Mafuriko ya Mjini Dar es salaam

Angalieni, isijekuwa yule mtu mzima alilia machozi ili mafuriko yatokee aseme; Cheti changu kirikuwa apa kwenye diroo ya pili, kimechukuriwa na mafuriko kwa bahati mbaya. Ohoo! Mjini shule
 
Ndio ijulikane sasa Baba mwenye nyumba na Baba mwenye Gari nani zaidi
 
Hivi enzi hizo serikali ilikuwa wapi hadi uholela wa ujenzi unatokea na kuleta shida hizi? Big up JPM for you strictness, i believe ingekuwa era hii urban planners wangekwisha jutia tamaa zao mbaya

Sidhani kama shida kubwa ipo kwenye mipango miji, shida kubwa Water table ya Dar iko juu sana so mvua kidogo tu udogo unakuwa Saturated na maji yanashindwa pa kwenda, pili Sehemu kubwa ya mabonde ya Dar yapo almost at sea Level, chukulia Mikocheni yote, Jangwani, so kama kuna Bamvua (hightide) maji huwa yanajaa bHarini nakutapika maeneo ya Mikocheni, Kawe, kunduchi, jangwani nk so hiyo scenario ya high tide inasababisha maji ya mvua kushindwa kuingia baharini kwa urahisi

Ili kuzuia madhara kwa wakazi wa Dar basi Dar nzima ingepaswa kuwa low Density tena makazi yangejengwa sehemu zenye miinuko, ukweli ni kiwa sehemu kubwa ya Dar ni sehemu hatarishi
 
Huu ndio muda wa kununua kiwanja
Umenikumbusha kitu, kuna mtu bado kidogo anunue nyumba, sa ile kafanya ziara ya kustukiza baada ya mvua kunyesha si akakuta maji yamejaa ndani ya nyumba... Kumbe nyumba ilivyojengwa maji ya kutoka mtaani yote yanaingia kwake... Yaani alimshukuruje Mungu!!!
 
Angalieni, isijekuwa yule mtu mzima alilia machozi ili mafuriko yatokee aseme; Cheti changu kirikuwa apa kwenye diroo ya pili, kimechukuriwa na mafuriko kwa bahati mbaya. Ohoo! Mjini shule
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ kwani si naskia alienda kusini mwa Africa kutafuta vyeti
 
Asante kwa majibu mazuri kwa kuwa tunaelimishana, binafsi sioni kama mipango miji au hata wanasiasa walioruhusu makazi holela na ofisi hata kwenye mikondo na maeneo oevu ambayo ni kama sponge wanakwepa lawama. Nikubaliane na wewe pia sea level yaweza kuwa sababu, lakini katika ulimwengu huu wa teknolojia haikubaliki. Mbona netherland wameweza? ukienda Amsterdam utaona wametengeneza mifereji ya maji hayo ya bahari hadi ndani kabisa mji na yanatumika kama njia za usafiri toka eneo moja la mji hadi lingine.
Funzo: kwa miji mingine inayochipuka kama dodoma mipango miji wapewe nafasi kutumia taaluma yao na wawo wenyewe wasimaie maadili ya kazi zao
 

Uko sahihi kwa mifano hiyo ya Netherland, lakini kwa Dar inakalika bila kuwa na shida ya kusogeza bahari, lakini iwe Low density, chukulia mfano wa maeneo ya Tabata, mabibo, Mazense, Tandale, Sinza, Kijitonyama, Mikocheni, Kawe, Mbezi beach, hayo maeneo hata kama ni kiangazi bado utaona kuna maji yanatiririka, ukifika maeneo kama mbagala, mbande, kiwalani Airport na ukanda wote huo utaona wenyeji wanachimba visima vya futi chache sana na wanakutana na maji, so watertable iko juu sana, altenatively kwa maeneo kama haya ya Dar palipashwa kuwe na maeneo ya wazi mengi ambayo maji yangeweza kupita kwa wingi hivyo kungejengwa Maghorofa ya kuchukua watu wengi na sehemu kubwa iwe maeneo ya wazi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…