Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
Ujasiri kwa Upinzani, Kimya kwa CCM
Jana, kupitia ukurasa wake wa Facebook, Balozi Humphrey Polepole alitoa maoni bila kupepesa macho kuhusu uteuzi wa Rais Samia kuwania tena urais na kuvunjwa kwa baadhi ya desturi za Chama cha Mapinduzi (CCM). Hata hivyo, magazeti nchini yameshindwa kuripoti moja kwa moja kauli hizo, tofauti na jinsi yalivyo mstari wa mbele kuripoti taarifa za vyama vya upinzani, hata pale zinapokuwa na ladha ya kuharibu taswira ya vyama hivyo.
Sababu kuu ya hali hii ni uoga uliokita mizizi ndani ya vyombo vya habari vya Tanzania. Magazeti na redio nyingi huogopa kuchapisha taarifa zinazoweza kutafsiriwa kama ukosoaji kwa Serikali au chama tawala kwa kuhofia kufungiwa, kupokonywa leseni, au kupewa onyo na mamlaka za udhibiti kama TCRA. Matokeo yake, vyombo hivi vinachagua ukimya pale ambapo hoja zinagusa misingi ya chama tawala, huku vikitoa nafasi kubwa kwa taarifa za upinzani, bila kujali madhara au ukweli wake.
Hali hii inaibua maswali juu ya uhuru wa vyombo vya habari na nafasi yake katika kuelimisha umma kwa kuandika ukweli bila hofu wala upendeleo. Kauli za Polepole, ambazo zilihusu uhalali wa mchakato wa uteuzi ndani ya CCM, ni mfano wa taarifa ambazo zingepaswa kujadiliwa kwa uwazi, lakini zimezuiliwa na hofu ya kisiasa.