Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,427
Maelfu ya watu waliandamana katika mji mkuu wa Romania, Bucharest na katika miji mingine mikubwa nchini humo kupinga mabadiliko yanayotarajiwa kufanywa katika mfumo wa sheria, ambayo wanasema yataruhusu ufisadi mkubwa kufanyika bila ya hatua kali kuchukuliwa.
Waandamanaji hao waliandamana katika mitaa kadhaa kuonyesha hasra zao dhidi yaserikali ya mrengo wa kushoto nchini humo ambapo pia wanapinga mabadiliko kuhusu mfumo wa kutoza kodi unaoweza kukasababisha wafanyakazi kupata mapato ya chini.
Maandamano hayo ya jana Jumapili ndiyo makubwa kuripotiwa tangu yale yaliyofanyika mapema mwaka huu kupinga ufisadi nchini humo. Mabadiliko mengine yanayotarajiwa kufanywa ni kumzuia rais kuzuia uteuzi wa majaji muhimu.
Hata hivyo rais wa nchi hiyo Klaus Iohannis amesema atatumia katiba kuzuia mabadiliko hayo.
- DW Swahili