Maelezo ya Dr. Slaa na Mnyika/Makene yanatofautiana

Maelezo ya Dr. Slaa na Mnyika/Makene yanatofautiana

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
579
Wadau,

Lengo langu si kuendeleza mjadala wa Mwigamba, japo swala hili limenichoma moyo kwa sababu mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa wakifurahia kazi kubwa aliyokuwa akiifanya Mwigamba, pamoja na makala murua alizokuwa akiziandika katika safu yake maarufu ya Kalamu ya Mwigamba. Lengo langu katika uzi huu si kuonyesha kuwa Mwigamba alikuwa sahihi au alifanya usaliti, wala si kuonyesha kuwa Uongozi wa Kanda ya Kaskazini umemwonea.

Ninachohitaji kukieleza hapa ni kuwa maelezo aliyoyatoa JJ Mnyika na Tumaini Makene kwa upande mmoja na maelezo aliyoyatoa Dk. Slaa kwa upande mwingine, yote yakijibu hoja ya Mwigamba kuwa katiba ya 2004 ilichakachuliwa, yanatofautiana.

Wakati Mnyika na Makene wanakiri kwamba kipengele cha ukomo wa uongozi kilikuwepo katika katiba ya 2004 ila kikaondolewa katika katiba ya 2006 (rejea maelezo ya Mnyika pamoja na press conference aliyozungumza Makene), kwa upande mwingine Dk. Slaa alikanusha kuwa kipengele cha namna hiyo hakikuwepo katika katiba yoyote. Hapa chini nanukuu maelezo ya Dk. Slaa katika majibu yake ya awali:


WanaJF,

Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kazi kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.

Swali langu ni kuwa, mbona kipengele akisemacho Dk. Slaa kuwa hakijawahi kuwepo kwenye katiba yoyote ya Chadema kimesemwa kuwa kilikuwepo katika tamko la Makene ambalo ndilo tamko rasmi la chama? Je, wakati Makene na Mnyika walipotoa matamko yao (kwa niaba ya chama) walishasoma tamko la awali alilolitoa Dk. Slaa? Kwanini Dk. Slaa alijibu hoja Maskini Mkulima (Mwigamba) bila kufanya utafiti wa kina kwanza?

My Take:
Huu ni mkanganyiko mkubwa sana na unaonyesha ukosefu wa umakini na weledi katika tamko la awali lililotolewa na Katibu Mkuu, Mh. Dk. Slaa. Hili linaonyesha kuwa alitoa tamko kwa kujihami zaidi, badala ya kuangalia mambo yalivyokuwa katika uhalisia wake. Mkanganyiko huu unaweza kuwafanya wanachama (mimi nikiwa mmoja wao) kupata wasiwasi kuwa labda ni kweli kulikuwa na hila fulani kama anavyosema Mwigamba.

Ni vyema Dk. Slaa afanyie tamko lake marekebisho ili kuondoa utata huu.

Nawasilisha na nawasihi tujadili kwa busara ili kujenga chama hiki ambacho kimebeba matumaini ya Watanzania wengi kwa sasa.

Majibu ya Dr. Slaa >

Filipo,
Nilikwisha kutoa Tamko. Sababu ya press Conference ya Jana, ni kuwa tumerudi kufanya utafiti wa kina, tumefukua records zote, tumetafuta hand written drafts, tumetafuta nyaraka zilizopitushwa na Kamati Kuu mbalimbali, tumepitia upya minutes za Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.

Kama ilivyoelezwa Jana hakuna badiliko lolote lililofanyika kinyemela. Ndio maana uchaguzi wa 2009 ambako Mhe.Kassisiko, mkiti wa Mkoa wa Kigoma alichaguliwa kwa kipindi cha tatu na hakuna aliyelalamika( yeye ni mjumbe wa Baraza Kuu wa muda mrefu),na wako wenyeviti wengine kadhaa ambao wamechaguliwa 2009 kwa Mara ya tatu.

Ni Imani yangu kuwa hoja hii sasa haina tija yeyote baada ya Press Conference ya jana. Maamuzi ya chama hufanywa na vikao husika, demokrasia ya kweli ni pale ambapo maamuzi yamefanyika kwa njia ya demokrasia, na Kama kuna upande au kuna mtu hajaridhika anafuata utaratibu tuliojiwekea kueleza kutokuridhika kwake. Nasisitiza, chadema haina cha kuficha, haina sababu yeyote ya kufanya jambo lolote kinyemela. Aidha, Jana ilifafanuliwa kwa kina utaratibu uliotumika kandika upya Katiba ya 2006, tofauti na maelezo mengi kuwa " hatukuandika Katiba mpya..". Tuliandika upya kabisa Katiba. Wanaopenda kuendelea kujadili hoja hii wanaweza kuendelea Kama sehemu ya burudani, lakini wale wote ambao ni serious na ukombozi wa Taifa letu, na hasa mjadala wa Katiba ya Taifa letu, naomba tuelekeze nguvu zetu katika upatikanaji wa Katiba ys Wananchi. Ukombozi wa Taifa letu hautaweza kupatikana bila Katiba ya Wananchi.


Shukrani

Mh. Dk. Slaa,

Nashukuru sana kwa majibu ya hoja yangu, japo vijana wachache wameugeuza huu uzi na kuufanya sehemu ya mipasho na kutukanana, hasa Ben Saanane na vijana kadhaa wa CCM. Binafsi nimefurahishwa na majibu yako.

Nimesikiliza kwa makini sana taarifa ya Tumaini Makene na nimesoma kwa makini, tena kwa kurudiarudia, kile alichokiandika Mh. JJ Mnyika. Nilielewa pasipo shaka kuwa hakukuwa na uchakachuaji wowote kama alivyosema Mwigamba. Nimeamini kuwa Mwigamba alikurupuka kutoa tuhuma pasi na kufanya utafiti wa kina, na yeye kama kiongozi hakupaswa afanye hili.

Ila mkanganyiko wa maelezo yako ya awali na yale ya akina Tumaini Makene ndiyo yaliyonisukuma nitoe hoja hii. Mlipoandaa tamko rasmi la chama lililotolewa jana na Makene, kama ulivyoeleza, mlifanya kwanza uchunguzi wa kina na kuchukua katiba zote za zamani na kuzipitia na ndipo mligundua kile alichokisema kuwa kipengele hicho kilikuwepo lakini hakikuingiza katika katiba mpya ya 2006. Hiki ndicho nidhanicho na wewe pia, hasa Katibu Mkuu wa chama ungekifanya awali kabla hujatoa lile tamko, na hapa ndipo ninapoona ulikosea. Kama nilivyosema kwenye hoja yangu ya msingi, sisi tunawatazama nyinyi kama madereva wa mabadiliko ambayo wengi tunayatamani. Kwa mantiki hiyo, ni vyema umakini uongezeke hasa katika kujibu tuhuma mbalimbali dhidi ya chama. Hili litasaidia sana kuondoa hisia hasi, na litasaidia kupunguza makali ya propaganda hizi ambazo kiuhalisia zina madhara yake, japo madogo, kwa chama.

Vilevile, bado nina maoni kwenu viongozi wakuu wa CHADEMA. Ikiwa kuna kufanya makosa kama haya ya kutoa tamko kabla ya kuchimba kwenye makabrasha yote ya kiofisi (kama nawe ulivyofanya), ni vyema tukaelewa kuwa Bwana Mwigamba naye si malaika, alifanya hivyo kwa kukurupuka, akiongozwa na hisia zake dhidi ya uongozi mkuu. Ikiwa Mwigamba atasimama na kuomba radhi, pamoja na kuonyesha majuto yake kwa kutoa hoja isiyofanyiwa utafiti kwanza, tena hoja iuhusuo uongozi mkuu wa chama (nasikitika bado hajafanya hivyo), tafadhalini msameheni na kumpa nafasi ya pili. Bado binafsi naamini Mwigamba ni mwanamapinduzi mwenzetu aliyepitiwa na jinamizi hili la kutokuwa makini.

Na kwa Ben Saanane,

Filipo Lubua, Sio lazima kutafuta sifa ili tu uonekane na wewe umeanzisha thread

Ni vyema ukajifunza kuwa siasa si kujibizana kwa visirani na kuzodoana. Kama Katibu Mkuu anaweza kuchukua muda wake kutoa maelezo marefu na ya kina, sembuse wewe uliye mwanachama tu? Ni vyema ukajenga mazoea ya kujibu hoja kwa hoja, au kukaa kimya kama umeona hoja haina maana kwako, kuliko kuandika maneno ya kanga ambayo naona yanaishusha hadhi yako na heshima yako na heshima ya chama chetu. Sisi sote ni Watanzania na tuna wajibu sawa wa kulijenga taifa letu. Asante sana kama umenielewa na kama hujanielewa basi sina namna nyingine ya kuelezea.

Ama mwisho niseme tu kuwa, kiukweli hoja ya Mwigamba haina mashiko tena kwa sababu imeshajibiwa, kwa hiyo si vyema ikaendelea kufunika hoja nyingine za msingi kama hija za Katiba Mpya ya Tanzania.

Nashukuru sana Dk. Slaa na nakutakia utendaji mwema. Bado tumaini la Watanzania wengi liko kwako, na sisi, ama niseme mimi, niko nyuma yako
 
Filipo Lubua Majibu yameshatolewa tena huku.Sio lazima kutafuta sifa ili tu uonekane na wewe umeanzisha thread
 
Last edited by a moderator:
Filipo Lubua Mkuu mkanganyiko huo unathibitisha kwamba position hicho kifungu hakijaondolewa kwani katika maelezo yao hakuna anayesema kwamba kifungu hicho kilikuwemo hitimisho lao wote ni moja kwamba allegation za mwigamba ni afterthought kwa hiyo hakuna discrepancy yeyote inayojitokeza katika maelezo ya watu hawa watatu vinginevyo labda mtu aaamue kwa makusudi kutokuelewa.

Ikumbukwe watu hawa wamejibu katika mazingira tofauti ilikuonyesha uwajibikaji wao au tulitaka wajibu yale majibu ya Kisiasa kwamba tusubiri msimamo wa Chama au Mimi siyo msemaji wa chama?
 
Last edited by a moderator:
Majibu yameshatolewa tena huku.Sio lazima kutafuta sifa ili tu uonekane na wewe umeanzisha thread
Ben, wewe ndo umeandika kwa kutafuta sifa. Mimi sijayapata hayo majibu uyazungumziayo. Kama umeyapata mahali fulani ni vyema ungeyapachika hapa ili nami niyaone badala ya kuandika ulichokiandika.

Majibu ya namna hii ndo yasababishayo kukosekane uhuru wa maoni na hatimaye watu wanatumia majina bandia. Umegeuka kuwa kijana ateteaye lolote lile lisemwalo na uongozi hata kama lina walakini? Sidhani kama huo ni mtazamo mzuri katika karne hii ya watu watoao majibu ya hoja.
 
Majibu yameshatolewa tena huku.Sio lazima kutafuta sifa ili tu uonekane na wewe umeanzisha thread

Kauli ya Slaa inanikumbusha Kauli ya George Bush, "Saddam Hussein has the weapons of Mass destruction"
Au Kauli ya Tony Blair, "Saddam Hussein can deploy the mass destruction weapons in 45 minutes"
Au kauli Powell UN " Saddam hussein has the weapons of mass destruction".

Lies, Lies, Lies, throughout and if people do nothing with this kind of lies, then should expect the BIGGER LIES!. so sad!!!!!!
 
Mungu ni mkubwa siku hadi siku anadhihirisha unafiki wa Chadema na ulaghai wao.
 
kwa hivyo BWANA MBOWE atakuwa mwenyekiti wa KUDUMU WA CHADEMA na Dr. SLAA atakuwa KATIBU MKUU WA KUDUMU WA CHADEMA, this is poor thinking, uroho wa madaraka , ufisadi na urafi, poor CHADEMA hata walioanza kuwaamini wameanza kukosa imani na nyie, SLAA na MBOWE ni wale wale kama wengi wa viongozi wa CCM waponda raha na waponda starehe ni vile hawajapata nafasi ya kula tu.
 
Mkuu mkanaganyiko huo unathibitisha kwamba position hicho kifungu hakijaondolewa kwani katika maelezo yao hakuna anayesema kwamba kifungu hicho kilikuwemo hitimisho lao wote ni moja kwamba allegation za mwigamba ni afterthought kwa hiyo hakuna discrepancy yeyote inayojitokeza katika maelezo ya watu hawa watatu vinginevyo labda mtu aaamue kwa makusudi kutokuelewa.

Ikumbukwe watu hawa wamejibu katika mazingira tofauti ilikuonyesha uwajibikaji wao au tulitaka wajibu yale majibu ya Kisiasa kwamba tusubiri msimamo wa Chama au Mimi siyo msemaji wa chama?

Mkuu, nashukuru kwa maelezo. Ila kama umemsikiliza vizuri Tumaini Makene katika tamko lake la press conference, ametamka wazi kuwa kifungu hicho kilikuwepo kwenye katiba ya 2004. Ila, kwa mujibu wa maelezo yake, kifungu hicho hakikuingia kabisa katika katiba mpya ya mwaka 2006. Hoja ya Makene, ambayo nami pia nimeilewa barabara, ni kuwa kifungu hicho hakikunyofolewa kinyemela kama alivyisema Mwigamba ila hakikuingizwa kabisa kwenye katiba ya 2006. Tofauti inayokuwepo kati yake na Dk. Slaa ni kuwa Dk. Slaa yeye anakanusha kuwa kifungu hicho hakikuwahi kuwepo kwenye katiba yoyote tangu ile ya 1992, na hapo ndipo nipazungumziapo.
 
Hili limeshatolewa ufafanuzi mara kibao - kwa sasa tunajadili mustakabali wa taifa letu kuhusu kutengwa wenye EAC.
 
kwa hivyo BWANA MBOWE atakuwa mwenyekiti wa KUDUMU WA CHADEMA na Dr. SLAA atakuwa KATIBU MKUU WA KUDUMU WA CHADEMA, this is poor thinking, uroho wa madaraka , ufisadi na urafi, poor CHADEMA hata walioanza kuwaamini wameanza kukosa imani na nyie, SLAA na MBOWE ni wale wale kama wengi wa viongozi wa CCM waponda raha na waponda starehe ni vile hawajapata nafasi ya kula tu.


Mkuu, kama katiba inaruhusu na kama wakichaguliwa na wanachama kidemokrasia, basi hilo si tatizo. Mimi nilichokisungumzia hapa ni usahihi na usawa (consistence) wa maelezo yao; yanakinzana na yanatia wasiwasi kuwa viongozi wanakurupuka kujibu hoja badala ya kuzifanyia uchunguzi wa kina kwanza.
 
Ben, wewe ndo umeandika kwa kutafuta sifa. Mimi sijayapata hayo majibu uyazungumziayo. Kama umeyapata mahali fulani ni vyema ungeyapachika hapa ili nami niyaone badala ya kuandika ulichokiandika. Majibu ya namna hii ndo yasababishayo kukosekane uhuru wa maoni na hatimaye watu wanatumia majina bandia. Umegeuka kuwa kijana ateteaye lolote lile lisemwalo na uongozi hata kama lina walakini? Sidhani kama huo ni mtazamo mzuri katika karne hii ya watu watoao majibu ya hoja.

Kufikia hatua ya kuanzisha thread bila utafiti ni kuonyesha kukosa umakini.

Halafu hizo hisia kwamba natetea kila kitu ni upuuzi mtupu ikiwa huwezi kuzithibitisha hapa.

NB:Majibu yapo hapa.Ungesoma page zote kwenye thread hii usingekurupuka kuanzisha thread mpya kama sio sifa

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/545874-kuhusu-katiba-ya-chadema-ufafanuzi-huu-hapa%3B-watoa-tuhuma-hawana-hoja-walete-nyaraka-14.html
 
Ben, wewe ndo umeandika kwa kutafuta sifa. Mimi sijayapata hayo majibu uyazungumziayo. Kama umeyapata mahali fulani ni vyema ungeyapachika hapa ili nami niyaone badala ya kuandika ulichokiandika. Majibu ya namna hii ndo yasababishayo kukosekane uhuru wa maoni na hatimaye watu wanatumia majina bandia. Umegeuka kuwa kijana ateteaye lolote lile lisemwalo na uongozi hata kama lina walakini? Sidhani kama huo ni mtazamo mzuri katika karne hii ya watu watoao majibu ya hoja.
Mkuu huyu jamaa anatetea ajira yake wala asikusumbue huyu ni nyoka wa Dr na Mnyika wala usitegemee
chochote kutoka kwake kwanza kwenye chama yeye ni nani?
 
Majibu yameshatolewa tena huku.Sio lazima kutafuta sifa ili tu uonekane na wewe umeanzisha thread

zamana ben saanane nilimwona kama mtu makini ambaye anaongea kwa hoja, ila hivi sasa nikisoma maandiko yake nashindwa kuamini kama ni yeye anakuwa ameyaandika au account yake inatumiwa na mtu mwingine, amekuwa akitoa hoja dhaifu sana, ameuweka usomi wake pembeni amebaki anatetea mambo mengine ambayo ni ya kijinga. Ben siku hizi amekuwa dhaifu sana amekuwa mfungwa si mtu huru tena ni mfungwa wa kifikra. Badilika kaka unaaibisha
 
Kufikia hatua ya kuanzisha thread bila utafiti ni kuonyesha kukosa umakini.

Halafu hizo hisia kwamba natetea kila kitu ni upuuzi mtupu ikiwa huwezi kuzithibitisha hapa.

Mkuu, mara ngapi umethibitishiwa au umeletewa vielelezo na bado umekuwa mbishi? hakika wewe ni mtu wa ajabu sana na unashangaza sana
 
Mkuu huyu jamaa anatetea ajira yake wala asikusumbue huyu ni nyoka wa Dr na Mnyika wala usitegemee
chochote kutoka kwake kwanza kwenye chama yeye ni nani?

Mkuu, Ben Saanane amekuwa kama msukule vile. maadam ameambiwa kuwa pigania chama cha babu na bibi basi anajitoa ufahamu kabisa
 
Mkuu huyu jamaa anatetea ajira yake wala asikusumbue huyu ni nyoka wa Dr na Mnyika wala usitegemee
chochote kutoka kwake kwanza kwenye chama yeye ni nani?
Wewe unatetea nini?Jadili issues acha ujinga
 
Back
Top Bottom