwenye kinga wengine wote ni wafungwa watarajiwa ni swala la muda hasa wapinzani . Ndo serikali tulonayo
Walahi
 
Hizo gereza wanawajengea Le mutuz, Musiba, polepole, Bashite jerry muro ili baadae waje kupumzishwa humo kwani mpaka yaje kukamilika Utawala huu wa kidikteta utakuwa unafika mwisho na ndipo Madhambi ya hao watu wabaya yataibuliwa kama uyoga na wote kwenda magerezani kuyazindua.
 
Afadhali hizo pesa zisipatikane tu
Wao katibu mkuu wizara ya fedha ni mtoto wa nje wa mtukufu ingawa huzuga kuwa ni mtoto wa dada yake, mtu na baba yake ndiyo wakuu wa hazina ya Taifa unategemea nini? Huchukua pesa BOT mda wowote wakitaka hata saa nane usiku, wakiamua watajenga hizo Gereza pa kuchukua pesa si humo Hazina ambapo wao ndiyo wamiliki kwa sasa.
 
komenti ujinga baadae yakikamilika tunapitia kila post na koment zake lazima uyatumikie
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema serikali ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti nchini.

Masauni aliyesema hayo bungeni jana alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rorya, Lameck Airo (CCM). Katika swali lake mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga gereza la Wilaya ya Rorya hasa baada ya kuwa kanda maalumu ya kipolisi.

Akijibu swali hilo, Masauni alisema serikali ina mpango wa kujenga magereza 52 katika maeneo tofauti likiwemo eneo la Rorya lakini changamoto kubwa ni upatikanaji wa fedha. Alisema Wilaya ya Rorya ni miongoni mwa wilaya 52 nchini zisizo na magereza.

Aidha kutokana na ufinyu wa bajeti, serikali itaendelea na ukamilishaji wa magereza ambayo ujenzi wake umekwishaanza ambapo kipaumbele ni kuhakikisha inakamilisha miradi ambayo ipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Inasikitisha sana wakati wenzetu ulaya magereza yanakosa wafungwa wanayafunga na kubadilisha matumizi.Gharama ya kujenga hayo magereza wangefunga cctv kila mji.Pia kuwekeza katika elimu mikoa ya ziwa victoria penye mauaji kila siku

ISIS
MSAGA SUMU
Mshana Jr
Pascal Mayalla
 
Sasa hata Kama wangefunga CCTV halafu zikanasa matukio SI lazima sheria ichukue mkondo wake..huwezi kujua kiwango Cha uvunjaji wa sheria kimeonekana Ni kikubwa
 
Nimelikumbka goma moja la lucky dube Lina mstari fulani

Ova
 
Back
Top Bottom