Mafunzo ya ufundi simu na TCRA

Mafunzo ya ufundi simu na TCRA

Realbest

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
812
Reaction score
301
Aisee wakuu kuna aliyebahatika kupata nafasi kwenye hii kitu hapa chini?

===
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (MB), amefungua mafunzo kwa mafundi simu za mkononi wa Kanda ya Ziwa wa kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Shinyanga na Simiyu

Kamwelwe amefungua mafunzo hayo yatakayofanyika kwa mafundi simu za mkononi wa Kanda ya Ziwa wapatao 200 ambayo yamepangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam, Kampasi ya Mwanza

Kamwelwe amewaeleza mafundi simu za mkononi kuwa wateja watakuwa hawana wasiwasi na wao kwa kuwa watakuwa wanaleta simu zao kutengenezwa kwa mafundi simu za mkononi ambao wamepata mafunzo yaliyotolewa na Serikali kupitia wataalamu wa DIT chini ya uratibu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) ambao wamedhamini na kufanikisha uendeshaji na kugharamia mafunzo hayo kwa Kanda ya Ziwa

“Ninyi ni mafundi ambao mtapata mafunzo na mtapatiwa miongozo, leseni na mmesajiliwa, mteja anapoleta simu yake kwako anakuwa hana wasiwasi kwa wizi na kwa wale ambao wanaiba simu na kuleta kwenu, nalo mtakuwa mmelimaliza kwa kuwa mtawabaini na kuwashughulikia kwa kushirikiana na mamlaka husika,” amesema Kamwelwe

Kamwelwe amewataka mafundi simu kujiunga pamoja ili waweze kupewa leseni na Serikali kutoka TCRA ili waweze kuitumia kununua vifaa vinavyohitajika kutengenezea simu ya mkononi na vifaa vingine vya TEHAMA ambavyo vitakuwa vimeharibika na vinahitaji kufanyiwa matengenezo ambapo amewaeleza mafundi hao kuwa kama hawana mtaji wamuone

Pia, ameongeza kuwa Serikali kupitia TCRA imeamua kuwajengea uwezo mafundi simu za mkononi ili kuweza kuwahudumia watanzania takribani milioni 34 wanaomiliki simu za mkononi na Serikali haiku tayari kuleta mafundi simu kutoka nje ya Taanzania ili kupitia mafunzo tuendelee kutoa ajira kwa vijana na tutaendelea kuwaweka kwenye vikundi maalumu ili muweze kusaidiwa kisheria kama ilivyo leo kwa kuwapatia mafunzo

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Kamwelwe, Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Dkt. Maria Sasabo amewaeleza mafundi simu za mkononi kuwa nae ni fundi kwa kuwa alisoma DIT akawa fundi mchundo ambapo amewahimiza mafundi hao na kuwatia moyo kuwa washirikiane vema na mafundi simu wa kike ambao wanapatiwa mafunzo na kuwaomba wakufunzi kuhakikisha kuwa wanawasaidia mafundi simu wa kike kushiriki kikamilifu na kuhitimu mafunzo hayo

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amewaeleza mafundi hao kuwa wayape kipaumbele mafunzo hayo kwa kuwa masuala mbali mbali yatafundishwa ikiwemo ujasiriamali ili kurasimisha mafunzo na ufundi kwa mafundi simu ili kuchochea ukuaji na ongezeko la la watumiaji wa vifaa vya huduma za mawasiliano na simu za mkononi

Kilaba ameongeza kuwa usalama na ubora wa vifaa vya mawasiliano ni jukumu letu sote ambapo mafundi simu ni sehemu ya utekelezaji na mafunzo haya yataendelea kutolewa na TCRA kwenye ofisi zake ikiwemo kwenye ofisi ya Kanda ya Kati ambapo amfunzo yatafanyika Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya), Kanda ya Kaskazini (Arusha) na Kanda ya Zanzibar (Unguja)

Mkuu wa Mafunzo wa DIT, kampasi ya Mwanza, Dkt. Albert Mmari amesema kuwa DIT ilitoa mafunzo kama hayo kwa mafundi simu za mkononi wa Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita na sasa wamejiandaa kutoa mafunzo hayo Mwanza kwa mafundi hao wa Kanda ya Ziwa

Mmari amewaomba mafundi hao kuhudhuria mafunzo hayo na washirikiane na TCRA kuwaelemisha wadau na wateja kupeleka simu zao za mkononi kwa mafundi simu waliopata mafunzo ili kulinda usalama na ubora wa simu zao na vifaa vingine vya TEHAMA

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Simu za Mkononi wa Kanda ya Ziwa, Magua Manyanda amemshukuru Mkuu wa Kanda ya Ziwa wa TCRA, Mhandisi Francis Mihayo kwa kuwakutanisha mafundi hao, kuwaweka pamoja, kusimamia uanzishwaji wa umoja wao na kuwaandalia mafunzo ili waweze kushirikiana na Serikali na mamlaka nyingine kudhibiti uhalifu unaosababishwa na simu za mkononi ambapo mafundi simu wako tayari kushirikiana na TCRA na Jeshi la Polisi kudhibiti wezi wa simu za mkononi na kupitia umoja huo, kwa fundi simu atakayebainika kushirikiana na wahalifu na genge la wezi ataondolewa mara moja kwenye umoja huo.

Chanzo: Michuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamwelwe amewataka mafundi simu kujiunga pamoja ili waweze kupewa leseni na Serikali kutoka TCRA ili waweze kuitumia kununua vifaa vinavyohitajika kutengenezea simu ya mkononi na vifaa vingine vya TEHAMA ambavyo vitakuwa vimeharibika na vinahitaji kufanyiwa matengenezo
Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani kununua vifaa vya simu vikiharibika napo kunahitaji upate leseni na kibali toka serikalini?

Yani mteja alete simu nibadilishe maiki,mpaka nianze omba kibali cha kwenda nunua maiki? ah wee

Kwenye leseni mnataka tu kupiga hela za mafundi ila vifaa vya simu vipo kibao mjini wala sihitaji kibali kupewa

kwani zimekua bastola hizo au risasi?
 
Taifa lenye watu wa ajabu, nawaapia mtakuja kusikia Sasa Tanzania nzima ili uwe fundi simu lazima uwe na kibali na hii sio simu tu ata PC ngoja tuone majambazi watakavyoongezeka.
 
Advancing tech haipatkan huko kweny semina zao mkuu...wakali wa hizi kazi wanaelewa

Sent using Jamii Forums mobile app

Nafikiri inawezekana kwa sababu kupitia semina, watu hupewa elimu ya ziada japo inaweza isiwe kwa kiwango kikubwa lkn pia njia zipi wahusika wapite ili kuweza kutanua ujuzi wa taaluma zao.
 
Semina za TCRA haziwezi kukufanya ukawa fundi mzuri wa simu hapo useme wanataka kodi na siyo vinginevyo. Ukijua Kiingereza + ukaipenda tech hii ndiyo njia ya kuwa fundi mzuri. Kwa ulimwengu wa sasa hivi ni WEWE + COMPUTER + INTERNET mchezo umeisha. Google is my friend
Nimejifunza vitu vingi sana vya ufundi simu, computer, modem na router. Kipindi hicho nilikuwa sijui hata kuflash simu, kuunlock simu, modem au router lakini kupitia rafiki yangu GOOGLE nimejifunza vitu vingi sana. Ulimwengu wa sasa ukiwa na kichwa kizito utaenda kwenye hizo semina, kutafuta mtu kukufundisha, chuo n.k Mambo yote nimejifunza Google

Nami namawazo km yako

Pia ni fursa kwa wale wapya wanaohitaji kujifunza ufundi simu mfano mm hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Semina za TCRA haziwezi kukufanya ukawa fundi mzuri wa simu hapo useme wanataka kodi na siyo vinginevyo. Ukijua Kiingereza + ukaipenda tech hii ndiyo njia ya kuwa fundi mzuri. Kwa ulimwengu wa sasa hivi ni WEWE + COMPUTER + INTERNET mchezo umeisha. Google is my friend
Nimejifunza vitu vingi sana vya ufundi simu, computer, modem na router. Kipindi hicho nilikuwa sijui hata kuflash simu, kuunlock simu, modem au router lakini kupitia rafiki yangu GOOGLE nimejifunza vitu vingi sana. Ulimwengu wa sasa ukiwa na kichwa kizito utaenda kwenye hizo semina, kutafuta mtu kukufundisha, chuo n.k Mambo yote nimejifunza Google
Nifursa kwa tusio na introduction

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iwapo makampuni ya Kujenga simu kama Ya Iphone,Nokia,infinix,Tecno etc yangeshirikiswa yakatoa service software na serivice manuals hapo sawa.DIT baada ya Kufariki Mwalimu Mwarembe(RIP) ni wasanii tuu,enzi za Mwalembe Dar nzima simu walikuwa wanatengeneza pale DIT....fundi simu spea atafute mwenyewe,ramani ya simu TCRA awawapi (TCRA wanatakiwa wawe nazo na pia wajua simu kama inameet specs za Tanzania),unampa fundi Leseni kwa kutumia vigezo gani???????????. niliwai kuwa fundi simu enzi hizo kwa Sapna electronics na freedom electronics........na pia mwalimu wa mafundi simu pale VETA pamoja na Mwalimu Ricky Sambo haya madudu ayakuwepo....guys lets pe serious
 
Hapo kodi inatafutwa wala usiumize kichwa. Wamechukua kundi la watu wachache ili kuwahamasisha wengine waingie kwenye suala la kupatiwa leseni na kuanza kulipa kodi. Wakisema watoe semina hawawezi kumaliza vitu vyote maana ufundi simu unataka mtu anayejua "kujiongeza".
Iwapo makampuni ya Kujenga simu kama Ya Iphone,Nokia,infinix,Tecno etc yangeshirikiswa yakatoa service software na serivice manuals hapo sawa.DIT baada ya Kufariki Mwalimu Mwarembe(RIP) ni wasanii tuu,enzi za Mwalembe Dar nzima simu walikuwa wanatengeneza pale DIT....fundi simu spea atafute mwenyewe,ramani ya simu TCRA awawapi (TCRA wanatakiwa wawe nazo na pia wajua simu kama inameet specs za Tanzania),unampa fundi Leseni kwa kutumia vigezo gani???????????. niliwai kuwa fundi simu enzi hizo kwa Sapna electronics na freedom electronics........na pia mwalimu wa mafundi simu pale VETA pamoja na Mwalimu Ricky Sambo haya madudu ayakuwepo....guys lets pe serious
 
mfano hapo Mwanza kuna fundi Mashaka😁 huyu anatengeneza simu zaidi ya miaka 10 iliyopita! je wanamjua na kuthamini mchango wake katika fani?????.
pale Mbeya kuna Fundi Erick wa Longtime huyu nae anatakiwa akasome au aende semina???je fundi Yahaya na Mwesiga wa Dar nao je????DIT waache usanii wakae chini waje na kozi zenye tija......je fotocopy ,printers,computers...scaners,Flat TV LED etcMAfundi wa kufunga madishi ya DSTV Startime etc....mafundi wanasomea VETA au DIT kwa sasa??.......akuna ata mmoja wao mwenye hizi kozi.........
 
Lesseni?? Kisha kwa mwaka ulipie lesseni yako,bado TRA nao hawatakua nyuma kudai kodi.Kama lengo ni kukusanya mapato basi wawape vitambulisho vya ujasiliamari
 
sad news.. TCRA wanadhani mafundi wote ni darasa la saba or form 4.. unakuta anayekufundisha umempita hata hyo elimu au upo naye sawa mpaka experience..DIT unarudi kusoma ufundi simu wanakufundisha basic electronics kwq m2 ambaye ameenda chuo ni holder wa diploma or degree unamrudisha kwenye basic electronics cjui point ipo wapi.. ifike pahali kuna wa2 washasoma sana. Waweke vigezo kwa m2 mwenye level fulani ya elimu awe anauwezo wakuomba licence moja kwa moja bila yakupitia hayo mafunzo maana almost 80% ya mafunzo washapitia kipindi wanatafuta elimu zao.
unakuta fundi ana degree or diploma (electronic/electrical or IT)na ana experience karibia 3yrs and more.. huyu unaenda kumfundisha nini chuo? Zaidi yakumpotezea muda wakufanya movement zake.Rules and regulation hazizidi hata page 5 ss hili sio jambo lakumpeleka m2 college. Na kwauzoefu wangu.. vyuo vyote vinafundisha basic 2 especially ngazi ya cheti... sasa wa2 washasoma hizo basic miaka kibao nyuma leo hii wanaleta story yakurudisha watu darasani.alafu chamwisho anayema mafundi hawalipi kodi.. anaakili timamu kweli... kwani c anakuwa na frame na licence ya municipal au ulitaka alipe kodi gani.. Mwisho wa cku huwezi endesha nchi kwa kodi za wananchi.. tafuteni njia zengine zakuongezea kipato wizara zenu.
 
Tcra Malengo yao ni kufundisha hasa mambo ya sheria za mtandao
Baada ya kuwauliza mimi nina degree na nimesoma Electronic wakasema lazima usome

Wanasahau wengine tumesoma na subject inaitwa electronic law sheria zote za makosa ya mtandao, electronic and postal communications act, 2010,na ile ya 2018,
Tatizo bado lipo wanataka ukiletewa simu hasa ya kutoa password basi udai listi mteja akuonyeshe listi ya kununua lia hiyo simu watanzania wangapi wanazo

Polisi na tcra wengine masikini hawajui neno flash, unlock, na password reset ni vitu tofauti

Tanzania bado tunasafari ndefu mahakimu nao wapo nyuma sana na teknolojia hapo ndipo mambo huwa moto
Kubadili imei ni kosa lakini kuflash sio kubadili imei ila utaona wanasema ameflash kafanya kosa
Wanatumia kifungu kwenye sheria ya Electronic and postal communications act 2010 kifungu 129 kuhusu Tampering with mobile telephones and SIM card
Hapo tunahitaji kukaa chini kwa pamoja kuona njia bora ya kufanya mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iwapo makampuni ya Kujenga simu kama Ya Iphone,Nokia,infinix,Tecno etc yangeshirikiswa yakatoa service software na serivice manuals hapo sawa.DIT baada ya Kufariki Mwalimu Mwarembe(RIP) ni wasanii tuu,enzi za Mwalembe Dar nzima simu walikuwa wanatengeneza pale DIT....fundi simu spea atafute mwenyewe,ramani ya simu TCRA awawapi (TCRA wanatakiwa wawe nazo na pia wajua simu kama inameet specs za Tanzania),unampa fundi Leseni kwa kutumia vigezo gani???????????. niliwai kuwa fundi simu enzi hizo kwa Sapna electronics na freedom electronics........na pia mwalimu wa mafundi simu pale VETA pamoja na Mwalimu Ricky Sambo haya madudu ayakuwepo....guys lets pe serious
Hii semina mwalimu Rick Sambo ndo anaefundisha mpaka sasa ashazunguka tz nzima
 
Back
Top Bottom