Magazeti ya bongo msioope kuwa huru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magazeti ya bongo msioope kuwa huru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GABE100, May 19, 2012.

 1. G

  GABE100 Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"] Magazeti ya Mail, Guardian yathibitishiwa uhuru [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 18 May 2012 22:33 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  JOHANNESBURG, Afrika Kusini
  MAGAZETI ya Mail na Guardian yameshinda kesi ya kupigania uhuru wa vyombo vya habari, baada ya mahakama kuamua kwamba waandishi hawatakiwi kulazimishwa kutaja vyanzo vyao vya habari.

  Katika uamuzi huo dhidi ya Bosasa uliotolewa jana katika mahakama Kuu ya South Boateng mjini Johannesburg, Jaji Moroa Tsoka alipigilia msumari uamuzi wa kisheria unaowazuia waandishi wa habari kuvitaja vyanzo vyao vya habari.

  Kesi hiyo ilikuwa ikiwahusisha Bosasa dhidi ya magazeti hayo mawili, na mwandishi wao wa habari za uchunguzi, Adriaan Basson kwa tuhuma za udhalilishaji dhidi ya Bosasa.

  Uamuzi huo umetolewa baada ya Bosasa kuyataka magazeti hayo kutaja vyanzo vya habari ya uchunguzi dhidi yake.

  Katika uamuzi wake jana asubuhi, Jaji Tsoka alisema kwamba kwa mtizamo wake, suala la kutaka vyanzo vya habari viwekwe wazi si sawa, na kuitaka Bosasa kuangalia zaidi suala la usahihi wa habari iliyoandikwa na si kujua majina ya vyanzo vya habari hiyo.

  Alisisitiza kwamba suala la kutoa taarifa “ni haki ya msingi ya kila raia katika jamii inayojali demokrasia”, akieleza pia kwamba Uhuru wa vyombo vya habari ni suala la muhimu katika demokrasia hivyo ili kuweza kuwatendea haki wananchi vyanzo vya habari havitakiwi kuwekwa wazi pale inapobidi.

  “Umuhimu huu kwa vyiombo vya habari ambavyo vinawajibika katika jamii inayojali demokrasia unahitaji uwazi, hasa katika wakati huu ambao rushw aimekuwa dondandugu ,” alisema Jaji huyo.

  Kesi hiyo ilifunguliwa baada ya makala iliyoandikwa na mwandishi Basson Mei 22, 2009 ikieleza kwamba Bosasa ameshinda zabuni ya mamilioni ya Rand kwa kutumia rushwa.

  Magazeti hayo yaliitoa habari hiyo kw amtiririko wake wakieleza namna nyaraka za zabuni hiyo zilivyoweza kupewa kipaumbele kabla ya kutolewa kwa tangazo la zabuni hiyo.

  Bosasa aliamua kuyashtaki magazeti hayo pamoja na mwandishi wake, Basson kwa kumdhalilisha ambapo pande zote zilitaka kupata maelezo ya kina kuhusu madai na mdaiwa ambapo kampuni ya Bosasa iliyataka magazeti hayo kutoa maelezo kuhusu uchunguzi wa habari hiyo, suala ambalo lilifanyika lakini baadhi ya sehemu zikiwa zimefutwa hasa zilizokuwa na majina ya wahusima.

  Bosasa ilikataa vielelezo hivyo na kutaka nyaraka kamili zikiwa na majina ya vyanzo, ambapo, katika majadiliano yao ya kina, walieleza kwamba vyanzo vya habari vya siri vinaweza kutumiwa kwa ajili ya kuendesha agenda ya siri, kuendesha propaganda za uongo na kusababisha kutowajibika katika kutoa habari.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...