Mafunzo mapya ya practical ya electronics 25/10/2014

Mafunzo mapya ya practical ya electronics 25/10/2014

Transistor

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,061
Reaction score
1,640
Habari wanajamvi,

Kuna wadau wamekuwa wakiulizia Workshop ya electronics nyingine ni lini,jibu ni kwamba workshop kwa sasa haita kuwepo hadi mwakani,kwa sababu kuandaa workshop ni gharama hasa katika swala zima la kukodi ukumbi kwa siku kadhaa.Harafu mara nyingi nakua sina wadhamini zaidi ya kampuni yangu hivyo inacost sana.


Workshop hii itakuwa inafanyika lakini kwa interval ya muda wa mienzi miinne hadi mitano ili niweze kujiandaa kidogo.


Pia kitu kingine naomba itambulike kuwa sisi tunatoa mafunzo ya kukufanya uanze kuunda vitu vinavyo hitajika sokoni na si elimu tu!

Kuna baadhi ya wadau wamemaliza vyuo vya VETA na vyuo vikuu katika mlengo wa electronics;napenda kuwaambia kuwa mafunzo haya ni muhimu sana kwao kwani hii si elimu ya darasani ni elimu ya duniani!

Vifaa vingi ambavyo jamii inahitaji kutengenezewa vipo katika mifumo ya juu zaidi ya kiusalama na ubora zaidi ya kile tulicho jifunza huko vyuoni!

Nimekuwa nikipokea baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao kabla ya kuanza mafunzo huonekana kujiamini sana;kuna mmoja aliniambia nimpe tu certificate of atendance kwani tulicho taka kujifunza yeye tayari chuo wamejifunza;

Kampuni ilimshauri japo akae tu darasani wakati wa theory na practical akae tu aangalie jinsi wenzake wanavyo jifunza lakini jinsi tulivyokuwa tuinaendelea ndivyo akaanza kuona tofauti kati ya elimu aliyonayo na elimu inayo tolewa!

Pia ijulikane kuwa katika dunia harisi vifaa vingi vya kielectronics vimebadilika,wakati ukweli usiopingika ni kuwa mashuleni bado wanatumia vitabu vya muda wa zamani kidogo hivyo ukija katika uharisia unakuta kuna mambo mengi unatakiwa kuyajua na kuyafanyia kazi licha ya kuwa kanuni za umeme zinabaki vilevile!

Mwanafunzi huyu wa chuo baada ya kuona hivyo Ikabidi ajiunge na wenzake ingawa kuna wadau wengine walikuwa hawajawahi kujifunza kabisa elimu ya electronics semina ile ndio ilikua darasa lao la kwanza lakini walikua makini na saketi zao zilikamilika mapema na kufanya kazi vizuri kuliko ndugu yangu aliye graduate ambaye hadi giza lilitukuta bado saketi yake haitaki kufanya kazi inayo kusudiwa.

Tukumbuke kuwa vyuoni na mashuleni tunajifunza simple projects lakini ukija katika dunia harisi mambo ni tofauti ndio maana mafunzo kama haya yakawepo!

Mimi mwalimu wangu wa electronics aliye nifundisha wakati nasoma VETA enzi hizo sasa hivi kuna vitu naye anakuja kujifunza kwangu;hivyo kuku bali kuelimika zaidi sio ujinga ila ni utayari wa kwenda na wakati.

Mimi mwenyewe na Degree ya electronics lakini kila siku najifunza zaidi na zaidi kuna wakali kibao duniani hapa ambao ndio wananijaza vitu vipya kila siku hivyo hata mimi mwenyewe najifunza.

Hivyo nawashauri vijana wenzangu tupende kujiongeza.



Kutokana na kwamba workshop ya electronics haita kuwepo kwa muda mrefu tumeona bora tu-compasate kwa wale wanao hitaji kujifunza Electronics tumetafuta sehemu ambapo tutakuwa tunafanya mafunzo yetu pale.

Mafunzo haya yatakuwa na lengo la kukupa ujuzi kwa vipengele flani tu ambavyo utakuwa umeomba;

Mfano ukitaka kujifunza namna ya kuunda Solar charger control utafundishwa hiyo tu,kwa nadharia na vitendo.ukiweza kuiunda vizuri ndio unaweza kuomba kipengele kingine.

Mafunzo yetu hayabagui swala la elimu ya mtu.


Kumbuka mafunzo yetu ya nadharia ni BURE mtu kama akielewa theory na akataka kuendelea na practical hapo ndipo itamlazimu agharamikie vifaa vya kufanyia mafunzo kwa vitendo.


Pia mwanafunzi atapata Elimu na mbinu za kijasiriamali kupata soko la bidhaa zake ambazo atakuwa anaziunda.


Tunatoa certificate of attendance kwa Yule tu aliye fanya na kumaliza mafunzo ya nadharia na vitendo kupitia

kampuni ya electronics ya MES

Mafunzo mapya yataanza Tarehe 25 October 2014 mafunzo haya yatakua katika vipengele vya;-
- Uundaji wa Voltage Stabilizer
-Uundaji wa Miziki mikubwa ya kwenye magari
-Uundaji wa Security systeme(za nyumba na magari)
-Uundaji wa solar control Charger
-Uundaji wa Auto back up Battery control charger
-Uundaji wa soft power inverter

Kama una kitu unataka kujifunza hakijaandikwa hapa unaweza kupendekeza.


Kila kipengere kina gharama yake na muda wake wa kujifunza,kwa kila kipengere gharama za kujifunza theory ni BURE!


Kwa taarifa za mafunzo ya mara kwa mara uwe unatembelea blog yetu hii HAPA.


Kama unataka kujifunza Wasiliana na mimi transistor kwa namba hii 0657-115587

Au fika ofisini kwetu Segerea Junction along Kinyerezi road


Tuko vizuri kutoa mafunzo ya theory na practical kuna wadau humu humu wamesha jifunza nasi na wame-appriciate!


Mtaarifu ndugu jamaa na rafiki yako.


ELIMU NI MSINGI WA KIPATO KWA MTOTO WA MASKINI!Karibuni!,
 
Back
Top Bottom