Magdalena Sakaya asema mgogoro wa CUF umekwisha; atoa maagizo kwa viongozi wote kujielekeza katika kujenga chama

Tunkamanin

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
951
865
Mbunge wa jimbo la Kaliua mkoani Tabora Magdalena Sakaya amesema mgogoro wa chama cha CUF sasa hivi umeisha na akaunti za chama zilizokuwa zimefungwa sasa zimefunguliwa na wanapokea ruzuku tangia wiki iliyopita na kuwaasa wananchama wa chama hicho kukiimarisha chama kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019
Amesema sasa wamezindua kampeni ya 10 kwa 10 ambayo kila mwanachama wa CUF atatakiwa kuvuta wanachama wengine 10 wapya na hao wapya watatakiwa kuvuta wanachama wengine 10 ili wafanye vizuri uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na kuchukua nchi mwaka 2020

Pia amemshukuru jaji wa wa kesi ya kupinga kuapishwa kwa wabunge wapya wa viti maalumu kwa kuzingatia katiba yetu ya chi inayotaka mihimili mitatu ya nchi yetu kutoingiliana na kuruhusu wabunge wao wateule waapishwe

 
Back
Top Bottom