Maendeleo yataletwa na CCM - Nape

Maendeleo yataletwa na CCM - Nape

Huyu mtu anaishi Tanzania? Yupo dunia gani huyu mtu? Anaishi kwenye ndoto ya kiza kama wafu. Eti ccm itawaletea maendeleo kwa hiyo hayajafika? Yapo wapi? Miaka 50 yapo njiani? So tueleze lini yatafika? Hivi huyu maswi ni mpinzani? Kuwaita wabunge tumbili na washenzi na wajinga nani anatukana? Wewe nape kuwa realistic wenye akili tupo wengi.
 
Kama Ccm imeshindwa kuyaleta hayo maendeleo kwa zaidi ya 50yrs sasa, hata mkiachiwa kwamiaka 1000 bado hamta weza leta maendeleo kwaWatanzania. You better go Ccm.
 
Hii ni kauli matata sana toka kwa Nape...

itoshe kusema kuwa Nape amefanya pre-visit huko siku za usoni, akaona namna nchi ilivoendelea papo hapo akaona yaani bila CCM maendeleo hayo yasingefikiwa.

Nape, maendeleo hayo yatafikiwa kwa utelezaji wa ilani ipi ya CCM? maana kweli mipango mingi imo kwenye ilani ya 2010-2015, utekelezaji uko wapi?
 
Nape hana jipya zaidi ya kujikumbata/kujificha kwenye makwapa ya Mzee wa Tembo (Bw. Kinana) kama kipochi cha mwanamke. Nape kama Nape hawezi kuwa na hoja ya msingi zaidi ya kupayuka na kuvimbisha mishipa ya shingo pekee. Ni vikundi kama CCM NA Serikali yake pekee vinavyoweza kuongozwa na watu kama Nape.
 
Kama.wapinzani awajaleta maendeleo futeni mfumo wa vyama vyingi tubaki na chama kimoja alafu tuone nani ataongelea wizi
 
Back
Top Bottom