Maendeleo yataletwa na CCM - Nape

Maendeleo yataletwa na CCM - Nape

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Nape-Nauye--November17-2014.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Nape Nnauye.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (pichani), amesema maendeleo kamwe hayawezi kupatikana kwa njia ya matusi na kufarakanisha wananchi kama wanavyofanya viongozi wa upinzani.

Pia amewataka wananchi kuhakikisha wanachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa akisema ndicho chama chenye viongozi imara watakaowaletea maendeleo.

Nape aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Chumo wilayani Kilwa na kwamba kazi ya CCM ni kuhakikisha inashirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo tofauti na wapinzani ambao kazi yao ni matusi na kufarakanisha wananchi.

Alisema wananchi wasichague vyama vya upinzani kwa sababu havina lengo la kuwaletea maendeleo, badala yake wachague CCM kwa kuwa ndicho chama kinachoweza kuwaletea maendeleo na kutatua kero zinazowakabili.

“Hakuna maendeleo yanayoweza kuja kwa njia ya matusi , ahadi hewa wala kukejeli kazi zinazofanywa za kuwaletea wananchi maendeleo, kazi ya kutukana na kukejeli ni ya wapinzani na CCM kazi yake ni kuboresha maendeleo ya wananchi,” alisema.

CHANZO: NIPASHE
 
aisee, miaka mingine 50 ijayo!? ...kwani umasikini umeletwa na nani!
 
Sometimes naona kama CCM wanasema kweli, hivi vyama vya upinzani michosho sana
 
"Italetwa na ccm" lini?
Miaka 50 haikutosha kuleta hayo maendeleo?....nani anayetoa ahadi hewa kama sio ccm wakiokaa nadarakani kwa nusu karne.
 
Kwa hali ilivyo hapa Tanzania, naamini tutasubiri kwa miaka mingine 50 na kauli zitakuwa bado ni hizi hizi za sasa hivi kwamba maendeleo yataletwa na CCM! Huwezi kupata maendeleo kamwe kukiwa na hali kama hii ya watu kufuja mali ya uma bila kuchukuliwa hatua yoyote! Rasimu ya jaji Warioba ililiona hili lakini kwa makusudi kabisa wameliondoa halafu hao hao wanasema watatuletea maendeleo. Hayo maendeleo yanakujaje kama fedha zinazotakiwa kwa ajili hiyo zinafujwa kama hazina mwenyewe?
 
Ha ha ha ha CCM ni vituko kwa kwenda mbele.Walikuja na ahadi ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania waliposhindwa kuleta maisha bora kwa kila mtanzania wakawageuka watanzania na kuwafanya ni watu wa vijiweni hawawezi wakapata maendeleo.Leo wamekuja na kali kama ileile ya maendeleo yataletwa na CCM. Bila kuchanganya akili zako na zakuambiwa utaingizwa mjini mzima mzima.
 
watawaletea maendeleo lini? atupe muda kuanzia lini sio nayeye anabaki kwenye ahadi tu!
 
Hicho chama anachosema kimeleta maendeleo fedha wametoa wapi?
 
Wapinzani tujikite ktk mind liberation ya wadanganyika, hiyo ndio sumu itakayoimaliza maccm ukoo wa panya, mbele ya vichwa vyenye fikra upuuzi huo ungeibua maswali magum mpaka angejuta kuyatamka
 
Lini hayo maendeleo? Tupe time framework. Kisha useme kwa nini hakuna maendeleo so far mpaka aombe muda zaidi? Kipi kimekwamisha? Je kimepatiwa jibu?
 
maedeleo gani yatakayo letwa lini? Aache uongo
 
Wapinzani tujikite ktk mind liberation ya wadanganyika, hiyo ndio sumu itakayoimaliza maccm ukoo wa panya, mbele ya vichwa vyenye fikra upuuzi huo ungeibua maswali magum mpaka angejuta kuyatamka
 
Nape-Nauye--November17-2014.jpg

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Nape Nnauye.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (pichani), amesema maendeleo kamwe hayawezi kupatikana kwa njia ya matusi na kufarakanisha wananchi kama wanavyofanya viongozi wa upinzani.

Pia amewataka wananchi kuhakikisha wanachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa akisema ndicho chama chenye viongozi imara watakaowaletea maendeleo.

Nape aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Chumo wilayani Kilwa na kwamba kazi ya CCM ni kuhakikisha inashirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo tofauti na wapinzani ambao kazi yao ni matusi na kufarakanisha wananchi.

Alisema wananchi wasichague vyama vya upinzani kwa sababu havina lengo la kuwaletea maendeleo, badala yake wachague CCM kwa kuwa ndicho chama kinachoweza kuwaletea maendeleo na kutatua kero zinazowakabili.

“Hakuna maendeleo yanayoweza kuja kwa njia ya matusi , ahadi hewa wala kukejeli kazi zinazofanywa za kuwaletea wananchi maendeleo, kazi ya kutukana na kukejeli ni ya wapinzani na CCM kazi yake ni kuboresha maendeleo ya wananchi,” alisema.

CHANZO: NIPASHE

Warudishe pesa za wizi kwanza ndio waonge, inamaana umaskini ulioko tanzania umeletwa na upinzani? Nape nauye ana ugojwa wa kupoteza kumbukumbu
 
Inategemea anaongelea maendeleo yepi.... Kama wizi wa mali za uma na ufisadi ndio maendeleo basi hapo nakubaliana nae 100%.
 
Sometimes naona kama CCM wanasema kweli, hivi vyama vya upinzani michosho sana

Yeah sometimes, but most of the time they are lying. Kumbe ukweli unaujua ila buku 7 ni nyingi sana kuiacha.
 
Hakuna maendeleo yanayoweza kuletwa na CCM.Labda kama ana manisha kuwa baada ya CCM kumaliza kazi ya kuwaletea maendeleo watoto wao akiwemo Nape mwenyewe sasa inahamia kuwaleletea maendeleo wajukuu wao hapo kwa CCM inawezekana.
 
Back
Top Bottom