Hakuna shaka Kikwete ana uwezo wa kubadilika na kuwa mkali na mtu wa msimamo wa juu kama akiamua. Lets just hope hajaropoka and then aishie kukamata dagaa badala ya mapapa wa ufisadi. He has put himself to a test in the eyes of watanzania. na huu mtihani ataupita kama ataacha huo ubia ambao anawadanganya watanzania kwamba hana wakati kilichompa nafasi ya uongozi wa serikali (sio nchi au taifa), ni mafisadi.
Kikwete hajachafuka bado, hilo halina mjadala. Kwahiyo kutokana na political crisis iliyopo, tulitegemea afanye kitu cha maana kwenye huo mpitisho wa wagombea NEC (huu haukuwa uchaguzi hata kidogo ulikuwa ni mpitisho), lakini as long as as ametoa ahadi kushughulikia mafisadi, labda tumpe muda kidogo. Lakini subira yetu hii tunataka izae matunda na mafisadi wa BOT na mikatba ya madini na umeme washughulikiwe.
Asisahau kwamba kuna nchi, taifa na serikali na yeye na wenzake hao wa mtandao wenye kukatia viuno mchiriku kutokana na kupitishwa NEC [picha za mchiriku zipo kwenye gazeti la Mwananchi] katika haya matatu ya taifa, nci na serikali, wameshika moja tu - serikali.
Kwanini uchaguzi ulimalizika usiku na matokeo kulala hadi kesho yake? jib ni rahisi sana. usiku ule mafisadi hawakulala. walikuwa busy wakipitishana na kupeana kura nyingi ili waonekane wana support kubwa ndani ya chama.
Kweli ccm kuna utamu. Hata mzee malecela anafikia hatua ya kusema kama akibaki mwanachama mmoja wa ccm basi atakuwa yeye? All this is not coincidence. At 73 years old, he must be expecting aidha pesa za BOT kama za mzindakaya akafungue mashamba yake ya mazabibu huko ugogoni au atatengenezewa cheo cha kumtunza.
Chama cha mapinduzi kitadumu. Ila viongozi wake wa sasa wameishiwa fikra sahihi.