Magari, pikipiki zaidi za CCM zaja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magari, pikipiki zaidi za CCM zaja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, May 31, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  KATIKA kujiimarisha kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinatarajiwa kununua na kusambaza magari katika mikoa mbalimbali nchini ndani ya wiki mbili zijazo, ikiwa ni katika awamu yake ya pili ya ugawaji.

  Magari yatakayonunuliwa katika awamu hiii yatakuwa ya viongozi wa mikoa kote nchini, Bara na Visiwani. Awamu ya kwanza ilihusisha wilaya zote nchini.

  Katibu wa Fedha na Uchumi wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Taifa , Amos Makalla, alisema hayo mwanzoni mwa wiki mjini hapa wakati akiwahutubia wanachama na viongozi wa Chama hicho katika Manispaa ya Morogoro.

  Hata hivyo alisema , kununuliwa kwa magari hayo, pikipiki na baiskeli ni moja ya mikakati ya kuwawezesha viongozi wa ngazi zote kushiriki kampeni za mwaka huu kwa ufanisi mkubwa zenye kuleta ushindi mnono kwa wagombea wa chama hicho.

  "Kamati ya Kampeni ya Uchaguzi wa mwaka huu inaendelea vizuriÂ…wiki mbili zijazo tutakuwa tumenunua na kuleta magari mapya kwa ajili ya mikoa yote kwa ajili ya viongozi wa CCM wa mikoa, Bara na Visiwani kwa ajili ya kampeni za uchaguzi," alisema.

  Hivyo alisema kwamba, ili chama kiweze kupata mafanikio zaidi, ni vyema viongozi wa ngazi zote wakaendelea kuwahamasisha wanachama, wapenzi na washirika kukichangia fedha kupitia mpango maalumu wa ujumbe mfupi wa 'SMS' uliozinduliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni.

  "Hapa naomba nisisitize kuwa, viongozi wa ngazi mbalimbali katika mikutano endelezeni kuwakumbusha wanachama juu ya kukichangia fedha chama kupitia ujumbe mfupi wa sms kuanzia kiasi cha Sh: 300, 500 na 1,000 na hii iwe ajenda ya kudumu katika uchaguzi huu " alisema Makalla.

  Naye Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Dk. Omari Mzeru, alisema wanachama wa Chama hicho katika kata zote 19 za manispaa hiyo wamejipanga vyema kuhakikisha CCM inashinda viti vyote vya udiwani pamoja na ubunge.
   
Loading...