this news is as old as....Mafisadi wazidi kumtishia JK baada ya kuonekana anataka kuwamaliza kwa kusimamia kufutwa kwa wagombea wa Vijana wa Bara na kuwapa wa Zenji nafasi .Kufuatia ujumbe uliotumwa kwa JK baada ya Kikao cha NEC wamesema kwamba wakao tayari kuja na Chama mbadala na kuachana na CCM kama JK atazidi kuwabana na hata kushindwa kumpata Katibu Mkuu wa Vijana .JK akiwa wazi kwamba anamtaka Kawawa achukue uongozi basi Mafisadi wamesema lazima kieleweke .
Wameamua sasa kumvaa possible mwenyekiti kati ya wale vijana 3 wa Zanzibar na jina tutaliweka hapa kwa uwazi muda si mrefu .Mafisadi wanasema watakula naye na lazima aelewe kwamba wao wako na wanataka kumtumia effectively akisha ukwaa ukubwa .Ngoma ni nzito na CCM si shwari .
Yangu macho sasa naangalia mwenendo mzima na saga hili huku kukiwa kumeitishwa kikao cha ghafla na tunatafuta yaliyomo .
More to come and stay tuned maana ufisadi sasa unaenda ikumba Zanzibar
Mkuu Lunyungu,
1. Tupo ukurasa mmoja, hapo wameamua ku-invest kwa kijana nayeitwa Masauni.
2. Wamemtaka awaachie nafasi ya katibu mkuu, ama sivyo watajitoa chama, na kwamba asithubutu kabisa kumuweka Nape kwenye hiyo nafasi, kama anafikiria hivyo.
3. Kikao cah wabunge wa CCM na chini ya Pinda na Sitta, kilikuwa leo mchana saa saba, Makamba apigishwa mchaka mchaka na wabuneg ambao wamedai hawawezi kwenda naye kwenye uchaguzi ujao 2010, ya Tarime yametosha.
Mkuu Lunyungu, huenda tunapata habari mahali pamoja, maana sio siri umenishitua bros, labda tu-linganishe notes cheki PM.
Dataz zingine za kikao, later zikipatikana!
Muungwana analo jina la katibu anayemtaka tayari, ambaye Jumamosi alikutana kwa faragha na rais Karume kupanga mikakati mipya, na you got it right Karume ameapa kuwa atakufa na any fisadi atakyejaribu kuwagusa wagombea kutoka huko, kampeni ya Z.Kawawa imeshaanza tayari.
Lete habari huko Mkuu Lunyungu!
Samwel doe naye wakati anapindua nchi alitumwa na mafisadi ili akishatekeleza hilo azimio la kumuua rais awape mafisadi hao nchi,lakini yeye alichofanya baada ya kumuuwa rais akajitangaza yeye ndie rais mafisadi yale akayatupilia mbali.
Rais wa poland mwenye elimu ya veta VAWESA(WAŁESA) naye alitumwa na maprofesa mvua kwenda kutekeleza azimio lao na akimaliza kazi yake awakabidhi hao maprofesa nchi,lakini baada ya kupata nchi akawa yeye rais na kumitupilia mbali mi prof.
Sasa swali kama mafisadi ndio wamemweka JK ulingoni yeye anashindwa nini kufanya kama wałesa na doe??
Lakini si unakumbuka yaliyomkuta doe? kwa hiyo unataka JK afanyiziwe kama doe?
Lakini pia WAŁESA hakuna yaliyomkuta mpaka leo yupo anapeta mtaani.Kwanini JK yasimkute ya WAŁĘSA??