Carina
Senior Member
- Jan 4, 2011
- 194
- 71
Habari za leo wanandugu,
Nina friji yangu kila nikiiwasha tu umeme unazima nyumba nzima (circuit Braker inafanya kazi yake)nikatafuta fundi wa kwanza akasema compressor ina matatizo, nikaona ngoja nitafute fundi wa pili naye akasema compressor ina matatizo. katika kuulizia ulizia kwa washkaji nao wakasema inaweza ikawa kweli compressor imekufa au inawezekana ni kidude kidogo tu kwenye compressor hakifanyi kazi ni cha kubadilisha tu sio lazima ununue compressor nzima.
Kufika hapo naona kama sijaelewa vizuri, hivyo nimekuja jamvini kupata ushauri safi najua huku kuna wataalam sana wa mambo ya friji wa kunielekeza kwanza ni wapi wanapatikana mafundi wazuri wa friji na kama ikatakiwa ninunue compressor ni wapi wanauza compressor za friji za uhakika (Original)
Kuna kitu kinaitwa Fridge Guard nasikia ni nzuri sana kuliko stabiliser kwani mimi nilikuwa natumia stabiliser lakini ndio hiyo imeua compressor.
Ushauri jamani