Mafia

mzurisana

Senior Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
133
Reaction score
27
nauliza kwa ambao washawahi kwenda mafia mnapita wapi kwenda kwa boti? kwa kutokea dar mnapandia wapi boti na nauli zikoje? na usalama? nataka niende kutafuta opportunity za biashara huko
 
nauliza kwa ambao washawahi kwenda mafia mnapita wapi kwenda kwa boti? kwa kutokea dar mnapandia wapi boti na nauli zikoje? na usalama? nataka niende kutafuta opportunity za biashara huko

mafia nenda kwa ndege ndugu, ni 90000/= . Ni ndege ndogo na ikiwa angani kama trekta sometym... Ila ni bora kuliko mashua
 
nilidhani unamaanisha lile genge la uharifu. Hongera kwa uzuri lakini
 
Piga mbizi...

nauliza kwa ambao washawahi kwenda mafia mnapita wapi kwenda kwa boti? Kwa kutokea dar mnapandia wapi boti na nauli zikoje? Na usalama? Nataka niende kutafuta opportunity za biashara huko
 
Majahadhi kupitia Kisiju. Usafiri wa uhakika ni ndege ni mwendo wa dk 45 toka JNIA
 
Boti unapandia Nyamisati ni kuanzia saa 4 asubuhi, nauli ni Tsh 10,000 na masaa 6 upo Mafia. Kufika Nyamisati unapandia gari Mbagala (uwepo pale saa 12 asubuhi na nauli ni 5,000 hivi.

Ndege zipo ni Tsh 105,000 na 120,000 one way na ni dakika 35 tu Dar to Mafia!
Karibu Mafia
 
Ukikoswa usafiri! PIGA MBIZI, kama alivyosema yule waziri wa Jakaya mrisho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…