KunjyGroup
JF-Expert Member
- Dec 7, 2009
- 352
- 26
mkuu naomba ufafanuzi kwenye mafuta,ina maana ndio bei ya mafuta?
thanx for good news. hope the same to happen in TZ
Ndugu zangu mimi ni huku Zambia.
- Mafuta yashushwa kwa K492 kwa litre
- Mshahara kima cha chini K2,000,000 kwa wafanyakazi wa migodini, makampuni yote ya wawekezaji (hado Shoprite).
- Ballot papers zitakuwa zinachapishwa Zambia kuanzia mwakani. Rais alisema, ‘Kwanini miaka 47 ya uhuru tunaendelea kuchapicha nje ya nchi? Kama ni gharama, tutaingia tu…'
- Mawaziri wapunguzwa kutoka 23 hadi 19.
- Amedai pia kwamba haoni umuhimu wakuwa na wakuu wa wilaya.
Sata ni kiongozi wa nchi na dhamana kubwa sana, lakini hatoweza kuiendesha nchi na kuleta maendeleo ikiwa Wazambia walio wengi (kama sio wote) hawatampa ushirikiano. Tuombe Mungu juhudi zake zifunue vichwa vya Wazambia na kuiona Zambia ni nchi ya Wazambia na wala sio ya chama tawala au kundi fulani la watu wachache, kama alivyotuhakikishi Bwanamdogo Nape juzi kuwa Wamiliki wa Tanzania si Watanzania bali CCM:Bravo Sata, ila zisiwe mbio za sakafuni au nguvu ya soda.
Ukiona mwenzako ananyolewa nywele....................Hivi Zambia ni sehemu ya Tanzania?
Pia rais Sata akiongea katika maombi yaliyofanywa na madhehebu yote jana, alipingana na wakuu wa dini kwamba Zambia kuna amani. Hoja yake ya kwamba hakuna amani ya kweli ni kwamba huwezi ukasema kuna amani wakati kuna watu ambao hawawezi kupata milo mitatu kwa siku.
Pia rais Sata aliukatalia ujumbe wa Bingwa Mutharika wa malawi kumwalika katika mkutano wa COMESA utakaofanyika Blantire, kwa maelezo kwamba hawezi kwenda nchini kwake mpaka hapo Serikali ya Mutharika itakapompa sababu za kumkamata sata na kumdepot wakati alipomtembelea Bakili muluzi. Aliuambia ujumbe huo kwamba hoja ya kuwa alitendewa hayo kwa kuwa alikuwa mpinzani, Sata amekataa kwa kusema katika nchi za commonwealth, hazina kanuni ya kuwa mpinzani ni jinai.
.