Maelekezo ya Kufeli

Maelekezo ya Kufeli

Clayton Paul

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
2,136
Reaction score
4,411
Toka kwa The Light Keepers
Ni ngumu ndege aliyezaliwa katika uzio kujua nini maana ya uhuru na hata akiachwa mlango ukiwa wazi ni ngumu kumkimbia mfugaji.

Hapo ndipo ulipo mtego wa maisha yetu. Ona huo uzio kama sheria na tamaduni amabazo umewekewa na mtu au watu fulani katika kufanya na kufanikisha jambo. Mfano halisi watu wengi kuamini huwezi kufanikiwa bila elimu au kuajiriwa. "Elimu iligunduliwa na wenye akili wakijua watakao ishika watakuwa ni wasio na akili".

Yote haya wanayafanya kwa kuwa wanajua Kuna mamlaka ya juu Sana ktk umiliki tabia za mwanadam au kuzitabiri. Kupitia Elimu na mitaala wanajua fika utatoka ukiwa mtu wa Aina gani na utaishia Kona gani.

Kwa kuwa fikra zetu ni kujitafakari kwa kike ambacho hatuna na kupuuza tulicho nacho .Basi tunapoteza vikubwa na kukumbatia vidogo.

Kwanini ugumu wa maisha upo ?
Wengi tunafuata na kutii sheria zilizowekwa na walio juu. Kitu kibaya sana tumejifunza, kuzikubali na kuziishi bila kuzihoji hizo sheria. Unapewa njia yenye mipaka kiunafiki.

Sheria au maelekezo hayo ukiyafuata si ajabu ukaangukia pua. Hizo zoote ni Dhana amabazo waliziunda ili kuupangilia ulimwengu kuelekea matakwa Yao.

Yataka Umakini ili ugundue kuwa Dhana ( sheria ) hizo ni kingo za wewe kufanya jambo na kusonga zaidi (Zinazuia mapana ya uwezo wako).
Dhana hizo ni jela halisi wanazoishi raia wengi kwa kujihami Jamii itawaonaje.
Mana unachotaka kufanya ukifanya tofauti na walivyozoeshwa ni utata.

"Kuna njia moja tu katika kuokoa maisha yako ya mbeleni nayo ni KUITENGENEZA" Acha kupita mapito ya watu na kuyafanya kuwa yako. Mfano kusoma vitabu na kupita mferji ule ule wa muhandishi pasipo kwenda mbali zaidi, wakati na Zama zitakuumbua Mana maswali ni yake Yale ila majibu lazima yawe tofauti.

Anguko linakuja pale unapotaka kulazimisha na kuharakisha ili kuwaaminisha watu kuwa upo sahihi.
Unahitaji uvumilivu mkuu maana huwezi kujenga sifa kwa kulazimisha na kushindana na asili hiyo.

UVumilivu una mambo makuu mawili:
1.Utayari
2.Upendo.
Kuwa tayari kuanzisha jambo na elekea vita kuipigania jambo hilo na matokeo yake. "pigania unachopenda, penda unacho kiheshimu na heshimu unachokijua".

Manhesimu Elimu na tafiti msizozijua, hapo mmeyumbishwa na hamkuelimishwa.

Nyuma geuza Quote hiyo, inakuja kuwa:
Unatakiwa kujijua ili Ujiheshimu na kisha kujipenda.

Je unajijua wewe ni nani ?
 
Ahsante kwa mada nzuri, kwa rukhsa yenu na mie nachangia kidogo,

Tatizo kubwa la binadamu ni akili zetu, akili ni moja ya Silaha yenye nguvu kubwa sana, ina uwezo wa kumuangamiza binadamu maisha yake yote, inaweza kumjenga au kujenga mazingira ya mwanadamu milele, akili ni kitu hatari sana ama kwa matokeo ya positive au negative.
Sisi binadamu hatujui kuwa akili zetu zinaweza kuwa programmed, zinaweza kujengewa na kuelekezwa nini zifanye au nini zisifanye,nini zifikirie au nini zisifikirie,nini ziamue au nini
zisiamue. Programs zinazoijenga akili ni kama elimu,dini,taarifa za habari,sanaa/movies na mazingira yetu ya kijamii
Programs hatari sana ni elimu na dini hizi zina uwezo wa kujenga reality kwenye akili,reality ambayo inaweza kuwa sio uhalisi hata kidogo lakini akili haitakuwa na uwezo wa kujinasua, itachukulia kila kitu ni halisi,programs za dini na elimu zinaitia kufuli akili ile kumtawala mwanadamu.
Kwa mfano:
mfumo wa elimu unasema namba zinaanza 0 mpaka 9, hapa maana yake akili za watu wote dunia nzima zimetiwa kufuli na haziwezi kutoka nje ya 0-9, inawezekana kabla ya zero kuna namba na baada ya tisa kuna namba nyengine lakini akili zimetiwa kufuli hazitoki tena nje ya 0-9, yaani kwenye akili ya mwanadamu nje ya 0-9 ni kiza kitupu,hatuoni kitu hata kama kuna mwangaza mkali sana na kuna mambo mengi sana akili zetu zinatufanya tuone kiza kitupu milele na milele, hapa namaanisha kuwa 0-9 ni mipaka ya chuma na hatuwezi kutoka nje ya hapo,maarifa yetu yote dunia nzima yaanzia 0-9, akili za binadamu wote zinaazia zero zinaishia nine,hebu jipime na ujaribu kufikiria namba mpya kabla ya zero au baada ya tisa kama utaweza, akili zake hazitakuruhusu hata kujaribu.

Mipaka ya aina hii ndio inayosababisha maisha yetu yote binadamu yanatabirika, hii ndio inayoijenga psychology ya mwanadamu, hii ndio inayoitawala psyche ya mwanadamu na kuifanya iwe limited, hii ndio inayomfanya mwanadamu asijitambue na asiwe na sovereignty yake mwenyewe,yaani elimu za kutunga ndio zinaijenga psyche ya mwanadamu alie halisi,elimu hizi zimetungwa na watu na ndio zimeiwekea mipaka akili za watu wengine

Nirudi kwenye mada, tatizo letu ni akili zetu na hatujitambui,hata uwe na elimu kiasi gani,hata uwe na cheo gani, hata uwe na pesa kiasi gani sisi binadamu hatujitambui wenyewe,tunaendeshwa na codes na standards,codes and standards zipo kwenye elimu zetu na dini zetu,kila tunachofanya tunafanya kwa matakwa ya elimu au dini,itatengemea una elimu kiasi gani au una dini kiasi ile update matokeo aina gani kwenye maisha yako au utaishi maisha ya aina gani.
Niishie hapa kwa sasa, pengine baadae ntarudi nitoe mifano ya dini inavyotutia kufuli kama nlivyotoa mifano ya elimu.
 
Usisahau ahadi Captain
 
asante sana, tafakuri muhimu sana kwa kizaai hichi, ila naturally wanadamu tuna uwezo mkubwa kuliko tunaoutumia, tuko limited sana na mazingira au wanaotuzunguka.
 
Back
Top Bottom