Wanaondoa 'magamba' ili iweje?
As long as matajiri wengi wanaohujumu raslimali za taifa letu wanakula na viongozi wa serikali ambao tunajua kuwa ndio CCM, hakuna Gamba linalovuliwa. Fikiria mabilioni ya tenda feki, fikiria madini yanayopotea, fikiria wakurugenzi na madairekta wa idara na wilaya mbalimbali wanavyobanjua hela za wananchi. Fikiria utendaji mbovu wa wanachama wa CCM unavyosababisha taifa kuwa gizani kwa kukosa umeme, Fikiria maofisa ardhi, maofisa wa TAKUKURU na wa TRA, maofisa wa bandarini na wa polisi, ambao kama wao sio wanaCCM, basi nafasi zao wamewekwa na CCM, jinsi wanavyopokea rushwa na kumuonea mwananchi wa hali duni Tanzania, hii, hivi kweli CCM inadhani kumuondoa Makamba, ndiyo kuvua Magamba?!!!!