Ahsante kwa mada nzuri, kwa rukhsa yenu na mie nachangia kidogo,
Tatizo kubwa la binadamu ni akili zetu, akili ni moja ya Silaha yenye nguvu kubwa sana, ina uwezo wa kumuangamiza binadamu maisha yake yote, inaweza kumjenga au kujenga mazingira ya mwanadamu milele, akili ni kitu hatari sana ama kwa matokeo ya positive au negative.
Sisi binadamu hatujui kuwa akili zetu zinaweza kuwa programmed, zinaweza kujengewa na kuelekezwa nini zifanye au nini zisifanye,nini zifikirie au nini zisifikirie,nini ziamue au nini
zisiamue. Programs zinazoijenga akili ni kama elimu,dini,taarifa za habari,sanaa/movies na mazingira yetu ya kijamii
Programs hatari sana ni elimu na dini hizi zina uwezo wa kujenga reality kwenye akili,reality ambayo inaweza kuwa sio uhalisi hata kidogo lakini akili haitakuwa na uwezo wa kujinasua, itachukulia kila kitu ni halisi,programs za dini na elimu zinaitia kufuli akili ile kumtawala mwanadamu.
Kwa mfano:
mfumo wa elimu unasema namba zinaanza 0 mpaka 9, hapa maana yake akili za watu wote dunia nzima zimetiwa kufuli na haziwezi kutoka nje ya 0-9, inawezekana kabla ya zero kuna namba na baada ya tisa kuna namba nyengine lakini akili zimetiwa kufuli hazitoki tena nje ya 0-9, yaani kwenye akili ya mwanadamu nje ya 0-9 ni kiza kitupu,hatuoni kitu hata kama kuna mwangaza mkali sana na kuna mambo mengi sana akili zetu zinatufanya tuone kiza kitupu milele na milele, hapa namaanisha kuwa 0-9 ni mipaka ya chuma na hatuwezi kutoka nje ya hapo,maarifa yetu yote dunia nzima yaanzia 0-9, akili za binadamu wote zinaazia zero zinaishia nine,hebu jipime na ujaribu kufikiria namba mpya kabla ya zero au baada ya tisa kama utaweza, akili zake hazitakuruhusu hata kujaribu.
Mipaka ya aina hii ndio inayosababisha maisha yetu yote binadamu yanatabirika, hii ndio inayoijenga psychology ya mwanadamu, hii ndio inayoitawala psyche ya mwanadamu na kuifanya iwe limited, hii ndio inayomfanya mwanadamu asijitambue na asiwe na sovereignty yake mwenyewe,yaani elimu za kutunga ndio zinaijenga psyche ya mwanadamu alie halisi,elimu hizi zimetungwa na watu na ndio zimeiwekea mipaka akili za watu wengine
Nirudi kwenye mada, tatizo letu ni akili zetu na hatujitambui,hata uwe na elimu kiasi gani,hata uwe na cheo gani, hata uwe na pesa kiasi gani sisi binadamu hatujitambui wenyewe,tunaendeshwa na codes na standards,codes and standards zipo kwenye elimu zetu na dini zetu,kila tunachofanya tunafanya kwa matakwa ya elimu au dini,itatengemea una elimu kiasi gani au una dini kiasi ile update matokeo aina gani kwenye maisha yako au utaishi maisha ya aina gani.
Niishie hapa kwa sasa, pengine baadae ntarudi nitoe mifano ya dini inavyotutia kufuli kama nlivyotoa mifano ya elimu.