Maeneo yanayonyesha mvua kwa sasa

Maeneo yanayonyesha mvua kwa sasa

  • Thread starter Thread starter guest-1793102819
  • Start date Start date
Ukiwa mjinga na mpumbavu lazima uwakubali mashehe. Hivi msimu wa mvua mtu anaomba mvua inyeshe na kuna wapumbavu wanaamini kaleta mvua. Kweli wajinga ndio waliwao. Waombe na msimu wa kiangazi inyeshe mvua.
Haaa mfuasi was gwajima kwenye ubora wake.
 
Huku Dodoma kwenye viunga vya bunge mvua imekata tokea mbunge Fulani achukue likizo ya kuugua ya muda mrefu, ilikuwa inanyesha mpaka tunapiga deki maiki. Elnino asikwambie ntu
 
Hapa nyumbani kwangu Kimara bado inaendelea kunyesha, ila ni mvua ya maneno kutoka kwa mke wangu eti mbona kutwa nzima nilikua sipatikani


Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aiseeee[emoji119]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niko kwenye mwendokasi. Kuna mzee mmoja naona kada wa chama cha CUF. anamsifu profesa utadhani profesa malaika. Kibaya zaidi amesimama na akiongea anatema mvua ya mate kila mtu ametoa hanjifu lkn hili zuzu linazidi tu kusifu na kuabudu
 
( napokea taarifa hapa kuwa; maeneo ya lupaso, buserere, kishimundu, kazula mimba, nkasi na baadhi ya maeneo ya nanjilinji kuna dalili ya mvua. Pia kule Namanyere na ikungi huenda ikanyesha muda wowote wiki hii. Maeneo ya Ingrijuu, Taveta mpaka juba huko jua litaendelea kuwaka. Bila kusahau maeneo ya ukanda wote wa pwani ya kaskazini kuanzia visiwa vya watumbatu, nchi ya wadigo, wabondei wanguu na wasagala huko itanyesha siku kadhaa zijazo. Huko Mwembe Ladu, Mchamba wima, Mnazi Mmoja mpaka visiwa vya Anjuani mvua itanyesha muda si mrefu kutoka sasa. Mikindani, Nanganga, Namajani, Nankonjela, Naunambe, Namichiga, Nangurukuru hadi Namungo huko tayari imeshanyesha hivyo wenyeji wanaweza kuanza kupanda kunde kwa sasa. Tutaendelea kutoa updates kadri zinavyopatikana).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom