Maendeleo Zambia yaanza kuonekana

KunjyGroup

JF-Expert Member
Dec 7, 2009
352
26
Ndugu zangu mimi ni huku Zambia.
  1. Mafuta yashushwa kwa K492 kwa litre
  2. Mshahara kima cha chini K2,000,000 kwa wafanyakazi wa migodini, makampuni yote ya wawekezaji (hado Shoprite).
  3. Ballot papers zitakuwa zinachapishwa Zambia kuanzia mwakani. Rais alisema, ‘Kwanini miaka 47 ya uhuru tunaendelea kuchapicha nje ya nchi? Kama ni gharama, tutaingia tu…’
  4. Mawaziri wapunguzwa kutoka 23 hadi 19.
  5. Amedai pia kwamba haoni umuhimu wakuwa na wakuu wa wilaya.
 
inatia moyo some of us black africans are starting to take serious steps towards serious developments of our people. bravo Zambians.
 
Pia rais Sata akiongea katika maombi yaliyofanywa na madhehebu yote jana, alipingana na wakuu wa dini kwamba Zambia kuna amani. Hoja yake ya kwamba hakuna amani ya kweli ni kwamba huwezi ukasema kuna amani wakati kuna watu ambao hawawezi kupata milo mitatu kwa siku.
Pia rais Sata aliukatalia ujumbe wa Bingwa Mutharika wa malawi kumwalika katika mkutano wa COMESA utakaofanyika Blantire, kwa maelezo kwamba hawezi kwenda nchini kwake mpaka hapo Serikali ya Mutharika itakapompa sababu za kumkamata sata na kumdepot wakati alipomtembelea Bakili muluzi. Aliuambia ujumbe huo kwamba hoja ya kuwa alitendewa hayo kwa kuwa alikuwa mpinzani, Sata amekataa kwa kusema katika nchi za commonwealth, hazina kanuni ya kuwa mpinzani ni jinai.
.
 
Ndugu zangu mimi ni huku Zambia.
  1. Mafuta yashushwa kwa K492 kwa litre
  2. Mshahara kima cha chini K2,000,000 kwa wafanyakazi wa migodini, makampuni yote ya wawekezaji (hado Shoprite).
  3. Ballot papers zitakuwa zinachapishwa Zambia kuanzia mwakani. Rais alisema, ‘Kwanini miaka 47 ya uhuru tunaendelea kuchapicha nje ya nchi? Kama ni gharama, tutaingia tu…'
  4. Mawaziri wapunguzwa kutoka 23 hadi 19.
  5. Amedai pia kwamba haoni umuhimu wakuwa na wakuu wa wilaya.

Mkuu Kwacha moja ni sawa na US dollar ngapi au sawa Tsh ngapi,Hivi niandikapo bei ya mafuta imepanda tena hapa Dar diesel litre moja ni Tsh 2010
 
King Cobra ni Cobra wa Ukweli,nawaonea wivu Wazambia ,sisi badala ya kupiga hatua mbele kumi ,tunarudi nyuma hatua kumi
 
Bravo Sata, ila zisiwe mbio za sakafuni au nguvu ya soda.
Sata ni kiongozi wa nchi na dhamana kubwa sana, lakini hatoweza kuiendesha nchi na kuleta maendeleo ikiwa Wazambia walio wengi (kama sio wote) hawatampa ushirikiano. Tuombe Mungu juhudi zake zifunue vichwa vya Wazambia na kuiona Zambia ni nchi ya Wazambia na wala sio ya chama tawala au kundi fulani la watu wachache, kama alivyotuhakikishi Bwanamdogo Nape juzi kuwa Wamiliki wa Tanzania si Watanzania bali CCM:
 
Pia rais Sata akiongea katika maombi yaliyofanywa na madhehebu yote jana, alipingana na wakuu wa dini kwamba Zambia kuna amani. Hoja yake ya kwamba hakuna amani ya kweli ni kwamba huwezi ukasema kuna amani wakati kuna watu ambao hawawezi kupata milo mitatu kwa siku.
Pia rais Sata aliukatalia ujumbe wa Bingwa Mutharika wa malawi kumwalika katika mkutano wa COMESA utakaofanyika Blantire, kwa maelezo kwamba hawezi kwenda nchini kwake mpaka hapo Serikali ya Mutharika itakapompa sababu za kumkamata sata na kumdepot wakati alipomtembelea Bakili muluzi. Aliuambia ujumbe huo kwamba hoja ya kuwa alitendewa hayo kwa kuwa alikuwa mpinzani, Sata amekataa kwa kusema katika nchi za commonwealth, hazina kanuni ya kuwa mpinzani ni jinai.
.

mkuu ni sawa kabisa kwamba huwezi kusema nchi ina amani wakati watu wanakula mlo mmoja......hospitalini wanalala chini....madawa hakuna....shuleni wanakalia mawe, wengine chini....wakati polisi wanabambikia watu kesi....wakati watu wakiandamana kwa amani wanapigwa risasi ni upuuzi kusema nchi ina amani.....
 
On Friday, energy Minister Chris Yaluma announced that goverment has reduced the price of Petrol by 5.7% to K8,155 per litre, diesel by 4.9% to K7,566 and Kerosine 8.6% to K5,641.
Yaluma said, 'I also wish to inform the public that the streamline of the fuel rpices is ongoing and where necessaryn further changes will affected in future.
 
Peri. Utendaji wa Sata unajukana. aliwahikuwa Waziri wa Afya, mda huo nilikuwa nasoma Zambia na hakukuwa na uzembe katika utendaji wa Drs & nurses. Alibadili system. Aliwahi kuwa waziri wa Local government & mayor wa Lusaka. Historia inaonyesha utendaji kazi wake.
Juzi tu alimwambia face blank Ambassador wa China kwamba 'I don't want us to come and point fingers at each other.' aliongelea conditions of service za employees and akasema hataki kuona wanaleta watuwao kufanya kazi amabazo wa Zambia wanaweza kuzifanya kama ukarani na udereva. "njooni nyinyi wawekezaji, wafanyakazi wapo wa Zambia...'
 
Tazara atafika. Kuna strike. Just yesterday we were talking the same issue ndani ya train. anajua sana.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom