Mafundisho Ya Kikristo Yasio na Uhalali Kibiblia

Mafundisho Ya Kikristo Yasio na Uhalali Kibiblia

Kalamu Nzito

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Posts
376
Reaction score
850
Kuna baadhi ya mafundisho yanaenea katika Ukristo ambayo hayana msingi wowote kwenye Biblia

1. KUAMURU MALAIKA (COMMANDING THE ANGELS)

Kuna baadhi ya watumishi wanafundisha waumini kuamuru Malaika kufanya mambo fulani. Jambo hili ni kinyume kabisa na maandiko kwani Malaika ni watumishi wa Mungu (Servants of God) na sio watumishi wa wanadamu. Mungu ndo anaamuru Malaika wake na sio mwanadamu.

2. TOA SADAKA INAYOKUUMA.

Kuna watumishi wanafundisha kwamba ili ubarikiwe na Mungu, lazima utoe sadaka inayokuuma. Hata hivyo, Biblia haifundishi kitu kama hiki. Maandiko yanahimiza kutoa kwa moyo mkunjufu (2 Wakorintho 9: 7) ukiona unaumia kwa kile unachotoa tayari unakua umekiuka kanuni ya utoaji.

3. KUOMBA KWA WATAKATIFU WALIOKUFA

Kuna mafundisho kwamba watakatifu waliokufa wanasikia maombi yetu na wanayasogeza mbele za Mungu. Hata hivyo, kwenye Biblia hakuna mafundisho ya aina hiyo. Wengi wanatumia mstari kutoka Ufunuo wa Yohana 5:8 kuteta hoja hii. Hata hivyo, msitari huo hautoi ufafanuzi wala mamlaka ya moja kwa moja kwamba tunaweza kuomba kwa watakatifu waliolala. Kitabu cha Ufunuo kimekua kikitumika kuhalalisha taratibu ambazo kimsingi zimepotoshwa ili kuendana na matakwa ya kibinadamu.

Yesu Kristo alishaweka mamlaka juu ya jina lake na akasisitiza kuomba kupitia yeye (Yohana 14: 14). Roho Mtakatifu ambaye Yesu alituachia ndiye muombezi wetu ambaye hutusaidia kuomba kwa kuugua kusikoweza kutamkwa (Warumi 8: 26-27).
Hata kama watakatifu wapo Mbinguni, hawana jukumu la kupokea wala kusikia maombi. Hakuna mtu yoyote kwenye Biblia aliwahi kuomba kwa Mitume waliokufa. Haya ni mapokeo ya kibinadamu.

BARIKIWA!
 
Kuna mahali kwenye Biblia umeambiwa Ukienda chooni kunya uchuchumae? Au Ukiamka asubuhi upige mswaki? Au mchungaji/Padre avae Joho/kanzu? Nani kakufundisha hayo?
 
Mwamposa mwenyewe anakwambia toa sadaka ujimalize, usibakize hata nauli.
Kama unakaa Chanika basi utoke kawe mpaka Chanika Kwa miguu.
Hiyo ndiyo sadaka inayouma na Mungu anakujibu haraka maombi Yako
 
Kuna mahali kwenye Biblia umeambiwa Ukienda chooni kunya uchuchumae? Au Ukiamka asubuhi upige mswaki? Au mchungaji/Padre avae Joho/kanzu? Nani kakufundisha hayo?
Nadhani mleta mada ameleta mambo ambayo yanafundishwa makanisani na hayana msingi kwenye Biblia.

Sasa wewe mambo ya kunya umeyatoa wapi? Au kanisani kwenu mnafundishwa kwenda kunya?
 
Tuwaache hawa ndug zetu wametuzidi kilakitu... Tupambane sisi kujikomboa kifikra na kiuchumi
 
Kuna mahali kwenye Biblia umeambiwa Ukienda chooni kunya uchuchumae? Au Ukiamka asubuhi upige mswaki? Au mchungaji/Padre avae Joho/kanzu? Nani kakufundisha hayo?
Biblia ni muongozo wa maisha ya kiroho unaoimarisha uhusiano wa mwanadamu na Mungu. Kunya, kupiga mswaki, kuvaa joho je hayo ni sehemu ya maisha ya kiroho katika kujenga uhusiano na Mungu?

Lakini tunapozungumzia namna ya kuomba, namna ya utoaji nk! Haya yote ni mambo ya kiroho na hakika utaratibu umeainishwa vyema kwenye maandiko.

BARIKIWA!
 
Nadhani mleta mada ameleta mambo ambayo yanafundishwa makanisani na hayana msingi kwenye Biblia.

Sasa wewe mambo ya kunya umeyatoa wapi? Au kanisani kwenu mnafundishwa kwenda kunya?
Unaposema hayana msingi kwenye Biblia una maana gani? Unadhani kila kifanywacho katika Ukristu lazima kiwe na msingi kibiblia? Biblia ni summary na muongozo wa maisha ya kikristu na laiti kama yangeandikwa yote hakika vitabu vya ulimwengu visingetosha, Kuna Injili nyingi mpaka Injili ya Barnaba ipo. Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa "Mapokeo" ambapo tunafundishwa kulingana na uhalisia na maisha yalivyokuwa na tunavyopaswa kuishi, Nimekutolea mfano, Wapi Kwenye Biblia imeandikwa padre/mchungaji avae joho? Kwa hiyo haina uhalali wala msingi kibiblia na hawatakiwi kufanya hivyo? Watakatifu wapo na Daima wanatuombea kwa Mungu.
 
Bahati mbaya Sana mkuu umenijibu maelezo marefu Sana wakati siamini kama Biblia ni kitabu aliandika Mungu.
Ngoja watu wa Dini waje wakujibu 🤣🤣🤣
 
Biblia ni muongozo wa maisha ya kiroho unaoimarisha uhusiano wa mwanadamu na Mungu. Kunya, kupiga mswaki, kuvaa joho je hayo ni sehemu ya maisha ya kiroho katika kujenga uhusiano na Mungu?

Lakini tunapozungumzia namna ya kuomba, namna ya utoaji nk! Haya yote ni mambo ya kiroho na hakika utaratibu umeainishwa vyema kwenye maandiko.

BARIKIWA!
Sijui kama unajua unachokizungumza, unaposema mambo ya kiroho una maana gani? Hakika hapa ndipo ninapolikubali na kuliheshimu Kanisa Katoliki, Ukristu/Ukatoliki ni mfumo wa maisha kiujumla kimwili na kiroho katika kutimiza lengo la kufika mbinguni, Mambo ya kimwili na kiroho yote yanashabihiana, Ndiyo maana Ulevi, Uzinzi, Wizi nk. Yote yanafanyika katika mwili na kuacha alama katika roho, Kwahiyo Biblia sio tu mwongozo wa kiroho ni muongozo wa maisha ya mkristu, kila siku ya namna anavyopaswa kuenenda.Kula, Kulala,Kuamka,namna ya utoaji, namna ya kuomba nk. Yote ni sehemu ya maisha mbele ya Mungu, sasa wewe sijui una maana gani kujaribu kutofautisha.
 
Back
Top Bottom