Maendeleo na muda

smartdunia

Member
Jul 29, 2021
12
9
Na Smartdunia

Ni dhahiri tangu tulivyofahamu maana ya neno muda, basi tumeshalitaja neno hili mara nyingi kiasi kisichohesabika.

Lakini pia ni jambo la kushangaza mno kwani wengi Bado hawajajua thamani ya muda kwani Bado wanaupoteza pasipo kujua.

Nanukuu kutoka kwa Bruce Lee mwigizaji wa zamani aliyewahi kusema ,"If you love life, don't waste time because it's what life is made up of".

Kama una mapenzi mema na maisha yako, acha kupoteza muda kwani, maisha mazuri huundwa na muda uliotumika vizuri.

Huenda Mimi na wewe ni wadau wazuri sana wa kupoteza muda ila bado hatujajua kua tunajitahidi kuyaharibu maisha yetu.

Ukifuatilia maisha ya matajiri na masikini utagundua Kuna tofauti kubwa katika matumizi ya muda.

Wote tumezawadiwa masaa ishirini na manne lakini wapo wanaojua kufanya kazi masaa hata sita tu kwa siku na kufanikiwa kuliko wanaokesha usiku na mchana.

Yafuatayo ni moja ya mambo ambayo yanapoteza muda na kuchangia sana kuyaharibu maisha yetu na maendeleo kiujumla.

1. Kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja; ni dhahiri kwamba ukifanya mambo mengi kwa wakati mmoja, huwezi kubobea kwenye chochote kati ya hivyo, utaishia kua na ujuzi nusu nusu tu Kisha utapotea, Chagua jambo lako Kisha lifanye kwa mbinu tofauti mpaka uone mafanikio.

2. Kujifananisha na watu wengine;utaishia kujiona upo chini na unakosea kila siku.

3. Kuruhusu kuumizwa na matukio mabaya yaliyopita;hayawezi kubadili a,elekeza akili kwenye matukio yajayo.


4. Kurudia makosa;ili kusonga mbele kimaendeleo,ni lazima tujifunze kutokana na makosa ya kila siku.


5. Kuanza upya kila siku
Hakikisha kila siku unaendeleza jambo lako pale ulipoishia,utakua na furaha na utasonga mbele.

6. Kuruhusu watu waingilie hisia zako.
Maendeleo yako, yanategemea hisia zako za huzuni au furaha, ukiruhusu watu waingilie hisia zako basi hata maendeleo yako yatawategemea wao.

7.Kufanya vitu kwa kufuata mkumbo,yaani
Kutokua na msimamo ni jambo baya kwani litafanya uishie njiani katika kila jambo unalofanya,hakikisha Kuna kitu sahihi unachokiamini katika maisha yako Kisha kifanyie kazi hicho mpaka uone mafanikio.

Mambo hayo yana uwezo mkubwa wa kupoteza muda na kuzuia maendeleo yako, chukua hatua mapema kuyaacha.

Nikutakie maendeleo mema.


photo-1533749047139-189de3cf06d3.jpg
 
Back
Top Bottom