Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,361
- 2,734
Yaani imenishangaza sana kuona magazeti ya serikali yanabeza mazungumzo ya amani yaliyofikiwa kati ya CHADEMA na Police. Watu wameitana wakaelezana vizuri na kushauriana kutoandamana ukizingatia uwepo wa Ugeni wa Rais wa China na kwamba duniani wengi kwa sasa wanaitazama Tanzania kwa karibu, lakini magazeti ya Uhuru na Jambo Leo yanaandika vichwa vya habari kuwa "Mbowe maji ya Shingo.....asalimu Amri" CHADEMA wasalimu amri n.k. Hii ni sawa na mtu kukuita mkaafikiana jambo alafu kesho yake anakwambia wewe ni lijinga kwa kukubali maafikiano.
Kusalimu amri ni pale ambapo pande mbili zinakinzana kwa mbali pasipo kukaa mezani na mmoja ana give up. Sasa kwa lugha za kipuuzi namna hii nani atakubali kukaa na serikali tena mezani wakati baada ya hapo mnasema fulani kaufyata?
Serikali inabidi iwe makini kwa kukemea vyombo vyake. Huu ni ujinga na inaonesha wanatamani confrontation masaa yote. Nawaambia tena huu ni ujinga.