MAENDELEO YA NCHI BILA UHURU WA WATU NI UBATILI.

MAENDELEO YA NCHI BILA UHURU WA WATU NI UBATILI.

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
5,186
Reaction score
5,455
Umuofia kwenuuuuuu!!!!!!!.
Kuna mwanafalsafa mmoja alisema hatuwezi kuishi bila siasa maana maisha ni siasa. Mwingine akasema bila wanasiasa matatizo yasingekuwepo maana wao ndiyo huibua matatizo.

Nchi hii imekuwa na pambio nyingi za kudai kuendeleza demokrasia lakini ukweli hata theluthi ya demokrasia hakuna.

Tumeshuhudia aina ya chaguzi na usimamizi wake ulivyo wa ovyo kiasi kwamba ni aibu hata kwa mwenyekiti wa tume kujiita mwenyekiti.
Hivi unawezaje kuendelea kujiita baba wa nyumba kama majukumu ya ubaba yakikushinda?.

Idadi ya watu waliopoteza maisha yao kwa sababu ya uzembe wa makusudi wa tume yetu ya uchaguzi ni kubwa sana.

Idadi ya watu waliobakia walemavu wa kudumu sababu ya uzembe wa tume yetu na serikali yetu bado ni mkubwa sana. Watu waliofungwa gerezani pasipo na kesi za maana ni wengi mno.

Hashimu Rungwe mwenyekiti wa CHAUMMA alikamatwa na kuwekwa ndani na baadaye alikuja kuachiliwa bila hata kuambiwa kosa lake huku akiwa amesota sana. Ni serikali hii hii ya chama cha mapinduzi.

Wizi mkubwa umefanyika kwa kigezo cha uwekezaji na wengi waliohoji waliishia kupata mateso na kufirisiwa lakini baadaye ukweli ulijulikana.

Hakuna maendeleo yaliyowahi kudumu mahali popote duniani eti kwa kuyafanya baada ya kubinya haki za watu kujieleza na kusikilizwa.

Ninashindwa kuamini kama haya yanayofanyika leo nchini Tanzania ktk kubinya haki zetu raia ktk kuchagua viongozi tuwatakao yanajulikana kwa mh. Rais na makamu wake pamoja na waziri mkuu.
Enyi viongozi mbona wote nyie ni wakristo kwa waislamu hivi ni misikiti ipi mnakopata mafundisho ya kutenda hayo hadi mwawatesa watumishi wa MUNGU eti wachochezi?.

Ni makanisa yepi mnasali na kuuungama kwa haya mbayoyafanya kwa wanadamu wenzenu. Tumeshuhudia askari wakimsulubu mwandishi wa habari karibia kuua,tumeshuhudia viongozi mbunge Lema akitemewa mate usoni makohozi na raia wa ccm huku askari akishangaa na silaha anayo mkononi.

Imeandikwa siku za mwisho amani ya ndugu na ndugu itatoweka. Hivi unamchukiaje nduguyo kisa si mwanachama mwenzako.

Hakuna maendeleo yanayodumu yakiwa yamefanywa kiharamu na watu wanaotiririka damu za watu wasio na hatia mikononi mwao.

Hayati Mandela aliwahi kataa kumpa mkono Rais Bush akidai kuwa mikono ya Bush inachuruzika damu za watu wasio na hatia. Unapata faida gani kumwaga damu na kumjeruhi mwingine kisa madaraka.

Rais Donald Trump alisema wenye akili hawataki kujiingiza ktk siasa sasa wenye akili ndogo ndiyo wamevamia hivyo kuwatawala wenye akili na wajinga pia.

Imeandikwa ktk vitabu vitukufu kuwa tutafute kuwa na amani na watu wote huo utakatifu ambao hapana mtu atamuona MUNGU asipokuwa nao. Jiulizeni wenyewe enyi viongozi wa nchi hii mna amani na watu mnaowaongoza?.

Hadi sasa sijawahi amini kuwa walioshiriki kumpiga risasi Tundu Lissu ni viongozi wa nchi hii.
Hadi sasa siamini kama Akwilina aliuawa na askari wa nchi hii kwa mikono yao,si kweli.
Siamini kama Mbunge Sugu alifungwa gerezani kwa maagizo kutoka juu ili asiwatumikie wananchi.

Katu siamini kama walioenda kungoa na kuharibu shamba la Mbowe ni viongozi wateuliwa wa rais.

Siamini kama serikali hii inatumia kodi za wananchi kuwanunua akina Kafulila,wabunge na madiwani na viongozi wa vyama akina Mtatiro Julius.
Biblia imesema masikini ni mtu asiye huru. Umasikini ni utumwa. Mungu aliwaambia waisrael kuwa watakaa utumwani miaka 400 nao watatoka huko wakiwa matajiri. Wapinzani na watanzania wengi ni masikini wa mali na akili na ndiyo maana umasikini wao unawaponza.

Mwandishi wa habari alimuuliza Mtatiro aeleze kanunuliwa shilingi ngapi hata hivyo jibu alilotoa halitofautiani na jibu alilojibu Adamu mbele ya MUNGU. Aliulizwa uko wapi..............yeye akajibu niko uchi....aibu mtatiro jamani.A very simple geographical question. Ukivurugwa na matatizo huwezi kujibu kilicho sahihi.

Kuna wakati watanzania watamkumbuka Mange Kimambi aliyepata umaarufu kwasababu ya viongozi wazembe tulionao.

TANZANIA haijafikia hata theruthi hata sudusi ya maendeleo aliyoyafanya Gaddafi Libya lakini leo Libya ni nchi masikini iliyoanza kutafuta mafanikio upya kwa kuwa tu maendeleo waliyoyapata yalikosa enforcement ya kudemokrasia. Mwalimu wangu wa sheria ktk biashara akinifundisha sheria za mikataba alisema any contract not enforceable by low is not a contract. Nami leo nasema MAENDELEO yoyote yasiyokuwa na uhuru wa watu kuyahitaji kwa amani na hiyari yao siyo maendeleo.

Kama serikali hii haitaregeza shingo yake na kuirudia kweli basi haiwezi kudumu kabisa ukizingatia viongozi wake ni wanadini lakini wakiwa mafarisayo halisi ambao U-uungu haumo ndani yao bali uhitaji pekee ndiyo unaowaongoza kipi cha kufanya na wapi kwa kuelekea.

Ktk jamii iliyokosa demokrasia ujinga husifiwa kuliko maadili na sifa kwa wafalme huwa ndiyo msingi mkuu. Kutokana na UHURU uliopotea hata uzi maneno haya yaweza yakasomwa na wachache mno.
Nawatakia tafakuri njema kwa wote mtakaofanikiwa kusoma ujumbe huu na kuufanyia kazi kwa kuendeleza misingi ya umoja miongoni mwetu bila kujali tofauti zetu za kiimani na mitazamo.
 
Back
Top Bottom