Maelekezo ya Waziri Silaa yatekelezwa

Maelekezo ya Waziri Silaa yatekelezwa

Joined
Oct 14, 2011
Posts
98
Reaction score
121
Maagizo ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Slaaa yameanza kutekelezwa kikamilifu ambapo Viongozi na Maafisa wa Wizara yake wamepiga kambi tangu jumatatu ya tarehe 8 Machi 2024 katika eneo la Olmoti linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa kisasa Jijini Arusha.

Maagizo hayo aliyatoa Waziri Silaa siku ya jumamosi ya tarehe 6 Machi 2024 kwa Katibu Mkuu wa Wizara yake kuhakikisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani na wataalamu wao wamefika eneo hilo kufikia jumatatu asubuhi ili kuanza Upangaji na upimaji wa eneo hilo.

Waziri Silaa alisema hayo wakati wa Hafla ya kumkabidhi Mkandarasi eneo la ujenzi wa Uwanja wa Kisasa wa Mpira wa Miguu unaotarajiwa kujengwa na unatazamiwa kutumika kwenye michuano ya AFCON 2027 Jijini Arusha.

Aidha, Waziri Silaa alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake kuhakikisha maeneo yote yanayozunguka uwanja huo wa michezo unaotarajiwa kujengwa ni lazima yawe yamepangwa na kupimwa ili kupusha makazi holela na migogoro ya ardhi hapo baadae.

Katika kuhakikisha jambo hilo linakamilika kwa wakati Waziri Silaa alitoa wito kwa Makampuni binafsi yanayojihusisha na kazi za upangaji na upimaji kushiriki katika kazi hiyo ya kupanga na kupima maeneo yote yanayozunguka uwanja huo wa mpira wa miguu.
 
Waziri Silaa aje atembelee UKEREWE alone hali ilivyo. Hakuna National housing; watu, wafanyakazi wanalazimika kuishi katika makazi duni ya kupanga ambayo hayaridhishi. Hamna hoteli wala majengo kwa ajili ya benki. Tafadhari njoo uone hali halisi.
Kuna beach safi sana kule Rubya ambazo zingefaa kujenga hotels za kitalii.
Watafutwe wawekezaji kwa ajili ya "Water taxis" ambazo zitasaidia usafiri ndani ya visiwa.
 
Back
Top Bottom