Magazeti ya Shigongo kulikoni

Magazeti ya Shigongo kulikoni

A man of God

Member
Joined
Sep 5, 2015
Posts
65
Reaction score
14
leo nimesoma katika gazeti la Mizengwe ya Uchaguzi. lakini nilichoshangaa ni kwamba karibu gazeti zima linakosoa juhudi za UKAWA kutaka kuchukua nchi. mara nyingi limemkosoa Lowassa na Sumaye kwa kuhama CCM. Kwa mfano kichwa cha leo kinasema Edward Lowassa awaambia watanzania waache upumbavu. lakini ukisoma kwa ndani utagundua kwamba kuna negative tu zinazungumzwa kuhusu Lowasa na Ukawa kwa ujumla isipokuwa kuna makala moja ambayo imeelezea namna watu walivyochoshwa na maisha magumu. jamani swali langu nataka kujua Eric Shigongo ni kada wa CCM na kama ni hivyo je na vyombo vyake navyo ni kada wa CCM. Kama anataka hivyo basi awaambie watu wajue kimoja baada ya uchaguzi hakuna kusoma magazeti yake
 
Kwani ni siri, mbona ameweka wazi. Hivi Startv umeisusa kwa sababu ni ya kada wa Ccm?
 
Shigongo ni msukuma
magufuli ni msukuma

hupati connection?

halafu Shigongo siku nyingi hamkubali Lowassa....
 
anajaribu kudhoofisha mapambano ya wana mabadiliko...abakie na utunz wa stories zake .... maana mara udini mara nn..... sitak kumsikia tena
 
Shigongo ni msukuma
magufuli ni msukuma

hupati connection?

halafu Shigongo siku nyingi hamkubali Lowassa....

Sio hivyo tu, Shigogo ni kada maarufu wa CCM. Mwaka 2010 alitaka kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kwa ticket ya lile jimbo la Dr. Chegeni, akashindwa kwenye kura za maoni. So, anachofanya ni kukitetea chama chake.
 
Kura za maoni 2010 aligombea jimbo la Buchosa nadhani liko Misungwi mwanza akashindwa kura za maoni ndani ya CCM na Dk Tizeba
 
Shigongo ni kada Wa CCM Wa muda mrefu sana, hata mwaka 2010 alikuwa ni miongoni mwa wanaCCM waliomba kugombea ubunge katika jumbo Fulani mkoani Mwanza, bahati mbaya alishindwa kwenye kura za maoni. Sijui kama mwaka huu kama hakugombea na kushindwa.

Kwa sasa Shigongo ni miongoni mwa team ya wanaCCM ya propaganda kwa kutumia vyombo vya habari wanavyovimiliki. Wengine ni Antony Diallo(Star TV, Free Africa, Kiss FM), General Ulimwengu(RAIA kwema na RAIA Tanzania), Ruge Mutahaba/Joseph Kusaga(Clauds FM,Coconut FM, Clauds TV), Msama(Dira Tanzania) nk.

Kwa sasa hali ya kisiasa ni mbaya sana kwa CCM hivyo kila chombo cha habari ambacho wanaweza kukitumia kufanya propaganda zao chafu watakitumia, ndio maana hata vyombo vya umma kama TBC, habari Leo, Daily News na Sunday News vimekuwa ndio vyombo rasmi vya kufanyia kampeni za CCM. Hawana jinsi tena, hali yao kisiasa ni mbaya sana na inazidi kuwa mbaya kila siku kuelekea siku ya uchaguzi.
 
Ameshindwa Slaa kuzuia mabadiliko, ataweza Shigongo???? TUMEAMUA, Rais wetu ni Lowassaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!! Hatutaki kusikia kabisa habari ya Mr Push-up!!!!!!!!
 
Huna aja ya kumjadili Shigongo ni kada wa ccm makapi,aligombea akakiona cha mtemakuni,asubui alishapigwa,sasa sijui ni kwanini anajipendekeza wakati hakubaliki ndani ccm!
 
Mbona Gazeti la Mwanahalisi na Mawio Hamyajadili Humu?

Yani kila mtu atakae kwenda kinyume na nyie basi hafai...

Basi Mngeanzisha na nyie la kwenu... Kumjadili mtu na Biashara Yake ni kukosa Uelewa.
 
Ndugu zangu bavicha, 4um na wanaukawa, jihadharini sana NA kauli zenu. siasa ni ushindani. na asiyekua upande wako huyo ni mpinzani wako na si adui. watu hutofautiana ki fikra, mtazamo. sote hatuwezi kuwa na mtazamo mmoja vinginevyo hakukua haja ya vyama vingi.ushauri wangu. kubalini tofauti na tuwe na subra(tolerance). Shigongo ana haki ya kukosoa, kutoa mawazo yake, msimamo wake na tuuheshimu.matusi, kejeli na mawama tuache. hi ni nchi yetu sote. hakuna aliye bora ya mwengine. kumbuka ushindani ccm vs vyama 22. vyote vikilenga ikulu na kutawala bunge. mziki mkali. hakuna anayetaka kushindwa. mshindi ataibuka mmoja. tuwe tayari kwa matokeo yoyote. na baada ya okt.25, maisha yataendelea.
 
leo nimesoma katika gazeti la Mizengwe ya Uchaguzi. lakini nilichoshangaa ni kwamba karibu gazeti zima linakosoa juhudi za UKAWA kutaka kuchukua nchi. mara nyingi limemkosoa Lowassa na Sumaye kwa kuhama CCM. Kwa mfano kichwa cha leo kinasema Edward Lowassa awaambia watanzania waache upumbavu. lakini ukisoma kwa ndani utagundua kwamba kuna negative tu zinazungumzwa kuhusu Lowasa na Ukawa kwa ujumla isipokuwa kuna makala moja ambayo imeelezea namna watu walivyochoshwa na maisha magumu. jamani swali langu nataka kujua Eric Shigongo ni kada wa CCM na kama ni hivyo je na vyombo vyake navyo ni kada wa CCM. Kama anataka hivyo basi awaambie watu wajue kimoja baada ya uchaguzi hakuna kusoma magazeti yake

Ulipata wastani wa ngapi FORM TWO Mkuu!!Bangi unaacha lini kuvuta?
 
Shigongo ni msukuma
magufuli ni msukuma

hupati connection?

halafu Shigongo siku nyingi hamkubali Lowassa....

Kwanini usiseme Shigongo ni CCM na Magufuli ni CCM.MMU Wamekumiss ujue...
 
sio hivyo tu, shigogo ni kada maarufu wa ccm. Mwaka 2010 alitaka kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kwa ticket ya lile jimbo la dr. Chegeni, akashindwa kwenye kura za maoni. So, anachofanya ni kukitetea chama chake.
acha kupotosha 2010 aligombea kule buchosa sengerema akashindwa na tizeba,chegeni ni busega ya magu
 
Back
Top Bottom