Maelezo binafsi ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya tuhuma za rushwa kwa Umma

Umeongea vizuri sana mwenye ushahidi wake wakuwa umepokea rushwa atoe sio kuleta majungu tu,
Rushwa yenye akili haiachagi ushahidi. Ndio maana unaona vigogo wa CCM wala rushwa wanapeta hadi leo. Waliochukua rushwa kipumbavu ndio wanao-umia.
 
Umesomeka Mh. Zitto, endelea kupambana na vikwazo kama hivi ndio vinakupitisha ndani ya tanuru na kukukomaza. Kumbuka, pamoja na kufanya kazi zenu kama POAC jaribuni kufanya mambo kwa principle zinazotabirika na sidhani kama ni busara kamati iwe 'ina-react' kila linapotokea jambo; na hata hili la Tanesco.

Naona kuna jambo haliwekwi wazi; aidha kwa makusudi au kwa kujumuisha mambo mengi kwa pamoja, bodi inamsimamisha DG wa Tanesco kwa uchunguzi na hapo hapo POAC ina-react kutaka nayo ichunguze, mara tuaambiwa ugomvi kati ya mwenyekiti wa POAC na Waziri/Katibu Mkuu????!!!!

Mnapokuwa OPPORTUNIST kujaribu ku-score political points kwa kila gogoro linaloibuka mtaishia kuunguza vidole.

Yaani Bunge limejikuta likitumia vibaya nafasi yake ya kuisimamia na kuishauri serikali kwa kujiingiza kwenye masuala ya utawala na utendaji wa siku hadi siku. Wameacha kuisimamia serikali katika masuala ya kisera, sasa wanakuwa mawakala wa wafanyabiashara waliokosa zabun.i
 
Nilipomwona Zitto anachakarika kutafuta sahihi za kumwondoa WM Pinda madarakani wakati yeye kama Waziri Mkuu hakuwa na kosa nikadhani hali kama hiyo ikimtokea Zitto atajiuzulu mara moja bila kusubiri ushahidi unaothibitika! Kumbe Zitto mwenyewe hayuko hivo. Kuna nini cha mno kwenye uenyekiti wa POAC? Kiongozi wa UMRI wa Zitto hapaswi kung'ang'ania madaraka ambayo ni ya kupewa tu.
 
Mh.ZZK pambana na hakika penye ukweli uongo hujitenga simamia haki na kweli ww na nafsi yako kwa maslahi ya TZ.nashukuru kwa kuwa uko tyar kutoa ushirikiano ili ukwelii ubainike othyc God bless u.
 
zzk anasema yupo tayari kujiuzuru yeye uenyekit POAC,ili awanusuru wajumbe wengine wa POAC! KAULI hii inaonyesha zito ana mapenzi na poac kuliko CDM, COZ,mara nyingi amehusishwa na tuhuma za kuhujumu cdm lakini hajawahi kusema yupo tayari kujiuzuru cdm ili kukinusuru chama chake!
bado naamini kuwa huyu dogo ni muhimu ktk chama lakini inabid kuwa na tahadhari naye sana
 
shida ya wanasiasa wa nchi hii wanaongea sana na tunashindwa sasa tumwamini nani,mara mifuko ya jamii,mara matrilioni,mara mishahara ya wabunge na malupulupu endless list,ebu tungoje mwisho wa ubaya tu
 
Hili lilikuwa kumbora kumlenga nani?

hapo ndio uamini kuwa huyu dogo anatumwa na ccm kwa kazi maalum, maana unapotaja neno 'upinzani bungeni wenye midomo mikubwa ndo mabingwa wa rushwa'maana yake ni CDM, Kwa kuwa ndio wanaongoza kambi rasmi ya upinzani bungeni.zitto usiwagawe wanachama plz, hakuna aliye maarufu kuliko chama.
 
ndio maana siasa huwa siiamini hamuaminiki si zito wala kikwete wala slaa wala lipumba wote wasaliti tu heri tuwatoe wote tueke watu wa jf waonoge nchi
 
Mhe. Zitto umekua Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma kwa muda gani mpaka hivi sasa? Kama umekua kwa vipindi vyote viwili vya hapo bungeni nafasi hiyohiyo ya uenyekiti kwa takribani miaka saba (7) sasa, na wananchi tumekua tukishuhudia madudu makubwa makubwa yakifanywa na mashirika haya ya umma kupitia watumishi wa mashirika hayo mfano Shirika la nyumba la taifa (NHC), Mashirika ya mifuko ya jamii nk.....Tumekua tukishuhudia upatikanaji wa watumishi katika mashirika hayo kwa njia ambazo sio halali huku wewe Mhe Zitto ukiwa mwenyekiti wa hiyo kamati ya bunge ya mashirika ya umma, ambavyo mashirika hayo yanawajibika moja kwa moja kwenye kamati yako.

Tumekua tukipandishiwa bei ya umeme kwa kasi isiyo ya kawaida kwa kipindi chako chote cha uongozi katika hiyo kamati na madudu yaliyotajwa na waziri wa nishati na madini katika hotuba yake juu ya wizi/ubadhirifu/uujumu/ufisadi na ujambazi wa kiwango cha Ph.D uliokuwa ukifanywa ndani ya shirika la usambazaji umeme (TANESCO) chini ya huohuo uenyekiti wako bado tu unaona kamati yako ya POAC haistahili kuvunjwa?

kipindi fulani Katibu mkuu wizara ya ardhi alitoa kauli yake waziwazi kuwa NHC ni pango la wala rushwa na baadhi ya watumishi wa shirika hilo wamekua wakijimilkisha majumba ya shirika hilo tena prime areas ( maeneo ya CBD) kwa kupangisha na kuelekeza kodi za majengo hayo ya umma kwenye mifuko yao. Wewe Mhe Zitto ukiwa mwenyekiti wa kamati hiyohiyo, vilevile mifumo ya kupangisha haijakaa vizuri watu wamepanga katika hizo nyumba tangu mwaka 1961 shirika likiwa bichi na bikra ila mpaka leo mtu huyo ambaye ni hayati ameacha vitukuu vyake bado vinaendelea kuishi, sasa watanzania hawa wanaokaa miaka yota katika nyumba za shirika la umma na baadhi yao wanavuka mipaka na kuchukua majukumu ya kuzipangisha kwa bei ya juu kwa watanzania wengine na hata wasio watanzania, je haya ndio malengo ya kuundwa kwa shirika hili la nyumba la taifa? Wewe kama mwenyekiti nilitegemea haya yote utakabiliana nayo na kurekebisha, ila mpaka sasa hali ni hiyohiyo.

Kazi ya hiyo kamati katika kusaidia na kuzilinda rasilimali za taifa kwa ajili ya watanzania wote katika kufaidika na kunufaika kwao na rasilimali zao imefeli na naipa zero kabisa kamati hiyo na naomba mheshimiwa spika aivunje na kuundwa upya. Vilevile viongozi na wajumbe wote wa kamati ikiwezekana wachunguzwa na kama wakithibitika kwa namna yeyote walikuwa wakinufaika na uozo unaofanywa na mashirika yetu ya umma basi hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi yao ili liwe fundisho kwa wanaokuja kuiongoza kamati husika.

Watanzania mapenzi yetu kwa viongozi wa CHADEMA yasipelekee kuona madhambi yao kama suna au mema, dhambi haiangalii itikadi ya mwanasiasa huyo na mwanachama au kiongozi wa chama chochote cha siasa anapohusishwa au anapojihusisha na ufisadi kwa namna yeyote ile hata kwa kutoa ushauri tu basi awajibishwe kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria.
 
just wait.kama umeula vumilia kwani umefika hapo kwa kuamua kwenda too fast.Kila mtu alikuwa akikuangalia na kukuombea uifaidi njia uliyoichagua na upo determined kutoiacha sasa unataka huruma ya Nani?

Unapiga sana kelele kuwa unaweza watu wanakunyima urais, huku ukisahau kuwa kama ni utendani uwaziri mkuu ndio pakee.Bado utajichafua na kuchafuliwa na mwaswahiba wako wa ccm kuliko unavyotaka chafua chama unachotaka simama kwa bendera yao.Mbaya busara zao wameamua kuacha ujichafue sana mwenyewe,huku ukitaka kigoma ipigane nyuma yao.Ila unasahau kuwa umri wako ni mdogo kusubiri miaka michache kutakujenga.

Kwa taarifa yako Zitto kelele ulizopiga na hii kashfa watu wanakushangaa, hata wewe mwenyewe umekosa moral authority kiasi hata hotuba zako huna tena ile sauti iliyozidi mwili wako.
 
mimi ningekuwa zitto, ningeanza kutangaza mali zangu muda huu, badala kupoteza muda kuchochea tuhuma zaidi. maana pengine mali nyingi kuliko kipato ndio zinazua tuhuma kwa mbunge wetu
 
yaani huoni hata aibu??? (hapo kwenye nyekundu).

Huna hoja? Kuna wengine ambao hawajafuatilia hili suala kwanini usieleze kwa kirefu ni wapi nimekosea. Don't be a slave of other people's opinion
 
Nadhani hapa tunaona picha halisi ya zzk kwamba haelewiki sana. Tafsiri zinaweza kuwa nyingi katika hili "

  1. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  2. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa."
TAFSIRI MOJA WAPO INAWEZA KUWA: 1.Kwa hiyo wewe ulijipendekeza kwa spika anaetoka ccm ndiyo maana amekuchagua? 2. Aliona kwamba ww hutofautiani sana nao ndiyo maana wakakupa nafasi nyeti ili uwalinde? 3. inaonekana haupo pamoja na wenzako-either kwa makusudi au kwa kukuona kwamba wewe unaelekea kuwa msaliti? 4. Kwamba hata wewe usingefurahia kama hiyo nafasi angepewa mtu mwingine kutoka upinzani-ndiyo maana unahisi hawafurajii wewe kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo nyeti-'yamtokayo mtu ndiyo yaujazayo moyo wake'. HIZI NI BAADHI TU YA TAFSIRI YA MAZUNGUMZO YAKO KWENYE HOJA MBILI. HOJA ZAKO NYINGI ZIMEKUWA ZIKIACHA MASWALI KULIKO MAJIBU
 
Hotuba kama hii aliyoitoa ZZK siwezi kuitofautisha na utetezi wowote ambao ungeweza kutolewa na mtu yeyote eidha awe ana makosa au hana! ametumia sana "vague sentences" ambazo kwa akina sie hazitusaidii sana! Ningetegemea katika press conference ile angejaribu kupiga specific issues zitazo-support utetezi wake, na pia evidence kama anazo! vinginevyo ni muendelezo wa ngonjera tu!
 
Inawezekana ZZK si mla rushwa. Inawezekana pia kuwa ZZK ni mla rushwa. Naamini ZZK si malaika. Naamini pia ZZK ni mwanasiasa, na nionavyo mimi, wanasiasa si watu wa kuwatumainia sana, kwani hunena uongo mwingi kuliko ukweli.
:rant:
 
tulikuamini kaka,na bado tunakuamini lakini ktk hili ngoja tusubiri matokeo ya tume siamini kama hata wabunge wa chadema wanaoilaumu POAC nao watakuwa wanakupinga kwa maslahi yao binafsi siamini anyway tusubiri
 
Back
Top Bottom