Madudu CCM hayaupi hadhi upinzani kushika dola

Maendeleo huchagizwa na viongozi bora. Siasa nayo ndiyo huzalisha viongozi. Sentensi hizo mbili zinatosheleza ufafanuzi kuwa kama nchi zinahitajika siasa safi ili kupata matokeo mawili kwa mpigo; viongozi bora na maendeleo.

Inapotokea kwenye nchi kunakuwa na siasa ambazo hazikidhi hadhi ya kuitwa siasa safi, vyama na wanasiasa wanakosa misingi ya kujipambanua kwa ujenzi wa hoja, hapo matarajio huwa ya aina mbili kwa mkupuo; kukosa viongozi bora na maendeleo yenye unyoofu.

Zifahamu siasa za kigotcha (gotcha politics). Gotcha ni neno la Kimarekani ambalo limetokana na maneno mawili “got you”, yaani kunaswa au kukamatwa. Ukiambiwa gotcha maana yake ni got you, kwamba umenaswa. Gotcha politics ni siasa za kuviziana, kutafuatiana makosa ili kumkamata mpinzani wako. Siasa za ‘kipaparazi’.

Mwanasiasa anajikita kwenye kutafuta kasoro za mpinzani wake na kuzipigia mbiu ili zijulikane. Ndiyo maana siasa za kigotcha zikawa ni aina fulani ya siasa za kipaparazi. Husemi ubora wako ni nini mpaka upewe nchi, wewe unakazana kusema upungufu ya mwenzako.

Sawa, unaweza kusikika sawia kwa jinsi unavyochambua upungufu wa mwenzako, je, hiyo ndiyo sifa ya kukufanya upewe nafasi badala yake? Siasa za kutafuta kasoro ya mpinzani na kuipigia debe ijulikane inaitwa utapeli kwa sababu unautumia udhaifu wa mwenzako kama mtaji wa kisiasa.

Wananchi wanahitaji kukuona ulivyo bora ili wakuamini na wakuchague. Haitakiwi wakuchague kwa sababu wameona mwenzako amejaa kasoro. Unamfanya mwananchi akuchague akiwa hajui unakwenda kufanya nini katika uongozi wako.

Siasa za kuviziana hazijengi. Ni siasa za ulaghai. Viongozi bora hupambanuliwa na jinsi ambavyo wanajijenga kisiasa. Wanapambanua rangi zao na kuwaaminisha wananchi kisera, kifalsafa na kiitikadi.

Wanajiweka wazi kwa yale ambayo wanayapigania. Inakuwa rahisi kutabirika kuwa wakipewa mamlaka nini watafanya. Hizo ndizo hasa zinatakiwa kuitwa siasa safi. Siasa za kujipambanua kuliko kujificha kwenye mwavuli wa makosa ya wapinzani.

Tanzania inahitaji tiba

Siasa za kuviziana kuliko kujipambanua ndizo ambazo zinachukua nafasi kwa sasa chini. Chama Cha Mapinduzi (CCM) wapo tayari kuwekeza rasilimali zao kwenye kuutangaza upungufu wa wapinzani, kama ambavyo wapinzani wanavyokuwa wepesi kupigia debe kasoro za CCM.

Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii, hakuna siri tena kuwa CCM wana watu wao wa kushambulia na kutetea, kama ilivyo wapinzani. Nguvu kubwa inajikita kumtazama hasimu, kuchambua kasoro zake na ‘kuzibeba bango’ ili zifahamike kwa uwanja mpana.

Wale wa CCM, jukumu lao ni kutetea pale chama chao kinaposhambuliwa na kushupalia kasoro za wapinzani. Vivyo hivyo kwa wapinzani mitandaoni, wao ni kupiga mbiu kwenye ule udhaifu wanaouona CCM na kukosoa yote yanayofanywa. Wakikosa la kukosoa, wanaona bora wanyamaze kimya.

CCM wanayo majukumu mawili tu, kukitetea chama chao kisha kutazama kasoro za wapinzani wote na kuzisemea. Wao hawana rafiki kwenye upinzani. Kila chama cha upinzani wanapambana nacho kwa uzito sawa, inategemea na wakati husika.

Wapinzani wao wanayo majukumu mengi zaidi, kila chama kina watu wake wa kukitetea kisha kutazama kasoro za CCM na kuzishikia bango. Kazi nyingine ya vyama vya upinzani ambayo ni ngumu zaidi ni kutazama udhaifu wa wao kwa wao na kuupigia debe.

Mathalan, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinajielekeza kwenye upungufu wa ACT-Wazalendo, kama ambavyo ACT-Wazalendo kinavyoziona kasoro za Chadema kama mtaji wa kisiasa. Vita ya wapinzani kwa wapinzani.

Kabla ya kuwepo kwa muungano wa vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Chadema kilikishambulia Chama cha Wananchi (Cuf), kama ambavyo Cuf nacho kilivyokuwa kinayatolea macho na kuyasemea yaliyokuwa yanajiri ndani ya Chadema. Ilikuwa hivyo pia hata kwa NCCR-Mageuzi na Chadema.

Hili la wapinzani kushambuliana wao kwa wao limekuwa mtaji mzuri kwa CCM, maana ni kawaida hasimu wako anapokuwa na mahasimu mbali na wewe, kipindi ambacho anakong’otana na wengine, wewe unabaki unapumua, ukitazama mchezo unaishaje.

Ikiwezekana yule hasimu ambaye haguswi, hutazama mgogoro husika na kufanya uchochezi ili mapambano yaendelee. Vievile anaweza kuusaidia upande usio na madhara kwake au wenye hatari ndogo dhidi ya hasimu wake mwenye nguvu.

Ndege mpya na mgogoro Cuf

Sakata la ununuzi wa ndege mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATC) liliibua hoja za ushambulizi na utetezi. Kulikuwa na upondaji mkubwa kutoka kwa wapinzani, vilevile utetezi wa kiwango cha juu ulifanywa na vijana wa mtandaoni wenye kujipambanua kuwa wafuasi wa CCM.

Wapondaji hawakuwa na na kazi nyingine zaidi ya kuponda aina ya ndege zilizonunuliwa Bombardier Q400, kwamba hazina hadhi. Hawakuishia hapo walijenga hoja kwa historia ya ndege kubwa zilizowahi kununuliwa nchini lakini hivi sasa hazipo kutokana na sababu tofauti.

Hoja za wapondaji ziliingia mpaka kwenye kufananisha kuwa Tanzania kama taifa kubwa na lililo na utulivu wa katosha kwa miaka yake 55 ya Uhuru, inashindwa na Rwanda na Somalia zenye historia ya machafuko, vileveile ni nchi ndogo.

Kwamba mashirika yao ya ndege yenye kubeba bendera za taifa, RwandAir na Somali Air, yanamiliki ndege kubwa aina ya Boeing na Airbus zenye kubeba abiria mpaka 300, wakati ATC imenunua Bombardier Q400 yenye wastani wa kubeba watu 70.

Watetezi kwa kasi kubwa nao wakawa na hoja ya kwa nini imekuwa mwafaka kununua Bombardier Q400 badala ya ndege kubwa. Sababu nyingi walitoa kuhalalisha na kupongeza uamuzi huo ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliutekeleza wa kununua ndege hizo mpya.

Baadaye zilipoibuka taarifa kuwa mwakani kuanzia Machi, Serikali ina malengo ya kuinunulia ATC ndege kubwa aina ya Airbus, upande wa utetezi ambao ulisema mengi kuhalalisha uamuzi wa ununuzi wa Bombardier Q400, ukaibuka tena na sifa kemkemu kuhusu ujio wa Airbus.

Suala la ndege linavyoamsha hisia za mgawanyo wa pande mbili, zinakuja pia na namna ambavyo CCM wanavyofurahia mtifuano wa sasa ndani ya Cuf. Siyo uongo kuwa kuyumba kwa uongozi Cuf, kunatoa nafuu kubwa kwa CCM na Serikali yake, hususan Zanzibar.

CCM ni wanufaika wakuu wa mgogoro wa Cuf, maana endapo katika vuta nikuvute ya sasa, itakibakisha chama kwenye mikono ya Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba, maana yake majaliwa ya Ukawa yatakuwa shakani. Kuvunjika kwa Ukawa ni afya kwa CCM.

ACT-Wazalendo wanamtetea Lipumba. Kama ambavyo Chadema wanavyojiweka wazi kuhakikisha Lipumba habaki na chama. Utaona kuwa vuta nikuvute ya wapinzani wao kwa wao, inaipa ahueni CCM.

Cuf kikipasuka vipande viwili kama ambavyo dalili zinaonekana kwenda kutokea, ACT-Wazalendo wanaweza kunufaika kwa kupata wanachama ambao wataamua kujiunga nacho, Chadema na Ukawa, kuna mawili, kubaki na Cuf au watu.

Chadema na Ukawa wataweza kubaki na Cuf kama kitabaki chini ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na timu yake ya uongozi chini ya Julius Mtatiro. Hata hivyo, Chadema na Ukawa watavuna watu, kwa maana ya Maalim Seif, Mtatiro na timu yao, kama Profesa Lipumba atashinda vita ya uongozi kwenye chama hicho.

Matokeo yote yanayoendelea Cuf, mwisho kabisa ni sumu kali kwa upinzani. Hata kama baada ya dhoruba hakuna atakayejiunga na CCM, bado nguvu ya upinzani itakuwa imepungua.

Ubaya wa mwenzio si uzuri wako

Kuchunguzana na kuviziana ni siasa za umbea. Kuyasema mabaya ya mwenzako haikufanyi wewe uwe mzuri. Hili linatakiwa lifanyiwe kazi kubwa na wapinzani kuliko CCM. Maana CCM wana dola, wapinzani wanaifukuzia dola.

Si vibaya kuusema ubaya wa mpinzani wako lakini haipaswi kuwa agenda ya chama. Ubora wa chama hauwi katika kuibua dosari za chama pinzani, badala yake inatakiwa iwe kwa namna ambavyo kinajijenga kwa hoja endelevu. Kinavyojipambanaua kwa misingi yake ya kiitikadi na kifalsafa. Si hoja za kudandia.

Hii tabia ya wapinzani kujishughulisha zaidi na kasoro za CCM haina tija, maana hizo ni siasa za kipaparazi, kufuatiliana na kuumbuana, kwamba bila udhaifu wa mpinzani huwezi kujijenga. Hizo ndiyo siasa za kigotcha kama wasemavyo Wamarekani.

Wapinzani wakae na ukweli huu kuwa kuzijua na kuzisema sana kasoro za CCM, haziwapi hadhi na uhalali kwamba wanatosha kuongoza nchi, badala yake wajikite kwenye kuupambanua ubora wao kisha wafanye kazi ya kuwekeza itikadi na falsafa zao kwenye mioyo ya Watanzania. Kasoro za CCM zinapita, ndiyo maana leo litasemwa hili, kesho lile, lakini itikadi na falsafa vinadumu.

Maandishi Genius

Ndugu yangu Genius, asante sana kwa uchambumbuzi makini. Nilipoona ukubwa wa uzi wako, kasoro ni kate tamaa ya kuendelea kuusoma lakini umeandikwa kwa ubora wa hali ya juu na ukiwa umesheheni falsafa zaidi ya miparuro tuliizoea kwenye uwanja huu. Hongera sana.

Hata vyama vyetu havina falsafa zinazoweza kuvitofautisha. Mwanzoni CCM ilionekana na kutamka hadharani kuwa ni chama cha kijamaa, sasa haijulikani wanaelekea wapi?.

Chadema kilianza kutetea siasa za kibepari/ siasa za soko huru na kuonekana hadharani kupinga ufisadi na kulijimbikizia mali kiujanja ujanja, sasa sijui kama hilo linaendelea?.

Hakika tumekwama kama taifa, tumekwama kiuongozi na kwa bahati mbaya zaidi CCM sasa haitaki demokrasia. Hakuna anyeongelea katiba mpya, watetezi wa katiba ya Mzee Warioba sasa hawapo tena. Tumekwama, tumegota, tumenasa kwenye tope. Sasa hivi hakuna serikali ya chama cha mapinduzi kuna Serikali ya Mheshimiwa Magufuli, hakuna serikali imeamua, kuna nimeamua kumpa ardhi ekari elfu kumi bure, hakuna serikali itafuta hati, kuna nitafuta hati, nimeagiza arudishiwe sukari yake bila kuelezea kwanini ilizuiliwa. Tumekwama. Tumegiota, hakika tumenasa.
 
Kuhusu ufanyaji wa siasa za upinzani naona mapungufu kwenye hoja kuwa wapinzani kazi yao kubwa imekuwa kujadili mapungufu ya CCM peke yake. Wamekuwa pia wakiongea kile wangefanya na wakati huo huo wakisema mabaya ya watawala. Ndio maana umarufu wa Chadema umeongezeka mpiga kusababisha wazuiwe kuongea na wananchi moja kwa moja. Mfano mzuri ni wakati wa budget walitaka kujadili openly kuhusu mapungufu ya budget lakini wanyamazishwa kwa nguvu kubwa za dola. Kila kipimo kinaonyesha wafuasi wa upinzani wanaongoza.
 
Katika mfululizo wa makala makini ya Mwandishi mahiri Mtanzania Ndugu Luqman Maloto akichambua siasa za Tanzania. Pitia hii mada usiwe kama mkazi wa TANAPA kupitia Tiketi ya Lumumba ama Mkazi wa TANAPA kwa tiketi ya Ufipa:::::

Maendeleo huchagizwa na viongozi bora. Siasa nayo ndiyo huzalisha viongozi. Sentensi hizo mbili zinatosheleza ufafanuzi kuwa kama nchi zinahitajika siasa safi ili kupata matokeo mawili kwa mpigo; viongozi bora na maendeleo.

Inapotokea kwenye nchi kunakuwa na siasa ambazo hazikidhi hadhi ya kuitwa siasa safi, vyama na wanasiasa wanakosa misingi ya kujipambanua kwa ujenzi wa hoja, hapo matarajio huwa ya aina mbili kwa mkupuo; kukosa viongozi bora na maendeleo yenye unyoofu.

Zifahamu siasa za kigotcha (gotcha politics). Gotcha ni neno la Kimarekani ambalo limetokana na maneno mawili “got you”, yaani kunaswa au kukamatwa. Ukiambiwa gotcha maana yake ni got you, kwamba umenaswa. Gotcha politics ni siasa za kuviziana, kutafuatiana makosa ili kumkamata mpinzani wako. Siasa za ‘kipaparazi’.

Mwanasiasa anajikita kwenye kutafuta kasoro za mpinzani wake na kuzipigia mbiu ili zijulikane. Ndiyo maana siasa za kigotcha zikawa ni aina fulani ya siasa za kipaparazi. Husemi ubora wako ni nini mpaka upewe nchi, wewe unakazana kusema upungufu ya mwenzako.

Sawa, unaweza kusikika sawia kwa jinsi unavyochambua upungufu wa mwenzako, je, hiyo ndiyo sifa ya kukufanya upewe nafasi badala yake? Siasa za kutafuta kasoro ya mpinzani na kuipigia debe ijulikane inaitwa utapeli kwa sababu unautumia udhaifu wa mwenzako kama mtaji wa kisiasa.

Wananchi wanahitaji kukuona ulivyo bora ili wakuamini na wakuchague. Haitakiwi wakuchague kwa sababu wameona mwenzako amejaa kasoro. Unamfanya mwananchi akuchague akiwa hajui unakwenda kufanya nini katika uongozi wako.

Siasa za kuviziana hazijengi. Ni siasa za ulaghai. Viongozi bora hupambanuliwa na jinsi ambavyo wanajijenga kisiasa. Wanapambanua rangi zao na kuwaaminisha wananchi kisera, kifalsafa na kiitikadi.

Wanajiweka wazi kwa yale ambayo wanayapigania. Inakuwa rahisi kutabirika kuwa wakipewa mamlaka nini watafanya. Hizo ndizo hasa zinatakiwa kuitwa siasa safi. Siasa za kujipambanua kuliko kujificha kwenye mwavuli wa makosa ya wapinzani.

Tanzania inahitaji tiba

Siasa za kuviziana kuliko kujipambanua ndizo ambazo zinachukua nafasi kwa sasa chini. Chama Cha Mapinduzi (CCM) wapo tayari kuwekeza rasilimali zao kwenye kuutangaza upungufu wa wapinzani, kama ambavyo wapinzani wanavyokuwa wepesi kupigia debe kasoro za CCM.

Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii, hakuna siri tena kuwa CCM wana watu wao wa kushambulia na kutetea, kama ilivyo wapinzani. Nguvu kubwa inajikita kumtazama hasimu, kuchambua kasoro zake na ‘kuzibeba bango’ ili zifahamike kwa uwanja mpana.

Wale wa CCM, jukumu lao ni kutetea pale chama chao kinaposhambuliwa na kushupalia kasoro za wapinzani. Vivyo hivyo kwa wapinzani mitandaoni, wao ni kupiga mbiu kwenye ule udhaifu wanaouona CCM na kukosoa yote yanayofanywa. Wakikosa la kukosoa, wanaona bora wanyamaze kimya.

CCM wanayo majukumu mawili tu, kukitetea chama chao kisha kutazama kasoro za wapinzani wote na kuzisemea. Wao hawana rafiki kwenye upinzani. Kila chama cha upinzani wanapambana nacho kwa uzito sawa, inategemea na wakati husika.

Wapinzani wao wanayo majukumu mengi zaidi, kila chama kina watu wake wa kukitetea kisha kutazama kasoro za CCM na kuzishikia bango. Kazi nyingine ya vyama vya upinzani ambayo ni ngumu zaidi ni kutazama udhaifu wa wao kwa wao na kuupigia debe.

Mathalan, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinajielekeza kwenye upungufu wa ACT-Wazalendo, kama ambavyo ACT-Wazalendo kinavyoziona kasoro za Chadema kama mtaji wa kisiasa. Vita ya wapinzani kwa wapinzani.

Kabla ya kuwepo kwa muungano wa vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Chadema kilikishambulia Chama cha Wananchi (Cuf), kama ambavyo Cuf nacho kilivyokuwa kinayatolea macho na kuyasemea yaliyokuwa yanajiri ndani ya Chadema. Ilikuwa hivyo pia hata kwa NCCR-Mageuzi na Chadema.

Hili la wapinzani kushambuliana wao kwa wao limekuwa mtaji mzuri kwa CCM, maana ni kawaida hasimu wako anapokuwa na mahasimu mbali na wewe, kipindi ambacho anakong’otana na wengine, wewe unabaki unapumua, ukitazama mchezo unaishaje.

Ikiwezekana yule hasimu ambaye haguswi, hutazama mgogoro husika na kufanya uchochezi ili mapambano yaendelee. Vievile anaweza kuusaidia upande usio na madhara kwake au wenye hatari ndogo dhidi ya hasimu wake mwenye nguvu.

Ndege mpya na mgogoro Cuf

Sakata la ununuzi wa ndege mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATC) liliibua hoja za ushambulizi na utetezi. Kulikuwa na upondaji mkubwa kutoka kwa wapinzani, vilevile utetezi wa kiwango cha juu ulifanywa na vijana wa mtandaoni wenye kujipambanua kuwa wafuasi wa CCM.

Wapondaji hawakuwa na na kazi nyingine zaidi ya kuponda aina ya ndege zilizonunuliwa Bombardier Q400, kwamba hazina hadhi. Hawakuishia hapo walijenga hoja kwa historia ya ndege kubwa zilizowahi kununuliwa nchini lakini hivi sasa hazipo kutokana na sababu tofauti.

Hoja za wapondaji ziliingia mpaka kwenye kufananisha kuwa Tanzania kama taifa kubwa na lililo na utulivu wa katosha kwa miaka yake 55 ya Uhuru, inashindwa na Rwanda na Somalia zenye historia ya machafuko, vileveile ni nchi ndogo.

Kwamba mashirika yao ya ndege yenye kubeba bendera za taifa, RwandAir na Somali Air, yanamiliki ndege kubwa aina ya Boeing na Airbus zenye kubeba abiria mpaka 300, wakati ATC imenunua Bombardier Q400 yenye wastani wa kubeba watu 70.

Watetezi kwa kasi kubwa nao wakawa na hoja ya kwa nini imekuwa mwafaka kununua Bombardier Q400 badala ya ndege kubwa. Sababu nyingi walitoa kuhalalisha na kupongeza uamuzi huo ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliutekeleza wa kununua ndege hizo mpya.

Baadaye zilipoibuka taarifa kuwa mwakani kuanzia Machi, Serikali ina malengo ya kuinunulia ATC ndege kubwa aina ya Airbus, upande wa utetezi ambao ulisema mengi kuhalalisha uamuzi wa ununuzi wa Bombardier Q400, ukaibuka tena na sifa kemkemu kuhusu ujio wa Airbus.

Suala la ndege linavyoamsha hisia za mgawanyo wa pande mbili, zinakuja pia na namna ambavyo CCM wanavyofurahia mtifuano wa sasa ndani ya Cuf. Siyo uongo kuwa kuyumba kwa uongozi Cuf, kunatoa nafuu kubwa kwa CCM na Serikali yake, hususan Zanzibar.

CCM ni wanufaika wakuu wa mgogoro wa Cuf, maana endapo katika vuta nikuvute ya sasa, itakibakisha chama kwenye mikono ya Mwenyekiti, Profesa Ibrahim Lipumba, maana yake majaliwa ya Ukawa yatakuwa shakani. Kuvunjika kwa Ukawa ni afya kwa CCM.

ACT-Wazalendo wanamtetea Lipumba. Kama ambavyo Chadema wanavyojiweka wazi kuhakikisha Lipumba habaki na chama. Utaona kuwa vuta nikuvute ya wapinzani wao kwa wao, inaipa ahueni CCM.

Cuf kikipasuka vipande viwili kama ambavyo dalili zinaonekana kwenda kutokea, ACT-Wazalendo wanaweza kunufaika kwa kupata wanachama ambao wataamua kujiunga nacho, Chadema na Ukawa, kuna mawili, kubaki na Cuf au watu.

Chadema na Ukawa wataweza kubaki na Cuf kama kitabaki chini ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na timu yake ya uongozi chini ya Julius Mtatiro. Hata hivyo, Chadema na Ukawa watavuna watu, kwa maana ya Maalim Seif, Mtatiro na timu yao, kama Profesa Lipumba atashinda vita ya uongozi kwenye chama hicho.

Matokeo yote yanayoendelea Cuf, mwisho kabisa ni sumu kali kwa upinzani. Hata kama baada ya dhoruba hakuna atakayejiunga na CCM, bado nguvu ya upinzani itakuwa imepungua.

Ubaya wa mwenzio si uzuri wako

Kuchunguzana na kuviziana ni siasa za umbea. Kuyasema mabaya ya mwenzako haikufanyi wewe uwe mzuri. Hili linatakiwa lifanyiwe kazi kubwa na wapinzani kuliko CCM. Maana CCM wana dola, wapinzani wanaifukuzia dola.

Si vibaya kuusema ubaya wa mpinzani wako lakini haipaswi kuwa agenda ya chama. Ubora wa chama hauwi katika kuibua dosari za chama pinzani, badala yake inatakiwa iwe kwa namna ambavyo kinajijenga kwa hoja endelevu. Kinavyojipambanaua kwa misingi yake ya kiitikadi na kifalsafa. Si hoja za kudandia.

Hii tabia ya wapinzani kujishughulisha zaidi na kasoro za CCM haina tija, maana hizo ni siasa za kipaparazi, kufuatiliana na kuumbuana, kwamba bila udhaifu wa mpinzani huwezi kujijenga. Hizo ndiyo siasa za kigotcha kama wasemavyo Wamarekani.

Wapinzani wakae na ukweli huu kuwa kuzijua na kuzisema sana kasoro za CCM, haziwapi hadhi na uhalali kwamba wanatosha kuongoza nchi, badala yake wajikite kwenye kuupambanua ubora wao kisha wafanye kazi ya kuwekeza itikadi na falsafa zao kwenye mioyo ya Watanzania. Kasoro za CCM zinapita, ndiyo maana leo litasemwa hili, kesho lile, lakini itikadi na falsafa vinadumu.

Ndimi Luqman Maloto
 
Attachments

  • images.jpg
    images.jpg
    10.4 KB · Views: 29
Mbona hawataki Tume huru ya uchaguzi... Unafikiria CCM inashinda kwa haki.
 
Uchaguzi ni 2020......

Tungekuwa tunajadiri mambo ya msingi sasa.......

Kama katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.......

Hivi vingine ni siasa za kijinga tu.....
 
Ujinga upo wapi? Si kila jambo unalolichukia ama kutolipenda ni ujinga.
 
Back
Top Bottom