Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,962
- 166,352
UKIUKWAJI wa sheria, taasisi za serikali kushindwa kutimiza wajibu wake pamoja na rushwa, ni miongoni mwa sababu za kuanguka kwa maghorofa Jijini Dar es Salaam, imebainika.
Utafiti uliofanywa na MTANZANIA Jumapili, katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam, umebaini madudu ya kutisha, hali ambayo inaashiria sekta ya ujenzi inaelekea kuanguka nchini.
Uchunguzi wa MTANZANIA Jumapili unakuja ikiwa ni takribani miaka saba tangu ripoti ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kugundua kuwa Jiji la Dar es Salaam lina maghorofa 1,000 yaliyojengwa chini ya kiwango.
Pamoja na hilo, katika uchunguzi wake, gazeti hili pia limebaini kuwa ripoti hiyo ya Lowassa haijawahi kufika Wizara ya Ardhi.
Mtanzania Jumapili katika utafiti wake pia limegundua kuwa maghorofa karibu yote yaliyojengwa katikati ya Jiji la Dar es Salaam hayafai, kwa sababu yamekiuka sheria, huku Wizara ya Ardhi ikionekana kulifahamu vyema suala hilo.
Pia hayakutekeleza Sera ya mipango Miji pamoja na Sheria namba 8 ya mwaka 2007 ambayo inaagiza utekelezaji huo.
Katika hilo, taasisi za serikali, ikiwemo Bodi ya Wakandarasi nchini (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na Manispaa za Jiji zinashutumiwa kwa kushindwa kutimiza wajibu wake.
Timu ya uchunguzi ya MTANZANIA Jumapili, ikitumia Kanda za urefu wa majengo kulingana na mpango wa uendelezaji upya wa eneo la kati la Dar es Salaam wa mwaka 2000 kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambao umeainisha ukanda wa maghorofa mafupi, ya kati na marefu, imebaini madudu ya kutisha.
Kwa mujibu wa mpango huo, ukanda wa kwanza baada ya ufukwe wa bahari unaotakiwa kujengwa maghorofa mafupi ambayo ni kuanzia sakafu (floor) tatu hadi sita, unajumuisha maeneo ya Kivukoni Front-Ocean Road, Ufukweni, Ali Hassan Mwinyi, Ohio, Ghana Avenue, Shaban Robert, Luthuli na Kivukoni Front (Ferry).
Hata hivyo, katika utafiti wake gazeti hili limebaini kuwa maghorofa yaliyojengwa katika ukanda huo yamezidi kiwango kilichowekwa kisheria.
Uchunguzi unaonyesha kuwa miongoni mwa maghorofa yanayodaiwa kukiuka sheria ni pamoja na lile lililo karibu kabisa na Ikulu, linalodaiwa kuishi watu wa Usalama wa Taifa, ambalo lina sakafu 18, badala ya sita zilizowekwa kisheria.
Mengine ni ghorofa la NIC Investment katika Barabara ya Samora, ambalo lina sakafu 15. Vilevile majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo yana sakafu 20.
Hata hivyo licha ya kuvunja sheria, Wizara ya Ardhi imetetea ujenzi wa Majengo ya BoT na Kilimanjaro Hotel ikisema kuwa yalipata kibali maalumu.
Uchunguzi unaonyesha kuwa ukanda unaoruhusiwa kisheria kujengwa sakafu saba hadi kumi ambayo ni upande wa pili baada ya ufukwe wa bahari, unajumuisha maeneo ya Shaaban Robert, Luthuli, Kivukoni Front, Azikiwe, Sokoine, Shaban Robert, Gerezani, Bibi Titi Mohammed, Maktaba/Azikiwe, Upanga, India, Nkrumah na Bibi Titi.
MTANZANIA Jumapili limegundua majengo mengi hayajazingatia mchanganuo huo, katika barabara hizo baadhi ya majengo kama Uhuru Heights barabara ya Bibi Titi lina sakafu 27, Viva Tower lina sakafu 21 kinyume na ilivyoonyeshwa katika mpango huo.
Pia Ghorofa la PSPF linajengwa sakafu 35, katika barabara ya Kivukoni, PPF lililopo makutano ya Barabara ya Ohio na Garden Avenue lina ghorofa 20, pamoja na Golden Jubilee Tower lenye ghorofa zaidi ya 21.
Wakati maeneo ya ukanda wa majengo yenye urefu unaozidi sakafu kumi na kuendelea ni barabara za Uhuru, Sokoine, Shaaban Robert, Ghana Avenue, Ohio, Bibi Titi, Maktaba/Azikiwe, India na Barabara ya Uhuru.
Katika uchunguzi wake, gazeti hili limebaini kuwa barabara hizo zinapatikana katika maeneo ya Mnazi Mmoja na Kariakoo.
Licha ya kuruhusiwa kisheria kujengwa sakafu kumi na kuendelea, lakini yamevunja sheria kwa upande mwingine, kwani umbali kati ya ghorofa moja na jingine ni mita tatu kushoto na kulia na mita tano nyuma.
Kwa kuzingatia utaratibu huo wa sheria, maghorofa karibu yote ya Mnazi Mmoja na Kariakoo hayafai na baadhi yake yanatakiwa yavunjwe.
Mbali na hayo, katika uchunguzi wake gazeti hili limebaini kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wakandarasi wenye majina makubwa kuchukua kazi na kuwapa wakandarasi wadogo ambao hutumia majina yao.
Hali hiyo imeelezwa na baadhi ya wakandarasi kuwa imechangia kwa kiasi kikubwa majengo mengi kujengwa chini ya kiwango.
Pamoja na hilo, wizi wa vifaa mbalimbali kama nondo na sementi unaofanywa na baadhi ya mafundi ujenzi, wakiwamo pia wakandarasi nao ni tatizo jingine ambalo linaweza kusababisha sekta ya ujenzi nchini kuanguka.
Itaendelea wiki ijayo…..
CHANZO:MTANZANIA
MY TAKE:KUWA MFUASI WA VYAMA VINGINE NI TICKET TOSHA YA KUPELEKWA MIREMBE!
MTANZANIA MMETIMIZA VEMA WAJIBU WENU KAMA CHOMBO CHA HABARI KWA KUANDIKA HABARI HII MUHIMU YA KIUCHUNGUZI.