Maelfu waliofaulu darasa la saba wakosa pa kusomea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelfu waliofaulu darasa la saba wakosa pa kusomea

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 17, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi 3,500 waliofaulu mtihani wa taifa wa darasa la saba, mwaka huu, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, hawajachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani katika sekondari za serikali kutokana na upungufu wa madarasa.

  Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Raban Bituro, alisema hayo juzi na kufafanua kuwa wanafunzi hao wameshindwa kuchaguliwa kutokana na upungufu wa vyumba 88 vya madarasa katika shule za sekondari za kata 21 zilizoko wilayani hapa.


  Bituro alisema wanafunzi 12,585 sawa asilimia 97.3, wakiwamo wavulana 6,228 na wasichana 6,357, walisajiliwa kufanya mtihani huo, kati ya hao 6,484 walifaulu.

  Alisema kutokana na upungufu, wamechaguliwa wanafunzi 2,984, wakiwamo wavulana 1,590 na wasichana 1,394 kujiunga na kidato cha kwanza.

  Kutokana na wanafunzi hao kutokuchaguliwa wakati wamefaulu, baadhi yao walichana matokeo yaliyokuwa yamebandikwa na kisha zaidi ya wanafunzi 100 kumfuata afisa huyo ofisini kwake na kumhoji sababu za

  kutochaguliwa na kujibu kuwa ni upungufu wa vyumba vya madarasa.

  Alisema kutokana na wanafunzi hao kuchana matokeo yaliyokuwa yamebandika katika shule za msingi za Bunda na Kabarimu, alilazimika kuchapisha matokeo hayo kutoka kwenye kompyuta na kuwakabidhi walimu wakuu wa shule za msingi ili wayabandike kwenye shule zao.

  Shule 15 Moro zafeli

  Wakati huo huo, shule za msingi 15 mkoani Morogoro zimepata matokeo mabaya baada kushindwa kufaulisha hata mwanafunzi mmoja.

  Kati ya shule hizo, nane zipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ambazo zina wanafunzi 312, wote wamefeli.

  Afisa Elimu wa Mkoa huo, Fatuma Kilimia, alisema shule hizo zimefanya vibaya baada ya wanafunzi wake kupata chini ya alama 100.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...