Abby's
Member
- Jun 17, 2015
- 45
- 19
MAFUNZO YA HALI YA HEWA (TABIA YA NCHI)
By: Abineri Mwanuke
KARIBU KATIKA MAFUNZO YAHUSUYO MABADILIKO
YA TABIA YA NCHI.
FIGHT AGAINST GLOBAL CLIMATIC CHANGES
COMPAIGN
Tembelea:
www.tanzaniamynation.blogspot.com
Facebook:
A-newz classic
Abineri Wa Santina
SEHEMU YA KWANZA.
TABIA YA NCHI NI NINI?
(What is climate).
Tabia ya nchi ni wastani wa hali ya hewa ya mahali
fulani ambayo inarekodiwa kwa kipindi kisichopungua
miaka 30.
MABADILIKO YA TABIA YA NCHI NI NINI?
(What is global climatic changes?)
Ni kubadilika kwa hali ya hewa kiujumla katika eneo
fulani, inaweza kuwa mkoa, nchi, bara na hata dunia
kwaujumla. kwamfano; kama tabia ya nchi ilikuwa ya
kiikweta inabadilika na kuwa ya kitropiki au kutoka hali
ya kitropiki inabadilika na kuwa ya kijangwa.
Mabadiliko haya sasa yamekuwa yakijitokeza na
kushuhudiwa kwa sana katika dunia nzima kitu kibaya
zaidi ni kwamba mabadiliko haya yamekuwa
yakijitokeza katika dunia na kuleta athari hasi, yaani
dunia nzima imekuwa ikibadilika na kuelekea katika hali
ya ujangwa.
Jambo hili linabainika katika uwepo wa mvua
zisizotosheleza mahitaji ya shughuli za binadamu na
pia
zisizo za kutabirika au kutokuwepo kabisa katika
baadhi
ya maeneo.
Pia ongezeko la joto duniani(Global warming), kupotea
kwa baadhi ya wanyama na mimea au viumbe hai (loss
of biodiversity) yote hii inaonesha kuwa kuna
mabadiliko ya tabia ya nchi.
Katika Tanzania maeneo mengi yamekuwa yakikosa
mvua za kutosheleza shughuli za maeneo hayo na
mengine kukosa kabisa, hii ni hali ngeni kabisa katika
nchi yetu hivyo jitihada zinatakiwa kuchukuliwa ili
kupapambana na tatizo hili.
Kwa namnamoja ama nyingine hakuna kinachobadilisha
tabia ya nchi isipokuwa ni binadamu mwenyewe na
shughuli zake ambaye amekuwa akijitengenezea
mazingira ambayo hayatakuwa rafiki katika maisha
yake na kwa vizazi vijavyo. kwa kiasi kikubwa
mbadilishaji wa tabia ya nchi ni sisi binadamu
wenyewe
ambao tumekuwa tukifanya mambo bila ya kujua kuwa
yanatubadilishia tabia ya nchi ambapo mabadiliko
hayo ni hatari kwa maisha yetu.
MAMBO YANAYO SABABISHA MABADILIKO YA TABIA
YA NCHI. (FACTORS LEADING TO GLOBAL CLIMATIC
CHANGES).
mambo hayo ni:
1. Ukataji wa miti bila kupanda tena (defforestation)
hili ni tatizo kubwa duniani kote. ukatajo ovyo wa miti
umekithiri na kiwango cha ukataji miti ni kikubwa zaidi
ya kiwango cha upandaji miti.
kwanini tunahimiza "kata miti panda miti" na ni kwa
namna gani miti inabadilisha tabia ya nchi?
Miti ina kazi kubwa katika kutunza tabia ya nchi
kwakuwa inafanya kazi ya kufyonza hewa ya ukaa
(carbondioxide_CO2) ambayo inamadhara kwani
huweka utando katika tabaka la ozoni hivyo kupelekea
joto kuongezeka duniani, hivyo miti huifyonz hewa hii
na kutoa oksijeni (oxygen_O2) ambayo huunda au
huimarisha tabaka la ozoni na kutuepusha na ongezeko
la joto duniani.
Lakini suala hili la ukataji wa miti limekuwa ni tatizo
sana, Shirika la utawala wa anga la Marekani lilitoa
taarifa kwamba kama ukataji wamiti utaendelea kama
hali ilivyo sasa basi baada ya miaka 100 misitu yote ya
kiikweta itakuwa imepotea kabisa, Na hivyo ndivyo
maradhi yatakavyo zuka na kuimaliza dunia kutokana
kuongezeka kwa joto.
Afrika imekuwa ikipoteza hekta nyingi sana za miti na
hii ni kutokana na matumizi ya nishati itokananoayo na
miti yaani kuni na mkaa lakini pia kwasababu ya uhitaji
wa ardhi kwaajili ya shughuli nyinginezo. mpaka sasa
Afrika magharibi imekwisha poteza 90% za miti na hii
ni hatari kwa maisha ya watu na viumbe hai.
kunasababu ambazo binadamu wanazitumia hizo
kukata au kupoteza miti nazo ni kama vile:
i. Shughuli za kilimo
ii. Upataji wa magogo kwaajili ya shughuli mbalimbali
kama vile kutengenezea karatasi, matumizi ya
viwandani, ujenzi n.k
iii. Matumizi ya kuni na mkaa ambayo ni zaidi ya 10%
ya miti inayokatwa.
iv. kupata maeneo kwaajili ya shughuli za kiufugaji.
Kwa ufupi, kupotea huku kwa miti kunasababisha
ongezeko la hewa ya ukaa (CO2) ambako
kunaizamisha
dunia kwenye matatizo makubwa, kwasababu misitu au
miti inamchango katika kutokea kwa mvua kwani hutoa
maji kwa njia ya mvuke(Transpiration) ambapo maji
hayo husaidia katika kutokea kwa wingu na hatimaye
mvua.
ITAENDELEA.
ENDELEA KUFUATILIA UELIMIKE, PIA SHARE NA
WENGINE WAIPATE NA TUWAFIKIE WATANZANIA
WENGI.
TANZANIA BILA NJAA, INAWEZEKANA.