Magereza kwasasa zitengewe maeneo ya uzalishaji

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
2,478
3,363
Habari ya muda huu wadau
Ninaona kutokana na hali ya kiuchumi,mahitaji ya chakula,ufinyu wa maeneo kutokana na ongezeko la RAIA na shughuli za kibinadamu ninashauri magereza hizo zitengewe maeneo ya uzalishaji pembezoni mwa miji

Maeneo hayo yatasaidia katika kilimo cha mazao,miti ya matunda na mbogamboga,ufugaji wa mifugo kama ng'ombe,mabwawa ya samaki,kuku nk
Hatua hii itachangia kulifanya jeshi la magereza na wafungwa kujitegemea kwa chakula na kuzigawia taasisi nyingine kama hospitali,vituo vya watoto yatima na wazee wasiojiweza

Ili kuhakikisha zoezihilolinafanikiwa,yakishatengwa maeneo vipelekwe vitendea kazi kama matrekta,mbolea na mbegu za kisasa bila kusahau maji ya uhakika mfano kuchimba mabwawa makubwa au visima

Lengo nikuzifanya magereza zote nchini zijitegemee
 
Hv kwann magereza hayawez kujitegemea wakat wafungwa
Hua wanaacha hapo
Pesa kila sku
 
Back
Top Bottom