Magaidi wavamia Burkina Faso

Quickly

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
1,056
649
Hoteli yatekwa na wapiganaji Burkina Faso
  • Saa 9 zilizopita

151202161221_burkina_faso_map_512x288_bbc_nocredit.jpg

Maafisa wa usalama katika taifa la Magharibi mwa Afrika la Burkina Farso, wameanza mashambulizi kujaribu kuikomboa hoteli ambayo ilitekwa na wapiganaji Waislamu wenye itakadi kali walio na bunduki.


Mateka kadhaa wanadhaniwa kuwa katika jengo hilo katika mji mkuu wa OuagaDougou.
160116052350_officers_640x360_reuters_nocredit.jpg

Image caption Maafisa wa polisi wakijiandaa kukabiliana na wapiganaji.
Makomando walitegua vilipuzi waliopanza mashambulizi hayo na kwa wakati huu sebule ya hoteli hiyo inateketea.

Inadaiwa kuwa watu kadhaa wameuawa. Mkurugenzi wa hospitali moja aliyezungumza na manusura amesema kuwa waliofariki huenda wakawa zaidi ya 20.


160116015341_burkina_faso_attack_evacuation_640x360_ap_nocredit.jpg

Image caption Maafisa wa polisi wakiowaondoa baadhi ya mateka katika hoteli ya Splendid
Kundi la wapiganaji, lenye uhusiano na Al-Qaida, limedai kuhusika katika mashambulizi hayo.

Washambulizi hao pia walivamia mgahawa mwingine uliokuwa karibu na hoteli hiyo. Taasisi hizo zinapendwa sana na wateja wa kigeni kutoka mataifa ya Magharibi.


160116003738_burkina_faso_640x360_ap_nocredit.jpg

Image caption Eneo moja la hoteli hiyo linaonekana likichomeka kufuatia mashambulizi
Mapema mchana watu wenye bunduki waliwaua watu wawili katika shambulio lililofanywa karibu na mpaka na Mali.
====================================================================
Leo Burkina Faso,jana Kenya, kutwa Nigeria....sote tuko kwenye hali ya tahadhari.
 
Wanauharibu kabisa uislam sasa. Itafika siku mtu ataona aibu na fedheha kujitambulisha kama muislam
 
Marry

Hadi leo hujaweza kutofatisha kati ya dini ya kiislam na magaidi? Upo nyuma sana au laa wewe sio mfuatiliaji wa haya mambo kabisa
Ni MP nikuelimishe plz
 
Hao ni wahalifu kama wahalifu wengine hakuna DINI hapo.
Wamejificha kwenye mwavuli wa waislam lakini hakuna waislam hapo
DINI haisemi waislam wafanye hayo wanayoyafanya.
 
Ni sawa sawa na zile disco anazochezaga Rose Mhando and the like halafu useme kuna Mungu pale lol. Pale hayupo ni watu wanajitafutia maisha tuu hata Mch. Kakobe alishawahi kusema kuwa hakuna mungu pale ni wasakata rumba tu.
Soo is the same to wahuni wa bukina fasso tuu hakuna dini pale.
 
Back
Top Bottom