Madudu ya mkuu wa mkoa wa Mara

Madudu ya mkuu wa mkoa wa Mara

anania

Member
Joined
Jul 2, 2010
Posts
83
Reaction score
8
Mkuu wa mkoa huyo aliona vipi kama ngeruhusu gari liende hata kullala nje ya kituo cha police kama alikuwa anataka kulikamata gari.waliopata mateso si kampuni ya zuberi ila wa watanzania hasa watoto na kina mama waliokuwemo ndani ya gari hilo.nionavyo mimi hizi ni vita za kibiashara hivyo mkuu wa mkoa ilitakiwa afuate utaratibu unao faa sio huo wa kuhatarisha maisha ya watanzania na je hayo maisha bora kwa kila mtanzania watayapata wakiwa ndani ya matumbo ya wanyama wakali?

Ningeshauri mkuu wa mkoa wa mara aachie ngazi kwani alichemka na bila shaka alifanya hivyo pengine alikuwa amelewa au kwa sababu ilikuwa usiku alifanya hivyo kwa shinikizo la mke wake kwani wenzetu akina mama wana convincing power kubwa hata ukaamua kumhonga mkoa bwako.

Baba achia ngazi umetokoooooootaaaaa ile mbayaaaaa
 
anania basi lililozuiliwa safari sio kampuni ya ZUBERI ni kampuni ya ZAKARIA tajiri wa Tarime lilizuiliwa eneo la fort Ikoma ukiwa unaingia hifadhi ya taifa ya serengeti.
 
Rc huyu ni mtemi ana amri za kiafande na ni mkali mno,nimeshawahi kumwona ktk mkutano mmoja, anajiamini,anaweza kaa wiki tatu bila kuonekana meno,ila kwa hili amezidisha
 
Mkuu stori yako ni nzuri lakini haielezi tukio zima lilikuwaje. Tunaomba utupe zaidi.
 
Ndio alivyo huyo.
Namfahamu sana kabla ya kupewa promotion hiyo na JK, alikuwa DC wa Mpwapwa-Dodoma.
Hajatulia kabisa na hana sifa za uongozi na hasa wa ngazi kubwa kama ya u-RC, hawa ndo wale waliopewa fadhila na JK.

Ombi kwangu ni kuwa, abiria na mmiliki wa Kampuni ya Zakaria wampeleke RC huyu mahakamani ili sheria ifate mkondo wake. Watanzania tuache woga na uvivu wa kufukiri tuanze sasa na huyu ili kupata haki zetu, na ifike mahali tuwe na wakuu kama Mheshimiwa Lukuvi (Mnyalukolo).
 
Kwani askari walikuwa wapi mpaka hilo basi linaondoka na kufika kote huko? Au muheshimiwa alipigiwa simu baadae sana na watu fulanifulani kumfahamisha kuwa mbona basi limeruhusiwa kuondoka??

Huyu Muheshimiwa angetumia Busara, Angeliacha hilo basi lifike then awachukulie hatua za kinidhamu!! kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa!!?
 
Huyo jamma aligombea Ubunge Lushoto akapigwa chini ile mbaya ...... i mean ile mbaya . ... kwa huruma za JK akapewa mkoa. Jamaaa hafai katika maama kuwa hafai....... wamasai wamekoma na huyo bwana. Hakuna demokrasia mkoani Manyara hata kidogo.

kwa kweli ang'olewe tu arudi Lushoto akachume matunda
 
Rc huyu ni mtemi ana amri za kiafande na ni mkali mno,nimeshawahi kumwona ktk mkutano mmoja, anajiamini,anaweza kaa wiki tatu bila kuonekana meno,ila kwa hili amezidisha

Labda U-Muraa umemzidishia makucha yake!
 
Kwani yeye anahusika vipi kwenye Trafic case kama mkuu wa mkoa?? naomba kuelewa undani wa story yenyewe!
 
Back
Top Bottom