Magari yametekwa huko igunga

Magari yametekwa huko igunga

ndukushi

Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
7
Reaction score
3
kuna taarifa za malori 3 kutekwa na majambazi usiku wa kuamkia leo. madereva wamejeruhiwa kwa kuchomwa mwilini na vitu vyenye ncha kali pamoja na kutobolewa macho. kwa sasa malori na mabasi yamekwama baada ya wenye malori kuziba njia kati ya igunga na nzega wakilalamikia serikali kushindwa kuchukua hatua toka jana usiku walivyotoa taarifa na badala yake wamefika leo asubui. habari hizi nimejulishwa na ndugu yangu ambaye yuko eneo la tukio akisafiri kutoka mwanza kwenda Dar. Hadi sasa wenye malori wamegoma kuongea na wanadai wataongea na uongozi wa juu tu kwani serikali imeshindwa kuwapa ushirikiano.
 
poleni, ila nadhani inastahili hili suala la utekaji katika barabara hii liangaliwe sana, hasa maeneo ya sekenke shelui hadi nzega ni hatari sana
 
Back
Top Bottom