Maeneo yanayoongoza kwa utakatishaji fedha

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,426
Dar es Salaam. Baada ya juhudi kadhaa za kukabiliana na utakatishaji fedha, Serikali imebainisha sekta zinazoongoza kwa uhalifu huo sambamba na makosa yanayojirudia, ripoti inaonyesha.

Kwa mujibu wa ripoti ya utakatishaji fedha na ugaidi ya mwaka 2016 (National money laundering and terrorism financing risks assessment report 2016) iliyotolewa hivi karibuni na Idara ya Udhibiti Fedha Haramu (FIU) ya Wizara ya Fedha na Mipango, biashara ya magari, nyumba, maduka ya kubadilishia fedha na madini ndiyo maeneo yanayoongoza kwa utakatishaji fedha.

Ripoti hiyo inasema, watu wanaopata fedha chafu kutokana na uhalifu tofauti, huziwekeza kwenye maeneo hayo ili kuzitakatisha. Ukosefu wa vitambulisho hasa vya Taifa kwa wananchi wengi, ripoti inasema ni mwanya unaotumiwa vyema na wahalifu hao.

Licha ya maeneo hayo yanayowavutia watakatishaji fedha nchini, ripoti hiyo imebainisha makosa sita yaliyogundulika, kuchunguzwa na kuhukumiwa. Takwimu zilizokusanywa kutoka vyombo vya ulinzi na usalama zinabainisha makosa, thamani ya mali zilizokamatwa na kutaifishwa hata faini iliyolipwa na wahusika.

Ufisadi na rushwa, ukwepaji kodi, dawa za kulevya, uuzaji na umiliki wa noti bandia, uchimbaji na biashara haramu ya madini pamoja na ujangili na umiliki wa nyara za Serikali, ripoti inasema ndio makosa yanayohusiana na utakatishaji fedha.

“Maeneo hayo bado hayasimamiwi vya kutosha hivyo kutoa nafasi kwa watakatishaji fedha kufanya watakavyo bila kuingiliwa na vyombo vya usalama,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.

Biashara ya magari, ripoti inasema ni miongoni mwa sehemu zinazokimbiliwa na watakatishaji kutoka na watu wengi kupenda kumiliki magari ama kwa biashara au matumizi ya familia.

“Magari hasa ya kifahari hununuliwa na watakatishaji kufanikisha shughuli zao za kihalifu. Biashara hii ina mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi lakini matumizi ya fedha taslimu ni mwanya unaotumiwa na wahalifu hawa,” inasomeka sehemu ya ripoti hiyo.

Usimamizi mdogo uliopo kwenye biashara nyumba na viwanja, ripoti inasema unatoa mwanya kwa watakatishaji kujificha kwenye sekta hiyo. Matukio machache huripotiwa kwenye eneo hilo licha ya miamala mikubwa inayofanyika.

Taasisi za fedha yakiwamo maduka ya kubailishia fedha, benki za biashara, Saccos na Vicoba ni eneo jingine ambalo linaelezwa kutumika kufanikisha uhalifu huo. Bahati nasibu, casino na aina nyingine za bahati nasibu ni maeneo mengine ambako fedha haramu huelekezwa.

Uchimbaji na biashara haramu ya madini, ripoti inasema ni eneo linalopendwa na watakatishaji fedha kutokana na urahisi wa kuuza madini.

“Kwa Tanzania, ni rahisi kwa mtu yeyote kununua madini ya thamani kubwa hata kutoka mamlaka husika bila kushukiwa. Mara nyingi, biashara hii hufanyika kwa fedha taslimu,” inasema ripoti hiyo.

Kukabiliana na uhalifu huo, ripoti inapendekeza marekebisho ya Sheria ya Utakatishaji Fedha (Anti-Money Laundering Act) ya mwaka 2006 na Sheria ya Utakatishaji Fedha na Mwenendo wa Makosa Yake (Anti-Money Laundering and Proceeds of Crime Act) ya mwaka 2009 ili kuweka vifungu vitakavyoongeza adhabu kwa wahalifu.

- Mwananchi
 
Njoja waje wataalam tuone mambo talivyo
Kwenye kutakatisha pesa Kuna nchi ziko soft kidogo Kama mtu anatumia pesa ndani ya nchi kunyanyua uchumi wa nchi mfano ni Kenya .Kenya hugombana na kuchukua hatua Kali kwa watakatisha fedha wanaohamisha pesa kwenda nje ila kwa wawekezaji wanaowekeza ndani huwa Sio wakali Sana.Hili la utakatishaji fedha linahitaji nchi za kiafrika kuliangalia Mara mbili nitoe mfano.Pesa nyingi zinaondoka Afrika kwenda mabenki ya Ulaya ,kununua majumba ulaya nk mipesa kama ya viongozi wa kisiasa Akina Abacha nk Huwezi sikia wazungu hao wanakomalia utakatishaji pesa huo.Ila pesa zikitoka kwao kuja Africa wanataka kila pesa inayotoka kwao itolewe maelezo imetokana na Nini? Kifupi wanadhibiti pesa zao kuja Africa wakati wakiacha mlango wazi wa pesa za Afrika kwenda nje kwenye nchi zao bila maswali.Hii Vita ya kupambana na utakatishaji fedha Ni kubwa Afrika kuliko Ulaya na Marekani!!! Ni vizuri tuwe makini.Mfano kuna biashara zingine hufanyika kwa Mali kauli hasa zinazohusu biashara ya kuagiza bidhaa nje.Mtu analetewa mzigo bila kulipa hata Mia akiuza ndio analipa kwa aliyempa mzigo nk Nadhani twende taratibu tusije ua ukuaji wa uchumi wa ndani .Ni maoni yangu.
 
Duh mkuu hapo nimepata somo sana kumbe mambo ya utakatishaji ni mapana kuliko ninavyofikiri ila kuna hawa viongozi wetu wamekuwa wakibeba pesa zetu nyingi sana na kwenda kuzichimbia huko ulaya si wanatakatisha pesa nyingi sana ila kwa mtazamo wangu inshu ya utakkatishaji fedha zetu wakianza kukamata naona kama hawa viongozi wetu ndio watakuwa wa kwanza mana pesa zetu nyingi sana zimekuwa zikipelekwa nnje ya nchi pasipo maelezo yoyote isipokuwa kwa maslai yao binafsi
Kwenye kutakatisha pesa Kuna nchi ziko soft kidogo Kama mtu anatumia pesa ndani ya nchi kunyanyua uchumi wa nchi mfano ni Kenya .Kenya hugombana na kuchukua hatua Kali kwa watakatisha fedha wanaohamisha pesa kwenda nje ila kwa wawekezaji wanaowekeza ndani huwa Sio wakali Sana.Hili la utakatishaji fedha linahitaji nchi za kiafrika kuliangalia Mara mbili nitoe mfano.Pesa nyingi zinaondoka Afrika kwenda mabenki ya Ulaya ,kununua majumba ulaya nk mipesa kama ya viongozi wa kisiasa Akina Abacha nk Huwezi sikia wazungu hao wanakomalia utakatishaji pesa huo.Ila pesa zikitoka kwao kuja Africa wanataka kila pesa inayotoka kwao itolewe maelezo imetokana na Nini? Kifupi wanadhibiti pesa zao kuja Africa wakati wakiacha mlango wazi wa pesa za Afrika kwenda nje kwenye nchi zao bila maswali.Hii Vita ya kupambana na utakatishaji fedha Ni kubwa Afrika kuliko Ulaya na Marekani!!! Ni vizuri tuwe makini.Mfano kuna biashara zingine hufanyika kwa Mali kauli hasa zinazohusu biashara ya kuagiza bidhaa nje.Mtu analetewa mzigo bila kulipa hata Mia akiuza ndio analipa kwa aliyempa mzigo nk Nadhani twende taratibu tusije ua ukuaji wa uchumi wa ndani .Ni maoni yangu.
 
Ripot ya mwaka 2016 inakuja kutolewa 2019.
Hii inaonyesha namna gani mchakato wa ukusanyaji na uchakaji taarifa ulivyo mbovu.
Kama ripoti ingetoka 2017 basi ni dhahiri vyombo vya ulinzi na usalama vingefanikiwa kudhibiti njia zinazotumika
 
Kwenye kutakatisha pesa Kuna nchi ziko soft kidogo Kama mtu anatumia pesa ndani ya nchi kunyanyua uchumi wa nchi mfano ni Kenya .Kenya hugombana na kuchukua hatua Kali kwa watakatisha fedha wanaohamisha pesa kwenda nje ila kwa wawekezaji wanaowekeza ndani huwa Sio wakali Sana.Hili la utakatishaji fedha linahitaji nchi za kiafrika kuliangalia Mara mbili nitoe mfano.Pesa nyingi zinaondoka Afrika kwenda mabenki ya Ulaya ,kununua majumba ulaya nk mipesa kama ya viongozi wa kisiasa Akina Abacha nk Huwezi sikia wazungu hao wanakomalia utakatishaji pesa huo.Ila pesa zikitoka kwao kuja Africa wanataka kila pesa inayotoka kwao itolewe maelezo imetokana na Nini? Kifupi wanadhibiti pesa zao kuja Africa wakati wakiacha mlango wazi wa pesa za Afrika kwenda nje kwenye nchi zao bila maswali.Hii Vita ya kupambana na utakatishaji fedha Ni kubwa Afrika kuliko Ulaya na Marekani!!! Ni vizuri tuwe makini.Mfano kuna biashara zingine hufanyika kwa Mali kauli hasa zinazohusu biashara ya kuagiza bidhaa nje.Mtu analetewa mzigo bila kulipa hata Mia akiuza ndio analipa kwa aliyempa mzigo nk Nadhani twende taratibu tusije ua ukuaji wa uchumi wa ndani .Ni maoni yangu.

Mkuu umenena vyema sana... Kama kuna viongozi na wanapitia jukwaa hili hii point yako ni nzuri sana. Huu utakatishaji wa fedha uangaliwe kwa jicho la tatu. Kama mtu anatakatisha hela kwa kuongeza mzunguko wa hela nyingi au kufanya vitu vyenye tija kidogo mamlaka kama zikimkamata zimpige fine kiasi na kumkanya asirudie hili suala. Ila haya mambo yakuwabana sana mwishowe wengi wao wanaishia kukimbizia hizo hela nje na mzunguko unakuwa mgumu sana nchini. Kifupi serikali iwe wakali pindi mtu anapotaka kutoa hela nje ya nchi na sio wakali sana mtu akitaka kuingiza hela nchini(simaanishi kuwa kila hela inayoingia ichukuliwe poa maana nyingine zinaweza kuwa zimeingizwa kwa ajili labda ya kusupport ugaidi etc)
 
Wenzetu utakatishaji wa pesa wanaukubali sana katika nchi zao
Kama watakatishaji wanatoka nazo nje na kuja kuwekeza ni sawa
Wazungu wamekubali (watake wasitake) kuwa wachina na Russians na hata waarabu waingize pesa zao na kununua majengo na mashirika na hata kuingiza kwenye hisa.
Hawahoji mtu katoa wapi hela
Ila sisi utakasishaji wetu ni hela za ndani na mali ya ndani ndio zinaibiwa halafu kuzihalalisha nchini na hii ni mbaya sana kwa uchumi.

Mtu anaiba billions nchini halafu anaingiza hela zake kwenye kampuni haina afya kiuchumi kwani ni za ndani.
 
Kwenye kutakatisha pesa Kuna nchi ziko soft kidogo Kama mtu anatumia pesa ndani ya nchi kunyanyua uchumi wa nchi mfano ni Kenya .Kenya hugombana na kuchukua hatua Kali kwa watakatisha fedha wanaohamisha pesa kwenda nje ila kwa wawekezaji wanaowekeza ndani huwa Sio wakali Sana.Hili la utakatishaji fedha linahitaji nchi za kiafrika kuliangalia Mara mbili nitoe mfano.Pesa nyingi zinaondoka Afrika kwenda mabenki ya Ulaya ,kununua majumba ulaya nk mipesa kama ya viongozi wa kisiasa Akina Abacha nk Huwezi sikia wazungu hao wanakomalia utakatishaji pesa huo.Ila pesa zikitoka kwao kuja Africa wanataka kila pesa inayotoka kwao itolewe maelezo imetokana na Nini? Kifupi wanadhibiti pesa zao kuja Africa wakati wakiacha mlango wazi wa pesa za Afrika kwenda nje kwenye nchi zao bila maswali.Hii Vita ya kupambana na utakatishaji fedha Ni kubwa Afrika kuliko Ulaya na Marekani!!! Ni vizuri tuwe makini.Mfano kuna biashara zingine hufanyika kwa Mali kauli hasa zinazohusu biashara ya kuagiza bidhaa nje.Mtu analetewa mzigo bila kulipa hata Mia akiuza ndio analipa kwa aliyempa mzigo nk Nadhani twende taratibu tusije ua ukuaji wa uchumi wa ndani .Ni maoni yangu.

Kenya wamebadili hela recently. Wamekataa hela nyingi tu za zamani sababu hizo hizo za utakatishaji
 
Back
Top Bottom