Magamba yakiisha na CCM imeisha, kwani ni Chama Cha Magamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magamba yakiisha na CCM imeisha, kwani ni Chama Cha Magamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Apr 11, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, CCM imekiri hadharani kuwa imejaa magamba, na imeanza kuyavua.
  Lakini tujiulize Magamba yaliyopo ni CC na sektretarieti peke yake?
  Mimi naona kuwa Gamba kubwa kabisa, tena lililofunika sehemu ya kichwa hadi machoni ni Mwenyekiti, ambaye utendaji wake dhaifu serikalini unasababisha chama kionekane cha hovyo!
  Hivi Sophia Simba kweli sio Gamba nene sana ambalo limemaliza eneo lote la Jinsia?
  R1 Nae ni Gamba la ajabu kabisa ambalo bila kuvuliwa chama hakitembei
  Mawaziri wote nao ni magamba tu tena haya ndio mabaya kwani watu wanaihukumu CCM kutokana na performance ya serikali kwa ngio Chama kinachoshikilia serikali.

  Ki ukweli ni kuwa CCM imeundwa na mkusanyiko wa magamba mengi, na hakuna namna ya kuyavua. You are finally dieing.
   
 2. S

  Soyinkwa Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  chama ni mtendaji mkuu...so katibu mkuu akiwa vuvuzela hapo ipo shida...chairman akitoa uswaiba magamba yatang'oka...kiukweli still magamba bado yapo na makubwa kwelikweli...bt nice shot for ccm...
   
 3. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM yenyewe ni gamba ambalo linatakiwa kuvuliwa
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  magamba ya ccm kwangu mimi kubwa ni UFISADI na WIZI wakijivua hilo watakuwa wapya kabisa!
   
 5. d

  dotto JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sina uhakika kama Magamba wanamaanisha uenezi wa chama. NAfikiri walikosea kusema magamba. KAma ni magamba Kikwete anafanya nini. Kwani Mukama, Kinana ni wasafi. MAgamba kwetu sisi watanzania ni wizi wao kuhusu Rasilimali za nchi. Mbona Nec wamejaa mafisadi wakubwa.
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Lakini mkuu, hakuna UFISADI hakuna CCM. CCM ni mtandao wa ufisadi Tanzania. Kuwaambia wavue UFISADI ni sawa na uambie kanisa likome kueneza neno la mungu (Sorry kwa waumini). CCM kama chama cha kisiasa haipo tena na mabaki yake hayajulikani yalikofukiwa. CCM imebaki kama system ya kifisadi Tanzania.
   
 7. S

  Seal New Member

  #7
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili dhana ya neno magamba wapinzani wakilitumia vizuri na kufanyia propaganda litawalipa; wanaihitaji vazi la kondoo siyo fig leaves! yatakauka tu
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Tatizo siyo gamba hata mwenye magamba (CCM)Inatakiwa ianzishwe upya chama kingine!!siyo kuvua magamba hapa wanazunguka palepale!
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Magamba CCM yako mengi tu for instance mbunge wa Igunga RA ambaye ni mjumbe wa CC na mbunge wa Bariadi Mashariki ambaye ni mjumbe wa kama hiyo Andrew Chenge walipashwa wajiuzulu lakini matokeo yake ni kwamba Rais analazimsha kamati nzima kujiuzulu ili hali hawa wawili ambao ni mizizi inayopaswa kung'olewa wanaachwa nilikuwa nategemea mojawapo ya ajenda kubwa ingekuwa kuwataka hawa RA na AC wajiuzulu.
   
 10. s

  sawabho JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Wapinzani wanamalizana wenyewe kwa wenyewe, halafu wako wengi na kila mmoja ni mpinzani kwa mwezake. Sasa hiyo dhana itamlipa nani? Ngoja CCM wanfanye retreat uone mambo yatakuwa safi, maana tayari wamejifunza.
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wanaondoa 'magamba' ili iweje?
  As long as matajiri wengi wanaohujumu raslimali za taifa letu wanakula na viongozi wa serikali ambao tunajua kuwa ndio CCM, hakuna Gamba linalovuliwa. Fikiria mabilioni ya tenda feki, fikiria madini yanayopotea, fikiria wakurugenzi na madairekta wa idara na wilaya mbalimbali wanavyobanjua hela za wananchi. Fikiria utendaji mbovu wa wanachama wa CCM unavyosababisha taifa kuwa gizani kwa kukosa umeme, Fikiria maofisa ardhi, maofisa wa TAKUKURU na wa TRA, maofisa wa bandarini na wa polisi, ambao kama wao sio wanaCCM, basi nafasi zao wamewekwa na CCM, jinsi wanavyopokea rushwa na kumuonea mwananchi wa hali duni Tanzania, hii, hivi kweli CCM inadhani kumuondoa Makamba, ndiyo kuvua Magamba?!!!!
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Apr 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Fikiria ugumu wa maisha na mishahara midogo. Ewe Kikwete, fikiria wananchi wako kule kijijini wanaokufa kwa kukuosa huduma za afya, wanaohangaika kutwa kutafuta maji ya kunywa. Fikiria watoto wale walioshindwa kwenda shule, na wale walioenda shule wanakaa chini, na wale walioko shule zisizo na mwalimu, Fikiria maelfu waliofeli kidati cha nne, wanavyoteseka. Lakini ninyi mnagawiana mabilioni kwa cheki, eti mnasema mnavua magamba?

  Kuvua magamba kutamfaa nini aliyeshinda kwa njaa, aliyekosa dawa zahanati, anayepanda baiskeli kwenda kujifungua?!!!
   
 13. K

  Kihyoi Member

  #13
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM imekuwa ibilisi. Imechezea maisha na uhai wa WTZ kwa kiwango cha kupitiliza. Gamba hili ni zaidi ya sgluu kuweza kuling'oa. Inabidi ateketezwe na gamba lake haaminiki
   
 14. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Forget personalities and magamba. CCM kimeoza kwenye miziz.....yaani itikadi, sera yake, mfumo wake, maudhi yake na utashi wa kisiasa kwa Tz.
   
 15. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #15
  Apr 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kwa anaeitakia Tz mema anajua kwa uhakika kuwa ili nchi hii iendelee mbele na kujitoa kwenye lindi la umasikini ililomo, cha kwanza kufanyika ni kuitoa ccm madarakani., ccm kama ilivyo haiwezi kuisaidia hii nchi kupiga hatua yoyote ya maendeleo. kwa wanaoijua ccm, ambayo nayo inajua wazi kuwa haikubaliki tena kwa wananchi bila ya msaada wa dola, wataitazama tena kwa macho ya kebehi., kama mukama, kinana na zakhia ndiyo gamba jipya la kuikomboa ccm, basi mwerevu itabidi atazame la zamani lililotolewa lina tofauti zipi za kimsingi na lilioingia. nadhani haya ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu kwa nchi hii kuwa hatimaye hawa jamaa hawana tena pa kutokea wala watu wa kuwasaidia kutoka huko walikojiofikisha. wataishia huko huko huku nchi ikigeuka na kuchukua uelekeo inaostahili kuwamo.
   
 16. M

  Mantisa Senior Member

  #16
  Apr 11, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Gamba kubwa la ccm ni UFISADI. Kama kweli wanataka kuvua gamba kamata wote waliotufikisha hapa kwa maslahi yao weka ndani na wawajibike ila si wakamatwe kisanii kama kina Mramba then watakuwa wamevua gamba. Otherwise wao ndo watakuwa gamba na tutawavua 2015
   
Loading...