Mafundi simu ni wezi wa memory card

Mafundi simu ni wezi wa memory card

kibuyu180

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2016
Posts
1,778
Reaction score
1,907
Mimi binafsi nimeibiwa tatu mpaka sasa. Bahati yangu huwa zinakuwa na nyimbo na picha za kawaida tu. Juzi rafiki yangu nao kakutana na wizi wa memory card, kapeleka simu yake kwa fundi, nikamwambia atoe kabisa memory card. Akasahau kuitoa. Baada ya siku tatu akaipitia simu yake kwa bahati mbaya hakukagua memory. Kufika home kucheki hamna.

Kumwambia fundi, fundi kasema hakuichukua wala kuiona. Ukweli mafundi simu uiba memory card za wateja. Kwa kuziuza tena kwa wateja wengine. Ama kuvujisha picha ama video.

Nawashauri kabla ya kumkabidhi fundi simu toa memory card yako.
 
Hakuna fundi simu mwenye njaa ya kuiba kitu kma memory card,huwa zinapotea Tu,memory card Ni kitu cha bei ndoto mno,32gb Ni 18000,
 
Huko kwa Fundi simu unapeleka kutengeneza simu au memory card?
 
Watu hutofautiana kwako ww unaweza ukaona ni k2 kidogo sana lakin kwa mwenzio kina thamani na ni kwl mafundi wengine hawawez kuiba hila baadhi yao huiba hata kukubadilishia v2 tu wanabadilishaga mafundi wengine wezi tuuu
 
Mkuu hakuna hicho kitu
Huo na-consider ni uzembe wa mmiliki wa simu .

Ofisi kwangu lilikua lipo tangazo kubwa

1.ndugu mteja hakikisha unaondoka na simcard/memory card/betri ya simu yako.

2.hatuna dhamana na vitu hivyo, ukiviacha simu imiwa kwenye matengezo hatutahusika na upotevu wowote
 
Hakuna fundi simu mwenye njaa ya kuiba kitu kma memory card,huwa zinapotea Tu,memory card Ni kitu cha bei ndoto mno,32gb Ni 18000,
18000 kwa Fundi simu ni kubwa ukizingatia ujira wake wa kutengeneza unakuta haifikii hata hiyo.
 
Hakuna fundi simu mwenye njaa ya kuiba kitu kma memory card,huwa zinapotea Tu,memory card Ni kitu cha bei ndoto mno,32gb Ni 18000,
Ni wezi sana, mi nilipeleka simu kwa fundi ikiwa na memory ya 8gb, ndani ikiwa na album tano za wenge musica, siku nachukua simu sikuwa na wasiwasi ila nimefika nyumbani kutaka kusikiliza nyimbo pendwa hakuna kitu, kuangalia memory sio yenyew ina 2gb nikajua tayari nishalizwa.
 
Mi kwa Fundi wangu wa kitaa huwa ni 10000,15000 au 20000 kwa matatizo ya kawaida.
Hizo ni bei standard ila simu inavyokuwa ya gharama kubwa ndio bei inapanda,

Mfano ; network ya tecno ni 15000 ila network lock ya simu kama galaxy s6 edge ni 50000,

Kutoa screenlocks ni 15000 ila kutoa passcode ya iphone ni kuanzia 20000-35000 ikitegemea na aina ya iphone..
 
ww mwenyewe na huyo rafiki yako in wazembe,,,nijuavyo mm ukipeleka simu kwa fundi anakuambia toa m,card
 
Back
Top Bottom