Magari yanayokwenda Ilala - Buguruni kupitia service road ya Shule ya Msimbazi kutokea Mafao Road hukamatwa kwa kosa gani hasa?

drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
4,664
4,764
Foleni huwa ndefu sana kuanzia soko la sambusa kigogo mpaka mataa ya Karume. Kuna magari yanaenda Ilala hadi Buguruni kupitia barabara ya mafao. Swali langu hawa watu wanaokwenda ilala Buguruni wakipitia service road ya Shule ya Msimbazi waje watokee Mafao Road hukamatwa.

Je, huwa kosa gani hasa? Maana wanakwepa foleni pia nakupunguza mlolongo wa magari sehemu moja kwanini isiwe ruhusa kupitia service road ya Msimbazi centa na Ramada Hotel unatokezea mafao.
 
Mimi sio trafiki ila ni raia tu wa kawaida. Sasa ukitaka iwe hivyo, watembea kwa miguu na watumia baiskeli wapite wapi?
 
Hata hapa makonde ukipita service road ili uibukie pale tank bovu wanakurukia na kukuandikia kosa la kutumia barabara hiyo kwa kukwepa foleni yaani wao wanaokamata wanataka mkae foleni,waliopo madarakani wanaumiza vichwa kwa kubuni barabara za michepuko ili kupunguza foleni,basi unabaki na sintofahamu ni nini haswa tunasimamia
 
Back
Top Bottom