Mafundi makochi Mungu anawaona!

Mafundi makochi Mungu anawaona!

Unakuta kochi limemaliziwa vizuri linang'aa na kitambaa safi cha nguo, turubahi, au ngozi. Utadhani limetengenezewa Ulaya! Utapigwa hela ndefu seti 1.5million mpaka 5m. Sasa lipeleke nyumbani watoto waanze michezo yao! Utasikia mara ndani mbao zinaanza kukatika mara ukikaa unadumbukia kwenye uwazi/ shimo ndani ya miezi sita magodoro kama chapati na kuacha ngozi tipwatipwa kama ngozi ya mzee!

Niliwahi kununua makochi ya mnada pale British council Mitaa ya Posta huu mwaka wa 7 bado safi kama mapya nikiyasafisha na kuyapiga dawa fulani hivi ya kusafishia siti za gari.

Kwanini mafundi wa kiswahili mnashindwa kuwa wabunifu na kujiharibia soko? Nenda stoo za watengeneza makochi utakuta kochi kama lisiponunuliwa litaharibikia nyanga nyanga hapo hapo showroom bila hata kutumika kwa kuoza au kuliwa na mchwa kutokana na mambao chakavu wanayotumia.

Mafundi makochi badilikeni!! Mnashindwaje hata kuchukua/ kununua kochi moja la mtansha/mzungu mkadesa kalitengenezaje? Nenda hata pale 'Danube' Mlimani City chunguza yalivyotengenezwa na nyie tengenezeni hivyohivyo! Vinginevyo njaa zitawauma na kuwafichua hadi uvunguni.

Sasa kama kumbe nia yako ilikuwa Kuupigia Promo Mnada wa British Council na kulipigia Promo Duka la Danube kwanini umepita njia ndefu sana Mkuu?
 
Popote ulipo fundi sofa wangu wa pale Tandika Mungu azid kukubariki.
Nina sofa set flan ya kwanza ambayo nilianzia life nikiwa mwananchuo ile ki gheto, mpaka leo ipo nondo imesimama sana.Mpaka leo.

NB.
Nikifika level za ku acquire furniture pale mlimani city nita leta mrejesho maana hata keko tu bado siwez mudu.
Ahahahahahahaha
 
Mimi bado mshamba, ninakalia makochi ya mbao tena mninga safi, nikiyawekea mito ya ngozi utayapenda bure. Watoto wanachezea mpaka wanapata akili bado yamo.
Mimi mwenyewe nimeshakata shauri sofa za ngozi sitaki tena. Nimeshanunua sofa 3 tofauti tena kwa mafundi wanaoaminika na zote sasa ziko nyang'anyang'a. Nachotaka ni kutafuta design nzuri ya makochi ya mbao yenye mito nitengeneze. Mkuu kama hutajali hebu niyaone hayo yakwako
 
Kuna haja gani ya kununua Kochi za kukalia za mamilioni wakati mikeka ya elfu tano ya kukalia ipo
 
Natafuta sofa simple jamani. Seti mbili za kukaa watu wawili wawili. Natapatikana Ubungo. Bajeti yangu 300,000 sofa mbili zote.
 
Toka lini watu weusi wanaweza kutengeneza sofa na lidumu mwaka?
 
Back
Top Bottom