Mafisadi waogopa mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi waogopa mahakama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, May 17, 2011.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Baada ya Dr. Slaa kuwatangazia watanzania watu wanaoimaliza nchi kwa kuibia fedha za umma, ama kwa kubebwa ili kuiba, ama kujitajirisha kwa migongo ya kodi zetu kwa njia za udanganyifu. Ama kutumia vyeo na nafasi zao au za ndugu zao kuwaibia wavuja jasho walitishia kwenda mahakamani. Wengine siku saba, na wengine hawakutoa siku.

  Kubwa zaidi Mtoto wa kiume wa Raisi aliitisha vyombo vya habari na kukanusha ubilionea huku akiwaita waliomwita bilionea majina ya ajabu. Sasa siku saba zimekwisha na zaidi hatumwoni tena mahakamani. Je tuelewe nini. Ubilionea aliombiwa anao ni kweli, na ameupata kwa njia gani? kama si kweli kwa nini mpaka leo anaogopa mahakama?

  Wito tayari tumeambiwa hawa watu ndio wanatufilisi, nao wameshindwa kujitakasa, kwa maana nyingine wanakubali kuwa wanakula jasho letu. Je tuwafanyeje kama raia wa nchi ambayo inaliwa? Fedha hizi ndizo zinatumika kunyanyasa uchumi wetu na njia zote ambazo zinaweza kutuletea maendeleo. Fedha zao ndizo zinazalisha viongozi wasio wazelando na vibaka wa mali ya umma.

  Orodha ya mafisadi inapaswa itafutiwe adhabu za kimila ili kukomesha tabia kama hizi.
   
Loading...