Maegesho ya magari ya kisasa

Maegesho ya magari ya kisasa

Jidu

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
1,232
Reaction score
757
Haya ni maegesho ya kisasa kabisa ya kutuondoshea usumbufu mjini!

parking iliyoenda shule.jpg
 
Hawa watu wenye akili ya kubuni hivi, kiongozi wao mkuu wa nchi huwa akimaliza mwaka madarakani basi ni bahati yake. Sisi tumeng'ang'ania magamba mpaka ubongo umeota kutu!
 
Haya yapo siku nyingi sana. Hata bandari ya HAMBURG, German, wanatumia System hii kupakua Makonteina kwenye meli na kuyapanga hapo bandarini. Wajapan na Scandnavian/Uholanzi, wanaitumia kupark Baiskeli zao. Nafikiri imeanza kuwa mashuhuri miaka ya 90.
 
rush hour mnaondokaje hapo? manake kila mtu anataka kwenda nyumbani
 
rush hour mnaondokaje hapo? manake kila mtu anataka kwenda nyumbani

lane unayo paki ina uhusiano na muda wa kutoka. suala la kuwai nyumbani limeshahusishwa humo. siyo kuwa unapaki tu, kumbuka unalipa hapo na kuna sheria nzito, kama unazidisha muda, hapa siyo kuzidisha bila kulipa, bali kama ulisema unakaa masaa 2, kuzidisha muda ni gharama kubwa, hivyo utajikuta unalazimika kupanga muda wa kupaki kwa uhakika bila mabadiliko
 
Vibaka wa laptop na side mirrors bongo watakula wapi? Wale wazee wa mitungi wasiruhusiwe kabisa karibu na maeneo hayo,bila havyo zitakua SENEMA za ajabu kila siku...
 
Miaka hamsini ya uhuru vitu kama hivyo ni ndoto kila kukicha ni ufisadi, kuiba madini na kugombania nafasi za kutawala kwenye vyama na serikali na wanaogombania hata uwezo wao wa kutawala ni mdogo
 
Back
Top Bottom