Maeneo matatu ya mwili yanayohusika na utimilifu wa ndoto yako directly.

Mzee wa kusawazisha

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,587
1,136
1. MOYO (Your Heart).

Hapa ndo mahali ndoto zinazaliwa, Passion za kitu fulani huwa zinaanzia kwenye Moyo......Ukisikia mtu anasema "Nina Passion ya Kufanya jambo fulani" basi ujue hilo jambo limetoka moyoni......Hapa ndipo hazina kubwa ya Ndoto yako ilipo,.....Hapa ndipo mahali palipobeba hatima ya ndoto yako kwa asilimia kubwa..... Hapa ndo mahali panapohusika na mtu kukata tamaa au kuendelea mbele...... Hapa ndo mahali panapohusika na kuanza kuiishi ndoto au kushindwa......Kuchukua au kutochukua hatua ya kwanza inategemeana na Kiwango cha Passion kilichozalishwa na Moyo.

BURNING DESIRE huwa inazalishwa kwenye MOYO kisha hiyo Burning Desire Inatengeneza STRONG WILL POWER (NIA KUBWA), Ambayo ndiyo chachu ya kuleta msukumo wa Kuchukua hatua ya kwanza kuelekea ndoto yako!!

Sasa, Ukiona Mtu anaongea tu Maneno na hachukui hatua yoyote kuanza kuiishi na kuziweka kwenye matendo ndoto yake basi jua bado MOYONI mwake hamjawaja na PASSION ya kutosha na BURNING DESIRE haijazalishwa bado......Ukishafika hatua ya kuwa na PASSION ya kutosha na BURNING DESIRE basi YOU CAN'T WAIT ANY MORE!!

PASSION, FEELINGS, DESIRES, WILL POWER (NIA YA DHATI) vyote hivi hutoka ndani ya MOYO, Sasa kama vyote vikiambatanishwa kuhusu Ndoto yako na ukaamua kuchukua hatua basi jua kuwa utakuwa UNSTABLE kwenye Ndoto Yako!!

Biblia Inasema "Linda Sana Moyo wako kuliko chochote kwani huko ndiko zitokazo Chemichemi za uzima"...... Kwenye MOYO ndipo pamebeba Hatima ya ndoto yako..... Ndipo Ndoto Inazaliwa......Ndipo Uvumilivu huzaliwa pale ndoto yako inapopita kwenye Changamoto.......Ndipo mahali ambapo ile sauti ya upole inayosema "SONGA MBELE UTASHINDA" Inapotoka......Ndipo mahali ambapo Ukijihisi kama kukata tamaa na kuona kama huwezi kutimiza ndoto yako unatakiwa kurudi na kusikiliza Moyo Unakwambia nini?? Je nao Moyo Unakwambia acha au Endelea mbele.....Hapa ndipo Penye Sauti ya kweli kuhusu NDOTO Zetu!!

MOYO unabeba picha halisi ya kile tunachotamani kukiona.....Ile kauli ya "I CAN" Ikitoka ndani ya MOYO basi jua kweli hicho kitu kinawezekana!!.....Unapopita kipindi cha magumu, maumivu makali, Kukatiswa tamaa, Kuona kama ndoto yako haiwezekani nenda ndani ya MOYO wako kisha utapata majibu sahihi!!

Ule msemo wa "FOLLOW YOUR HEART" ni Msemo sahihi 100%....Kwani MOYO huwa hauzikubali LIMITATIONS isipokuwa wewe mwenyewe umeamua kuuaminisha!!.....Kwenye MOYO ndipo ile Confidence ya kuchukua hatua ya kwanza na Kuendelea mbele inapokuwepo!!

2. UBONGO (AKILI).

Sasa hapa ndo sehemu ambapo Uhalisia wa mambo huwa unapimwa.....Na kupima huko mara nyingi kumesababisha watu wengi washindwe kuziishi ndoto ambazo Mungu ameweka ndani yako kwa kupima uhalisia wa ndoto ya Mungu ndani yao na Uhalisia wa dunia......Sisemi kwamba usitumie akili, ila ninachojaribu kukujuza hapa ni kuwa "Akili hutafuta sana uhalisia wa Kidunia na kukufanya uachane na uhalisia wa Mungu juu ya ndoto yako"..... Embu muangalie Daudi, Mungu aliweka ndoto na Passion ya Kumuua Goliath ndani ya Moyo wake, Lakini kama angeamua kifuata uhalisia wa dunia ilivyokuwa inamwambia kuwa huwezi kumuua Goliath basi kweli asingeweza na angeahirisha kabisa kwenda kwenye uwanja wa mapambano.....au kama angeamua kufuata uhalisia wa akili zake kama binadamu angesema " Yaani mfalme ameshindwa na majemedali wakubwa wa jeshi wameshindwa, mimi ntaweza kweli?? Basi angeacha kukifanya kile ambacho Mungu alimsemesha".

Ukiangalia watu wengi waliamua kuzisikiliza sauti za ndani yao za kutoka kwenye Moyo na kuamua kupuuzia akili zao ndiyo waliofanikiwa kuvunja rekodi za dunia.

Sometimes ni kweli kwa akili za kibinafamu haiwezekani lakini Je, ndani yako unasikia nini??.......Donald Trump wakati anaanza mbio za kuusaka Urais watu walimwambia ni vizuri kuwa miongoni mwa washiriki ili kuweka historia yaani walijua kabisa kuwa huwezi Kushinda hata iweje......Kitendo cha Thomas Edson kujaribu zaidi ya mara 1000 kutengeneza electric bulb bila mafanikio maana yake ni kuwa akili za kibinadamu zilikataa lakini yeye alisema Inawezekana kutoka Moyoni mwake.....Bill Gates aliambiwa na IBM idea yake haiwezi kufanikiwa, akaamua kuachana na IBM na kuamua kukipambania kitu ambacho sayansi ya dunia ilikuwa inaona hakiwezekani, na mwisho wa siku kikawezekana!!

Kitendo cha Ubongo (Akili) kupima uhalisia ni kizuri lakini jaribu pia kusikiliza Moyo unasema nini?? Kwani sometimes uhalisia wa dunia ndio unaweza kuwa kizuizi cha kutimiza ndoto yako.

Ni kweli watu wakikutazama kiuhalisia wanaona kuwa hufananii na ndoto yako.....Ni kweli akili za kibinadamu zinaona kama huwezi fanikiwa.....Ni kweli unaonekana huna uwezo wa kufika popote.....HIZO NI AKILI NA UHALISIA WA DUNIA.....JE, NI UHALISIA WA KITU KILICHOPO MOYONI MWAKO.....JE NI UHALISIA WA NDOTO MUNGU ALIYOWEKA NDANI YAKO!!

Hakikisha Ubongo wako unapata chakula chake pia ili uwe kwenye hali nzuri ya kufanya maamuzi sahihi.....Chakula kikuu cha ubongo ni Maarifa, Soma vitabu, jifunze vitu chanya, semina ili tu uwe kwenye hali nzuri ya kufikiria!!

Kumbuka msemo unaosema "Whatever your Mind can conceive it can achieve it"....NOTHING IS IMPOSSIBLE!!

Myles Munroe aliwahi kusema "In order to be successful on your Dream you must BREAK THE RULES"..... Je, umeshawahi kuwaza unavowasiliana na mtu aliyepo Dar kwa simu kuwa ni kitu akili inaweza kukikubali kirahisi....au kumuona mtu anachokifanya Marekani kwa TV au Internet,.....Walioyagundua haya mambo yote MIOYO yao ilikubali baada ya Mungu kuweka hizo ndoto ndani yao lakini AKILI za watu Wengine ziliona kama haiwezekani na inawezekana hata akili zao ziliwashawishi kuwa haiwezekani lakini walipoamua Kufuata nia ya MOYO, Hatimaye WAKAFANIKIWA!!

3. MWILI

Mwili ni kama bendera fuata upepo.....Wenyewe husikiliza Maamuzi yenye nguvu kati ya maamuzi ya Moyo na Maamuzi ya Ubongo (Akili).....Kitakachoonekana kuwa na nguvu ndicho ambacho mwili huamua kukitii.

Kitu cha msingi cha kukifanya ili mwili wako uendelee kuwa na uwezo wa kutii maamuzi either ya Moyo au Akili ni lazima uwe na AFYA NJEMA.....Mwili ndo unaotumika kufanya Utendaji kuhusu Ndoto yako, Hivyo ni lazima uhakikishe kuwa Mwili uko kwenye hali nzuri kiafya.

Yaani hata kama ikitokea MOYO na UBONGO (AKILI) Vimekubaliana na Maamuzi ya aina moja, Lakini kama mwili ni dhaifu basi jua kuwa itakuwa kazi ngumu sana kwenye Utendaji!!

"Ni Upumbavu mkubwa sana kuwa na ndoto kubwa halafu hujali afya ya mwili yako".....Unakuta mtu ana ndoto halafu kicheche, anakula hovyo hovyo, hafanyi mazoezi n.k.....Hakikisha mwili wako unakuwa katika hali nzuri kiafya kwa kuepuka magonjwa ya zinaa, kwa kuufanyisha mazoezi na kuutunza kwa vyakula vizuri ili uwe na uwezo wa kuyaweka kwenye vitendo maamuzi yanayohusu ndoto yako.

Moyo ukitengeneza PASSION, WILL POWER, BURNING DESIRE NA COMMITTMENT na Vitu hivi Vikakubaliwa na UBONGO (AKILI YAKO).....na UBONGO Ukatoa Amri kwa Mwili kuwa Uwe Tayari kwa Mapambano, Basi jua kuwa utakuwa UNSTOPABLE na NDOTO YAKO LAZIMA ITATIMIA!!
 
Back
Top Bottom